Jamal Tamimu akikatwa jina CCM kwa mara nyingine Muhambwe mtapata shida

DINATALI

Member
Mar 30, 2021
8
2
Jina la bwana Jamal Tamim aliyeshinda kura za maoni za ubunge kupitia CCM jimbo la MUHAMBWE limekatwa,hivyo kuliacha jimbo hilo likiwa katika hati hati ya kuchukuliwa na wapinzani.

Bwana Jamal Tamim amekuwa akijitahidi sana katika shughuli za maendeleo na WANAMUHAMBWE wanalijua hilo, na amekuwa mvumilivu sana japo kuna genge la baadhi ya viongozi linaloonesha kumpiga vita.

karibu kila mara amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni ( kasoro mwaka jana ambako waliopiga kura walikuwa wajumbe wachache tu tofauti na miaka yote ambapo waliokuwa wakipiga kura ni wanachama wa CCM).

Wananchi wamekuwa wakimpenda na kumsikiliza sana hata mwaka 2015 wakati jina lake lilipokatwa kidogo kutokee vurugu, ikabidi awaombe wananchi kuwa watulivu na wavumilivu na akamuunga mkono MAREHEMU NDITIYE na kumsaidia!

Na hata HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI mwaka jana alimuambia BWANA JAMAL TAMIMU awe mvumilivu na kweli alisaidia kumpigia kampeni sana MAREHEMU NDITIYE na wala hakuonesha kukasirika.

Sasa mbunge NDITIYE kafariki, uchaguzi umefanywa na bwana JAMAL TAMIM aliombwa avumilie na MAREHEMU JOHN POMBE MAGUFULI.

sasa uchaguzi wa chama umefanyika na bwana JAMAL TAMIMU kashinda, kwa nini wanakata jina lake!? hawaoni watawawapa nafasi kina zitto aende kugombea MUHAMBWE na tupoteze jimbo!

 
CCM vumilieni, tunataka ilo jimbo achukue mpinzani, hasa Zitto ili kuleta umoja wa kitaifa!

huyo timamu atateuliwa kwenye nafasi nyingine!

natumaini umenielewa!
 
ccm vumilieni,tunataka ilo jimbo achukue mpinzani, hasa Zitto ili kuleta umoja wa kitaifa!
huyo timamu atateuliwa kwenye nafasi nyingine!
natumaini umenielewa!
Tatizo ni wanaMUHAMBWE kunyimwa HAKI YETU ya kuwa na kiongozi tumpendaye na tumtakaye kwa hivyo itabidi tu tumchague mwingine kwa sababu yule tunayemtaka hakupewa haki ya kushiriki, na bwana JAMAL TAMIMU inakuwa kama ananyimwa haki yake hata kama ni wewe ungejisikiaje!?

Bwana JAMAL miaka ya nyuma ametukopesha vijana boda boda nyingi sana tukawa tunalipa taratibu zimetupa ajira kweli na hapo hajawahi kuwa madarakani na amekuwa akitusaidia kwenye mambo mengi kiukweli kabisa ni mtu ambaye sisi huwa tunamuheshimu na kumpenda kwa juhudi zake zote kwa wananchi na hajawahi kuchoka miaka yote!

Zitto mwenyewe aliwahi kusema kuwa jimbo la MUHAMBWE kama wangempa JAMAL Hata yeye asingeenda kupiga kampeni dhidi yake kwa sababu anafahamau utendaji wake.
 
Pole sana, pasi na shaka wewe ni JAMAL SHAMIM
tatizo ni wanaMUHAMBWE kunyimwa HAKI YETU ya kuwa na kiongozi tumpendaye na tumtakaye kwa hivyo itabidi tu tumchague mwingine kwa sababu yule tunayemtaka hakupewa haki ya kushiriki, na bwana JAMAL TAMIMU inakuwa kama ananyimwa haki yake hata kama ni wewe ungejisikiaje ...
 
Kwani CCM ikipoteza Jimbo hill shida iko wapi..Mbona kabla ya kuvuruga uchaguzi wa mwaka jana CCM ilikuwa chalii.majimbo ya uchaguzi zaidi ya 90..so.hilo ngoja liendes upinzani ili Nchi tuendelee kupona
 
tatizo ni wanaMUHAMBWE kunyimwa HAKI YETU ya kuwa na kiongozi tumpendaye na tumtakaye kwa hivyo itabidi tu tumchague mwingine kwa sababu yule tunayemtaka hakupewa haki ya kushiriki,

Bwana JAMAL miaka ya nyuma ametukopesha vijana boda boda



mbona haueleweki mkuu, mnataka kumlipa fadhila Bw Jamal kwa kuwa aliwanunulia bodaboda?
 
Haya mpeni kura za maruhani
IMG-20210330-WA0131.jpg
IMG-20210330-WA0130.jpg
 
mbona haueleweki mkuu, mnataka kumlipa fadhila Bw Jamal kwa kuwa aliwanunulia bodaboda?
wewe ndio hueleweki soma mwanzo mpaka mwisho mbona unachukua vitu nusunusu na mbona hauongelei suala la kuambiwa na HAYATI MAGUFULI kuwa avumilie ingekuwa ni mtu asiyefaa hata HAYATI MAGUFULI asingemwambia avumilie!
 
Ndiyo umeamua ujipigie pande Ndugu?
pande gani mechi imeshaisha,
tunachoonesha hapa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za wananchi kuwekewa mgombea wasiyemtaka,kuhusu maamuzi walishafanya wanavyojua wenyewe lakini wanavunja wanaCCM mioyo na hilo jimbo upinzani watachukua kama mchezo
 
Back
Top Bottom