jaman tumsaidieni huyu amekata tamaa ya kuishi kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jaman tumsaidieni huyu amekata tamaa ya kuishi kabisa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Billie, Jan 20, 2012.

 1. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Jaman nimekosa raha ndugu wa baba wanadai eti mama yng mchawi anamloga baba hadi amekuwa mlevi mbwa pia kama anachanganyikiwa wameniita eti wanipe dawa ili wanipe dawa waliyopewa na waganga wao ili nimuwekee baba kwenye chakula nimeshindwa niwajibu nini nimeamua kumuomba ushauri mpenzi wangu hadi sasa hapokei simu yng tangu nimuelezee tatizo hili jumlisha na ugomvi uliopo nyumbani najikuta nashindwa hadi kusoma.
  Nimeombwa nimshauri huyu best wng mi nimeshindwa nimemuomba anipe muda nitulie (anasoma Environment engeneer mwaka 3 pale Ardhi) Hajui pa kuelekea,pia anachanganywa na situation ya mama yake kuambiwa mchawi na pia response ya mpenzi wake.TUMSAIDIE MAWAZO JAMAN.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Amweke mpenzi mbali sana kwanza , ili a'solve mambo ya familia yake!

  Hicho tayari ni kipimo cah upendo wao, kwahiyo wanadanganyana tayri hao!..hakuna penzi hapo!

  Hiyo dawa ya bila ridhaa ya mtu itafanyaje kazi?..kama ni sumu na mzee akafa mtajibu nini?
   
 3. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Ni serious jaman pia ni jiran yangu tunakaa mtaa mmoja mama yake ni msambaa baba ni mhehe Amenieleza kwa kirefu sana kuhusiana na tatizo lake mi nimelifupisha tu hivyo kama utakuwa una swali niulize na kama umeelewa tatizo tafadhali toa ushauri wako.ASANTEN
   
 4. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Kingine kinachomchanganya ni hilo swala kuikataa hiyo dawa yao watamchukuliaje au mshauri safe way ya kuikataa hiyo dawa.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Wanampa dawa ya kuzuia uchawi au dawa ya kuacha pombe?

  Kama ni dawa ya kuzuia uchawi wa huyo mke wake, SIAMINI katika dawa za kuzuia uchawi zaidi ya Imani yangu

  Kama ni dawa ya kumsaidia kuacha pombe, nimeshasikia ila sijawahi ona mtu aliyekunywa.
  Ila kuhusu Unywaji wa pombe kupita kiasi "alcoholism" kuna wataalam wa masuala hayo
  Ni ugonjwa kama magonjwa mengine bila msaada wa kitabibu ni ngumu kuacha.
  Mshauri cha kwanza, kama ni mkristu akaone mchungaji/padri

   
 6. piper

  piper JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Be consistent maana unajichanganya, mwanzoni umeandika kama vile we ndo ulokumbwa na swahibu hili ila baadaye ukasema ni rafiki yako, hao ndugu walimwona wapi anafanya uchawi? Beware of those who tell you about others!!!!!!!!!!!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Miafrika Ndivyo Tulivyo - Nyani Ngabu
   
 8. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Ni hivi hayo maelezo ndo alivyokuwa ananielezea na kuhusu uchawi ni kuwa ndugu zake na baba yake msichana walivyoona mabadiliko ya ndugu yao kama anachanganyikiwa wameenda kwa waganga na waganga wanasema eti analogwa na mkewe.
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  watampa sumu wamdanganye kuwa ni dawa. Asikubali.
   
 10. salito

  salito JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  yaan mwambie asikubali kabisa kuchukua dawa za ndugu zake,anachotakiwa kufanya n kufuat iman yake,kama muislam aite sheikh afanyiwe dua mfululizo atapata majibu 2,na pia asijethubut kumchukia mama yake,maan anaweza kukuta ni chuki 2 za mawifi na wakwe ndio zinawasumbua ndugu zake..
   
 11. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  aikatae hiyo dawa kwa technique gani?
   
 12. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Pole sana, pia achana na hizo Imani za kishirikina. Nilishawahi kupata case Kama hiyo ambayo ilikuwa na dalili nyingi ningeweza kuamini kweli. Nilipiga chini na kusimama kwa Imani yangu na Mungu.... Ni miaka mingi na bado nadunda.

  Ushauri wangu Kwako ' wache wafu wazike wafu wao'
   
 13. M

  MUHOJA-VENTURE Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo ndo utagundua ni jinsi gani sisi ni kizazi cha nyoka.Haimithiriki kwa mtu kuwa mgonjwa au kuwa mlevi halafu wanajamii wanaanza kushikana ulozi badala ya kushikana akili juu ya nini kifanyike ili muathirika arudie khali yake ya kawaida.
  Ushauri wangu:kwanza, huyo baba yetu anatakiwa apelekwe hospitalini kwa uchunguzi zaidi.Pili, aondoe fikra juu ya mama yake kuwa mchawi.Tatu,pamoja na kwamba huyo mpenzi wake hamfai, simshauri kuachana nae kwa mda huu kwani anaweza kuongeza tatizo jingine.Anachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kujitenga nae kwa mda ili ashughulikie suala la baba yetu.Plz,asikate tamaa ktk masomo.
   
 14. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Asante kwa ushauri wako mkuu Mungu akubariki.
   
 15. m

  manyusi JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  The only solution is to give your life to Jesus christ,biblia inasema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha asema Bwana wa majeshi,wakati mwingine tunajivisha mizigo isiyo yetu hao wanaokuita ukanywe dawa ndio wachawi wala si mama yako,kabidhi maisha yako kwa Yesu na yote hayo yatakuwa si kitu.Ubarikiwe
   
Loading...