MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wakuu,
Mtaniwia radhi kuufikisha ujumbe huu humu badala ya ukumbi wa michezo na burudani kule, kwani binafsi naliona suala hili ni kwa maslahi ya kitaifa zaidi.
Kiukweli kabisa katika nchi yetu kwa suala la soka tumezidi kudidimia zaidi tumavyokwenda mbele kuliko tuliko toka kipindi alipowahi kunena Mzee rukhsa kua kwenye sualala soka Tanzania ni kama "kichwa cha mwendawazimu", ni dhahiri kabisa hatuna msaada wowote kwa viongozi wa shirikisho la soka nchini TFF, Kilichobaki ni watu kutengeneza mitandao ya kulindana kuendelea kufanya siasa ndani ya shirikisho bada ya kutenda kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo.
Bwana Jamali Malinzi Rais wa TFF ameshindwa kabisa kulinusuru soka nchini kama alivyojinasibu wakati wakati anafanya kampeni kugombea nafasi ya urais, watu wengi nikiwemo mimi tuliamini maneno yake na ari tukampigania kila kona kuhakikisha anakua kiongozi wa shirikisho lakini hatuoni cha maana anachofanya muda wote tangu aingie madarakani, Yaani ni bora hata Mara 100 ya uongozi wa Rais mstaafu Leodgar Chilla Tenga.
Tanzania tumeshindwa kusimamia ligi za ndani, ratiba za mechi zinapangwa hovyo hovyo hazina mwelekeo, matokeo yamelalamikiwa kupangwa mezani, vyama vya soka ninalalamikiwa kwa rushwa,viongozi bodi za ligi wanalalamikiwa kwa rushwa, maamuzi kutolewa pasipo ufafanuzi wa kuelewa uliowazi, adhabu kali kwa achezaji zisizoendana na makosa.
Ikumbukwe tu jana Tanzania imejitoa kuandaa mashindando ya shirikisho la shoka nchi washirika Afrika Masharaki CECAFA bila sababu ya msingi, ati moja ya sababu ni mwingiliano wa ratiba za mechi za kimataifa! Is this a sensible reason? Walikua wapi wakati wote? Kwani hawakujua kua kuna rariba za kimataifa? Na hili ndilo lililoharibu ratiba za ligi kuu Vodacom nchi kufikia shirikisho kulalamikiwa na kila klabu yampira.
Malinzi anatakiwa ajitathmini maana watanzia tunahitaji burudani na sio siasa kwenye soka.