Jamal Khashoggi Atajwa Kuwa Mtu Mwenye Ushawishi Zaidi Kwa Mwaka 2018

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Jarida la Time limemtunuku Jamal Khashoggi na waandishi wengine duniani kuwa watu wenye ushawishi kwa mwaka 2018.

1544564078963.png


Waandishi waliouawa na kufungwa jela, wametajwa kuwa kama watu walio na ushawishi mkubwa zaidi kwa mwaka 2018 na jarida maarufu la Time.

Jarida hilo limetoa ukurasa wa mbele wa aina nne tofauti kwa heshima ya waandishi waliokumbana na madhila mbalimbali mwaka huu kutokana na kazi zao.

Kati ya hao yupo Jamal Khashoggi aliyeuawa Oktoba 2 ndani ya ubalozi wa Saudia Arabia jijini Istanbul, Uturuki.

Wengine niwaandishi wa Capital Gazette, jarida la nchini Marekani ambapo waandishi watano waliuawa, pamoja na Maria Ressa kutoka Ufilipino na Wa Lone na Kyaw Soe Oo kutoka nchi ya Myanmar.

Jarida la Time limesema limewachagua hao "kutokana na kuingia kenye dimbwi kubwa la hatari kwa kuusaka ukweli mkubwa, kwa kunyanyua sauti zao".

Jamal Khashoggi alikuwa mwandishi maarufu na kinara wa kuikosoa serikali ya kifalme ya Saudia. Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Watu wengi katika jamii ya kimataifa wanaamini Mauaji hayo yaliamuriwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.

Khashoggi alikimbilia nchini Marekani akihofia maisha yake mwaka jana. Akiwa Marekani alikuwa akiandika makala kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo aliendeleza harakati zake za kumkosoa Mohammed bin Salman. Alienda Istanbul kushughulikia mchakato wa ndoa na mchumba wake wa Kituruki.

Rais wa Marekani Donald Trump amejaribu kuukingia kifua utawala wa Saudia na bin Salman. Shirika la ujasusi la CIA linadaiwa kuhitimisha kuwa bin Salman alihusika kwenye mauaji, japo Trump alidai kuwa CIA hawakutoa hitimisho hilo. Lakini maseneta wa Marekani wanaamini kuwa mwanamfalme huyo alihusika.

BBC: Jamal Khashoggi atajwa kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2018
 
Back
Top Bottom