jaman mi naombeni jibu la hili swali langu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

jaman mi naombeni jibu la hili swali langu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by yaser, Jun 30, 2012.

 1. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  sisi ni great thinkers km tunavyojipachika wenyewe haya majina.sasa basi mwenzenu naombeni mnijuze tofauti iliyopo kati ya FISADI anayefilisi nchi na kutuacha masikini na DAKTARI anayegoma na kuuwa watanzania walipa kodi wasio na hatia? Nipe mawazo yko kwa kadri uonavyo.
   
 2. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sijawahi kujua kwamba hivyo ndivyo waitwavyo wauaji.............
   
 3. M

  Mboerap Senior Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  naona bora ya fisadi maana yeye haondoi roho yako kuliko dkt anaengangania ml 3.5 kwa kuiweka rehani roho ya mgonjwa ambae pato lake la mwezi halifiki hata laki moja.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,056
  Trophy Points: 280
  Daktali ndio nani tena?
   
 5. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Napita tu. Hii ndio TZ kuliko uijuayo.
   
 6. F

  FELIPE Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Daktali ni nini? nenda shule.
   
 7. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hujatoa jibu umetoa porojo zko.hayo ni makosa tu yakiuandishi.
   
 8. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  we ndio mtanzania usiotaka kuelewa ukweli na kufuata matakwa ya watu flan
   
 9. D

  DoPe Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana tofauti wote ni sawa
   
 10. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi nafikiri bora Daktari kuliko FISADI LAFI.
  Sababu ni Kama kusingekuwa na Hilo FISADI anayefilisi nchi na kufuja Mali za Umma, haya matatizo ya Madaktari yasingekuwepo. Kwa kuwa wangekuwa wanapata mahitaji Yao na Wananchi kupata huduma bora za AFYA. FISADI hilo hilo likiumwa linaenda kutibiwa nje ya nchi!? Kwa kweli afadhali Madaktari mara trillioni moja. Ni mtazamo wangu binafsi.
   
 11. T

  Thadeus JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 267
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hivi ndugu zangu, kuna mtu anayeitwa serikali ambaye ameenda kutibiwa muhimbili? Wanaoenda kutibiwa kwanye hospital ambazo madaktari wamegoma ni wananchi ambao wangi wao hawana uwezo wa kwenda tumaini au aga khan, tena wangi wao ni wale walipa kodi ambao ndio wamelipia mafunzo ya hao madaktari. Pia wengi wao hawajawahi kukwepa kodi na kuweka hela kwenye mabenki uswisi.
   
 12. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,201
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  We mjibu swali lake, kakosea spelling sio kuwa huyu hajui au ni illiterate kwa vile kakosea spelling
   
 13. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Mkuu Thadeus,
  Unajua mambo na madai ya kimsingi ya hawa Madaktari!? Nimegundua kuna watu wengi au wachache hawajui hata Madai ya Madaktari yanahusu nini! Baadhi ya madai yao yanatugusa na kututetea sisi walala hoi. Serikali inapotosha ukweli na kufanya issue ionekane wanataka mishahara mikubwa na posho nene.

  Tuwe makini katika kusoma na kuchambua habari. Sio jirani akikuletea habari tu kamuona mkeo amesimama na muuza genge,ukifika nyumbani unaanza kumpa vibao mkeo bila kutafakari habari nzima.
  Madaktari wanadai Haki za kimsingi. Mafisadi wametuharibu akili zetu Watanzania,inafika muda tunaona ufisadi wao ni Jambo la kawaida..mpaka wanatumia lugha Kama VIJISENTI na sisi tunawakubalia.
   
Loading...