GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nje ya uwanja chanzo chetu cha kuaminika kimebaini kuwa viongozi wa timu ya Geita Gold Sports, walitoa kiasi cha shilingi milioni 6 za kitanzania kwa viongozi na benchi la ufundi la timu ya JKT Kanembwa kwa ajili ya kupanga matokeo ya mchezo wa Februari 13 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
Athumani Ninja, ambaye ni katibu msaidizi wa chama cha mpira wa miguu Manispaa ya Kigoma Ujiji,siku ya mchezo majira ya saa 13:20 alionekana katika Hoteli mpya ya Green View iliyoko Mji Mwema mjini Kigoma, mahali ambapo viongozi wa Geita Gold Sports walikuwa wamefikia na kuonana na viongozi hao.
Haikujulikana mara moja sababu za kiongozi huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha makocha wa mpira wa miguu cha mkoa wa Kigoma, kuonana na viongozi hao ingawa chanzo chetu kilitia shaka mpango ambao baadaye ulikuja kuonekana wakati wa mchezo huo.
Ndani ya uwanja wachezaji wa JKT Kanembwa baada ya kubaini kuwa wamepunjwa kwa kupewa shilingi laki moja na nusu kila mmoja wakati viongozi wamepewa milioni 6 haikuwaingia akilini hivyo walipoingia mchezoni walikaza hivyo hadi mapumziko Geita Gold Sports walikuwa mbele kwa magoli 2-0 pekee.
Wakati wa mapumziko Athumani Ninja alikwenda upande wa Kanembwa na kuongea na wachezaji ambao walidai kuwa hawakubaliani na kiwango cha pesa waliyopewa vinginevyo mpaka pesa iongezwe ambapo baada ya hapo Athumani Ninja aliyekuwa playmaker kwenye saga hilo alikwenda upande wa pili wa Geita Gold Sports wakakubali kuongeza kiasi cha shilingi milioni mbili.
Hatua hiyo ilionesha kufanikisha malengo ya Geita Gold Sports, kwani magoli kipindi cha pili yalianza kumiminika kama mvua golini kwa timu ya JKT Kanembwa. Pia kulikwa na mawasiliano ya kila nukta baina ya viongozi wa Geita Gold Sports na watu wasiofahamika waliokuwa uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo kulikuwa na mchezo kati ya Polisi Tabora na JKT Oljoro.
Haikushangaza ukisikia Polisi Tabora wakiongeza goli na huku Geita wanaongeza goli, ukisikia kipa wa Polisi Tabora yuko chini kaumia na huku Lake Tanganyika kipa wa Geita Gold Sports kaumia ambapo kuna wakati alipelekwa chooni ambapo alikaa kwa zaidi ya dakika 20.
Hata hivyo ilibainika baadaye kuwa kulikuwa na mgawanyiko miogozi mwa wachezaji wa Kanembwa. Wakati mchezo wa Tabora ukiwa umemalizika na Polisi Tabora kupata ushindi wa magoli 7-0, mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa na Geita Gold Sports, Salehe Mang’ola kutoka Dodoma, ambaye aliboronga katika mchezo huo, aliwapa Geita penati isiyostahili.
Baadhi ya wachezaji Kanembwa waligomea penati hiyo na kutokea mvutano mkubwa uliodumu kwa zaidi ya dakika 20, na kwamba kama mwamuzi angezingatia sheria za mpira tungeweza kusema mchezo umevunjika jambo ambalo lisingekuwa na faida kwa Geita Gold Sports.
Wakati wa mvutano huo Athumani Ninja muda wote alionekana akizunguka kila kona ya uwanja na kuonekana akiwasiliana na baadhi ya wachezaji waliokuwa vinara katika mpango wa kupanga matokeo ambapo mara kadhaa aliskika akiwauliza wachezaji hao “Vipi bhana”.
Kitendo cha Athumani Ninja kiliwaudhi mashabiki waliofika kuangalia mchezo huo akiwemo mchezaji wa zamani Wastara Baribari ambaye nusura azichape na Athumani Ninja kabla ya askari polisi waliokuja mwishoni mwa mchezo huo wakisaidiana na askari mmoja wa Jeshi la Wananchi kuamua ugomvi huo.(picha tunayo).
Ikumbukwe kuwa Athumani Ninja hana nafasi yoyote katika timu ya JKT Kanembwa, bali ana ushawishi mkubwa kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kutokana na kufahamiana nao kwa muda mrefu.
Huku mchezo wa Polisi Tabora na JKT Oljoro ukiwa umemalizika, Geita Gold Sports, walikuwa wakihitaji goli moja ili kutimiza malengo yao, hivyo kwa vyovyote vile ilikuwa ni lazima penati hiyo ipigwe, kwa hiyo baada ya mvutano wa muda mrefu iliongezwa tena shilingi milioni moja na ndipo hapo wachezaji wa Kanembwa walikubali kuendelea na mchezo na penati ikapigwa na baada ya penati kupigwa mwamuzi akamaliza mchezo.
Tofauti na matarajio ya wengi baada ya mchezo huo viongozi wa Geita Gold Sports walikuwa na furaha isiyo ya uhakika, bali walionekana muda mwingi wakiongea na simu kama ilivyokuwa wakati wa mchezo.
Baadaye Athumani Ninja alisikika akisema tena bila hata chembe ya aibu kuwa walikuwa wakilipa fadhila kwa Geita Gold Sports, bila kubainisha fadhila hizo.
Kama asemavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: “Hiyo ndio Tanzania” nasi tunaongezea kuwa hiyo ndio TFF ya Jamali Malinzi.
Attachments area
Preview attachment RIPOTI MAALUM KUTOKA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA.docx
RIPOTI MAALUM KUTOKA MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA.docx
Taarifa Yote Hiyo Ni Kwa HISANI Ya Mtandao Wa Michezo Wa SHAFII DAUDA.