Ziroseventytwo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 7,971
- 13,605
Kuna jamaa ya yangu anatarajiwa kuingi theater kesho kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji utakao ondoa jicho lake 1. Nimeumia sana. Atafanyiwa upasuaji kesho kwenye hospitali ya mt Fransis hapa ifakara. Madaktari wamemweleza kuwa jicho lake limekufa.
Jamaa aliumia kama siku 10 zilizopita baada ya kukwaruzwa na kijiti kwenye shughuli zake za kivuvi. Kilichonifanya niilete hii thread hapa ni muda na aina ya tiba aliyopewa. Kwa maelezo ya mgonjwa alipewa dawa ya kuweka kwenye jicho ya matone. Na dawa ya kupunguza maumivu. Jana hali yake ikabadilika akidai kuwa anasikia maumivu makali. Leo hii kaja haspitalini hapa na madoctor wamemwambia kuwa jicho limekufa na linatakiwa litolewe.
Sina uhakika kama hii hospitali ina vipimo vizuri kwa ajili ya macho.
Jicho mpaka litolewa linatakiwa liwe katika hali gani.? Nina mpango wa kwenda kumshauri akatae maana muda na aina ya tiba alizopata kwa maana ya dawa si nzuri.