Jamal Khashoggi: Trump Asema Hatasikiliza Mkanda Wa Mauaji, Amtetea Bin Salman

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amejuzwa kuhusu mkanda wa sauti wa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi lakini amesema binafsi hatousikiliza.

"Ni mkanda wa maumivu, ni mkanda mbaya," Trump ameiambia runinga ya Fox News. Shirika la ujasusi la Marekani CIA linaaminika kufikia kikomo kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman aliamrisha kutekelezwa kwa maujai hayo, japo bado Ikulu ya White House haijathibitisha uchunguzi huo.

_104393970_1fa3a4fb-d472-45f8-8cbf-1cc6b7268199.jpg

Saudi Arabia imeziita taarifa hizo za CIA kuwa ni za uongo na kudai kuwa bin Salman hakuwa na taarifa yoyote juu ya kutekelezwa kwa mkasa huo.

Khashoggi, alikuwa ni kinara wa kuukosoa utawala wa kifalme wa Saudia. Aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul Oktoba 2 alipoenda kuchukua karatasi zake za talaka. Saudia inasema aliuawa katika operesheni haramu iliyotekelezwa na maafisa wake wa usalama.

Hata wanaomuunga mkono Trump ndani ya Bunge la Wawakilishi wanamtaka achukue hatua kali juu ya mauaji hayo. Lakini kutokana na unyeti wa Saudia kama mshirika thabiti wa Marekani katika Mashariki ya Kati kunamfanya Trump kuwa mgumu katika kufanya maamuzi.

Trump amesema hana haja ya kusikiliza sababu ameshaelezwa juu ya maudhui ya mkanda huo. "Ninafahamu kila kitu kilichomo ndani ya mkanda bila hata ya kuusikiliza," aliiambia Fox katika mahojiano yaliyorushwa jana Jumapili Novemba 18. "Iikuwa ni vurumai, uovu mkubwa na mbaya sana." Mkanda huo ambao unatajwa kuwa ni ushahidi mkubwa wa tukio hilo umesambazwa na Uturuki kwa Marekani na washirika wake.

Katika mahojiano hayo, Tump amesema Mohammed bin Salman amemwambia kuwa alikuwa hajui lolote juu ya mpango na kutekelezwa kwa mauaji hayo. Trump amedai kuwa yawezekana isijulikane kabisa nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo, hata hivyo amesema tayari kuna vikwazo vimeshawekwa juu ya wale wanaoshukiwa kutekelza uovu huo. "Lakini wakati huo huo tunaye mshirika na mimi nataka nishikamane na mshirika ambaye kwa namna nyingi tu amekuwa mwema," amesema Trump. Hata hivyo, mahojiano ya Trump na Fox yalifanyika kabla ya kuvuja kwa ripoti ya CIA.

Japo CIA hawakutoa ushahidi wa moja kwa moja juu ya uhusika wa bin Salman kwenye mauaji hayo, maofisa wa shirika hilo wanaamini tukio kama hilo lisingeweza kufanyika bila ruhusa yake. Jumamosi, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema haijafikia hitimisho juu ya mauaji hayo, ikisema kuna maswali mengi ambayo hayajapata majibu.

Jana Jumapili Trump amesema serikali yake lazima ifanye maamuzi. "Tutakuwa na ripoti kamili ndani ya siku mbili, yawezekana Jumatatu au Jumanne," amesema Trump.

Chanzo: BBC
 
trump hataki kusikia kwa sababu wana mkataba mnono na saudi arabia juu ya kuuziana siraha ni makataba wa mabilioni ya pesa
 
kuna issue ya doolar mabilioni ya silaha hapo ila MUNGU anamuumbua sana Trump,maupumbavu anayofanya angefanya obama sijui ingekuwaje,kisa alikuwa half black damu ilikuwa inawachemka akifanya mistake ndogo,kama kipindi aliposhindwa kurudisha salute kwa marine because alikuwa na coffe cup mkononi Trump alipiga kelele kwamba anadharau wanajeshi lenyewe juzi limeshindwa hata kwenda kwenye cemetery za veteran wa ww 1 and 2 kusingizia mvua
cha kushangaza wasiofatilia politics za US kama buku ya lumbumba hapa ndani wanamuona jamaa ni bonge la leader
trump.PNG
 
Huyo Trump nae anatuzungusha tu. Kipindi kile alisema baada ya wiki 2 atatoa tamko ambalo hadi leo kimya,jana baada ya kuona moto umewaka tena kasema ataongea baada ya siku 2 ambazo bado inaniwia vigumu kuamini kama atasema lolote la maana (vikwazo juu ya MBS) ambavyo ndivyo hasa tunavyotaka kusikia tulioumizwa na unyama huu.

Hili tukio linadhihirisha unafiki wa Marekani. Hawajawahi kujali chochote zaidi ya maslahi yao.
 
Huyo Trump nae anatuzungusha tu. Kipindi kile alisema baada ya wiki 2 atatoa tamko ambalo hadi leo kimya,jana baada ya kuona moto umewaka tena kasema ataongea baada ya siku 2 ambazo bado inaniwia vigumu kuamini kama atasema lolote la maana (vikwajo juu ya MBS) ambavyo ndivyo hasa tunavyotaka kusikia tulioumizwa na unyama huu.

Hili tukio linadhihirisha unafiki wa Marekani. Hawajawahi kujali chochote zaidi ya maslahi yao.
kuna deal kubwa la silaha almost 200 b dollars ,na miaka yote republicans ndo michezo,Trump ni mafia liloko pale kwa ajili ya pesa tu
 
kuna issue ya doolar mabilioni ya silaha hapo ila MUNGU anamuumbua sana Trump,maupumbavu anayofanya angefanya obama sijui ingekuwaje,kisa alikuwa half black damu ilikuwa inawachemka akifanya mistake ndogo,kama kipindi aliposhindwa kurudisha salute kwa marine because alikuwa na coffe cup mkononi Trump alipiga kelele kwamba anadharau wanajeshi lenyewe juzi limeshindwa hata kwenda kwenye cemetery za veteran wa ww 1 and 2 kusingizia mvua
cha kushangaza wasiofatilia politics za US kama buku ya lumbumba hapa ndani wanamuona jamaa ni bonge la leader
View attachment 939529
Duh!
 
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amejuzwa kuhusu mkanda wa sauti wa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi lakini amesema binafsi hatousikiliza.

"Ni mkanda wa maumivu, ni mkanda mbaya," Trump ameiambia runinga ya Fox News. Shirika la ujasusi la Marekani CIA linaaminika kufikia kikomo kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman aliamrisha kutekelezwa kwa maujai hayo, japo bado Ikulu ya White House haijathibitisha uchunguzi huo.

View attachment 939453

Saudi Arabia imeziita taarifa hizo za CIA kuwa ni za uongo na kudai kuwa bin Salman hakuwa na taarifa yoyote juu ya kutekelezwa kwa mkasa huo.

Khashoggi, alikuwa ni kinara wa kuukosoa utawala wa kifalme wa Saudia. Aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul Oktoba 2 alipoenda kuchukua karatasi zake za talaka. Saudia inasema aliuawa katika operesheni haramu iliyotekelezwa na maafisa wake wa usalama.

Hata wanaomuunga mkono Trump ndani ya Bunge la Wawakilishi wanamtaka achukue hatua kali juu ya mauaji hayo. Lakini kutokana na unyeti wa Saudia kama mshirika thabiti wa Marekani katika Mashariki ya Kati kunamfanya Trump kuwa mgumu katika kufanya maamuzi.

Trump amesema hana haja ya kusikiliza sababu ameshaelezwa juu ya maudhui ya mkanda huo. "Ninafahamu kila kitu kilichomo ndani ya mkanda bila hata ya kuusikiliza," aliiambia Fox katika mahojiano yaliyorushwa jana Jumapili Novemba 18. "Iikuwa ni vurumai, uovu mkubwa na mbaya sana." Mkanda huo ambao unatajwa kuwa ni ushahidi mkubwa wa tukio hilo umesambazwa na Uturuki kwa Marekani na washirika wake.

Katika mahojiano hayo, Tump amesema Mohammed bin Salman amemwambia kuwa alikuwa hajui lolote juu ya mpango na kutekelezwa kwa mauaji hayo. Trump amedai kuwa yawezekana isijulikane kabisa nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo, hata hivyo amesema tayari kuna vikwazo vimeshawekwa juu ya wale wanaoshukiwa kutekelza uovu huo. "Lakini wakati huo huo tunaye mshirika na mimi nataka nishikamane na mshirika ambaye kwa namna nyingi tu amekuwa mwema," amesema Trump. Hata hivyo, mahojiano ya Trump na Fox yalifanyika kabla ya kuvuja kwa ripoti ya CIA.

Japo CIA hawakutoa ushahidi wa moja kwa moja juu ya uhusika wa bin Salman kwenye mauaji hayo, maofisa wa shirika hilo wanaamini tukio kama hilo lisingeweza kufanyika bila ruhusa yake. Jumamosi, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema haijafikia hitimisho juu ya mauaji hayo, ikisema kuna maswali mengi ambayo hayajapata majibu.

Jana Jumapili Trump amesema serikali yake lazima ifanye maamuzi. "Tutakuwa na ripoti kamili ndani ya siku mbili, yawezekana Jumatatu au Jumanne," amesema Trump.

Chanzo: BBC

Unafiki wa Marekani hapa ndo huwa unaonekana wako radhi kumsupport na hata kumlinda dhalimu yeyote wenye maslahi naye , shenzi sana hili Taifa
 
kuna issue ya doolar mabilioni ya silaha hapo ila MUNGU anamuumbua sana Trump,maupumbavu anayofanya angefanya obama sijui ingekuwaje,kisa alikuwa half black damu ilikuwa inawachemka akifanya mistake ndogo,kama kipindi aliposhindwa kurudisha salute kwa marine because alikuwa na coffe cup mkononi Trump alipiga kelele kwamba anadharau wanajeshi lenyewe juzi limeshindwa hata kwenda kwenye cemetery za veteran wa ww 1 and 2 kusingizia mvua
cha kushangaza wasiofatilia politics za US kama buku ya lumbumba hapa ndani wanamuona jamaa ni bonge la leader
View attachment 939529

Trump fala sana huyo mbwa ,
 
Back
Top Bottom