Jamaa kajitosa zoo aliwe na simba akidai mwisho wa dunia umefika

mxyo16

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
1,243
758
Insikitisha kwakweli, ameokolewa na simba walioanza kumla waliuwawa. aliingia kwenye jumba la simba akavua nguo na kuwadandia baadae akachenjiwa, kwenye nguo zake kimekutwa kikaratasi-suicide note; kwamba mwisho wa dunia umefika kwa hiyo anajiwahi ana miaka 20, inaonekana alikua muumini maana alikuwa akimtaja yesu walioshuhudia wamesema nchini Chile.
=====================
Simba wawili wameuawa na walinzi wa hifadhi ya wanyama nchini Chile wakati walijaribu kumuokoa mwanamme mmoja ambaye alivua nguo na kisha kuruka kwenda kwa hifadhi walimokuwa simba hao.

Mwanamme huyo wa umri wa miaka 20 alijeruhiwa vibaya baada ya kuingia kwenye hifadhi hiyo ya simba na kuanza kuwachokoza simba akitaka wamshambulie.

Walinzi wa hifadhi walijibu kwa kuwafyatulia risasi simba hao walipoanza kumshambulia na kuwaua wote wawili.

3479986600000578-0-Zoo_keepers_killed_the_lions_to_save_the_man_who_was_gravely_inj-a-20_1463869446077.jpg


3479D2C500000578-3602819-image-m-3_1463872898888.jpg


3479987A00000578-0-A_20_year_old_man_took_off_his_clothes_and_broke_into_a_lion_enc-a-19_1463869433771.jpg


maxresdefault.jpg
 
Hao Simba bora ni wa zoo wangekuwa wale original wa Serengeti angekuwa maiti in fraction of second
 
Yaani Simba wenyewe wanajua huyu Chizi na hawezi kula nyama ya Chizi.
Wanamzingua na wao,angekuwa na akili timamu akateleza ndio angejua show yao
 
Simba wa ulaya kama wanaume wa DSM.
Hahahha sky eclat wanaume wa dar hawali binaadam....hahaha watu na research zenu bana. Ila tukumbuke tu kwamba dar ina wanaume wa makabila mengi sana ya mikoani....kusini kaskazini magharibi mashariki na kati pia. Sky wewe wa mkoa gani
 
Hahahha sky eclat wanaume wa dar hawali binaadam....hahaha watu na research zenu bana. Ila tukumbuke tu kwamba dar ina wanaume wa makabila mengi sana ya mikoani....kusini kaskazini magharibi mashariki na kati pia. Sky wewe wa mkoa gani
Wewe simba aone nyama aanze kuiromance kwanza,wale simba wa Serengeti? Hao kama wanaume wa DSM wala chips mayai.
 
ana bahati simba walikuwa hawajakata kachumbari la sivyo leo ingekuwa nyama choma festival kwa simba
 
Back
Top Bottom