Jamaa anayo ndoa halali, lakini haachi kulala kona...kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamaa anayo ndoa halali, lakini haachi kulala kona...kulikoni?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msindima, Apr 9, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mpenzi msomaji, vipo vituko vingine ukisimuliwa unapata kizunguzungu. Unajiuliza hivi kweli Ndivyo Maisha Yalivyo au ni watu wanabuni staili yao ya maisha mfano wa yale ya `kufikirika` tuliyojifunza zamani?

  Leo nianze moja kwa moja kukumegea kisa kimoja nilichosimuliwa hivi majuzi ambapo mabwana wawili walijikuta waking’ang’ania kuzika mwanamke ambaye kila mmoja alidai ni mkewe kwa kuwa walizaa naye.

  Rafiki yangu mmoja ananisimulia kisa cha kaka wa rafiki yake ambaye japokuwa alikuwa ameoa ndoa kubwa ya kikristo, lakini nadra alikuwa akilala nyumbani na muda mwingi aliutumia kwa mwanamke mwingine anayedai kuzaa naye mtoto kabla ya ndoa.

  Kwa mhutasari msomaji wangu ni kwamba, yupo baba mmoja aliyefunga ndoa ya kuvunja na shoka, tena mwanamke wa kumchagua mwenyewe. Maisha yakawa mazuri na yaliyojaa furaha na hata kujaliwa kupata mtoto.

  Mara baada ya kuzaliwa mtoto huyo, mume akaanza vituko. Mara anarudi amechelewa nyumbani huku akiwa amelewa chakari. Wakati mwingine anapitiliza anarejea asubuhi.

  Mama anapouliza kulioni, jamaa anakuja juu akimtishia kuwa kama amechoka kumvumilia anaweza kufungasha virago.

  Wakati mwingine mume huyu akirejea hamgusi kabisa mkewe kwa madai kuwa amechoka sana na majukumu ya nje. Mke akawa anajiuliza haya majukumu ya nje yanayoathiri majukumu ya ndani ni ya namna gani?

  Huku na huko bwana yule akawa anachoshwa na maswali aulizwayo na mkewe. Siku moja akamwambia mkewe ajiandae kwani anamtoa outing kujiburudhisha kwenye hoteli kubwa.

  Mke akajawa na furaha tele, japo kwa mashaka kuwa iweje leo apelekwe outing ilhali haijawahi kutokea?
  Naam. Wakaondoka na kutua hoteli moja nzuri.

  Wakakaa nje kwenye bustani nzuri. Wakaagiza vinywaji. Punde jamaa akamkonyeza mwanamama mmoja aliyekuwa tayari ameketi jirani na pale walipokuwa wameketi.

  Mwanamama yule akasogelea meza akaketi na kumchangamkia vilivyo bwana huyu. Kisha bwana akamtambulisha mkewe kwa mwanamama yule.

  ``Umekuwa ukiniuliza kwanini wakati mwingine sirudi nyumbani, basi leo nimemaliza mzizi wa fitna kwani huwa najichimbia kwa mchuchu wangu huyu, ndiye sabuni yangu ya roho na leo nakutambulisha rasmi kuwa ni mke mwenzio.

  Inasemekana kuwa mke wa baba huyu alipata kigugumizi na wala hakuweza kusema lolote mbali na kunyanyuka na kuondoka zake.

  Japokuwa aliletwa kwa gari na mumewe, alichukua teksi na kurejea nyumbani huku akiwaacha wapenzi wale wakitumbua vyao.

  Inaelezwa kuwa alipofika nyumbani alifungasha virago na kwenda kulalamika kwa wakwe zake kuhusu jinsi mumewe anavyomfanyia visa vya kumkatisha tamaa.

  Kikao cha wazee na washenga kilikaa na kumsihi bibie arudi kwa mume kwani hakuna sababu ya kuukimbia mji wake.

  Mpenzi msomaji, hivi ndivyo vitimbi vya baadhi ya kinababa ambao wamezipiga kisogo nyumba zao za ndoa na kuonja vya pembezoni ambavyo wakati mwingine ni viroja vitupu.

  Kwa mujibu wa simulizi toka kwa rafiki yangu, ni kwamba bwana yule kabla ya kufunga ndoa, alikuwa akiishi na mama yule aliyemtambulisha kwa mkewe wa ndoa na tayari alishazaa naye mtoto.

  Na kwamba mama yule kabla ya kuwa na mahusiano na baba huyu, alikuwa ameolewa na bwana mwingine ambaye waliachana baada ya kuzaa naye watoto wawili ambao ni wasichana wakubwa sasa.

  Kimbembe kingine kilizuka pale mama yule aliyetambulishwa alipougua na bahati mbaya mauti yakamkuta.

  Mvutano ukajitokeza nani atamzika mama huyu? Ni yule mumewe wa kwanza aliyezaa naye watoto wawili wakaachana au ni baba huyu mwenye ndoa yake aliyezaa naye mtoto mmoja?

  Baba wa watoto wawili akasema angependa kumzika mzazi mwenzie na baba huyu mwenye ndoa akadai hivyo hivyo kuwa lazima amzike kwa kuwa yule mume wa mwanzo alimwacha wakati yeye alizaa na marehemu na wala hakuwa amemuacha.

  Mwishowe ikaamuliwa bwana huyu wa pili amzike lakini iwe kwenye makaburi ya serikali. Yote hayo yakafanyika na mvutano ukaisha.

  Jamaa sasa bado moto unawake nyumbani. Baada ya msiba ule ndiyo bwana huyu akazidi kumvuruga mkewe ili aondoke. Ikafikia wakati badala sasa ya kulala kona anakuja na vimwana nyumbani na kulala navyo bila aibu.

  Pia wale watoto wawili wa marehemu ambao baba huyu anadai kuwa alikuwa akiwasomesha, sasa akawaruhusu kuja kuishi pale nyumbani.

  Mama mwenye nyumba akawa na mzigo wa usumbufu toka kwa mumewe na karaha pia toka kwa watoto wale ambao katu walikuwa hawamheshimu mbali na kumdharau.

  Mama kuona maji yamemfika shingoni akaamua sasa kufungasha moja kwa moja. Wala hakwenda kwa wakwe akaamua kwenda kuanza maisha.

  Ajabu ni kwamba bwana yule baada ya kujua anakoishi mama mtoto wake huyu, akawa anamtuma hausigeli kumletea chakula mwanae kwa maelezo kuwa japokuwa amemuacha(yeye mke), lakini mwanaye bado anahitaji matunzo ya baba. Upo hapo msomaji wangu?

  Naam. Inaelezwa kuwa baba huyu amekuwa hovyo, tangu wakati huo hajaoa mwanamke mwingine mbali na kuokota huyu, mara yule na kuwaoa kwa muda kisha kuwatosa.

  Je, haya ni maisha gani katika wakati huu dunia inapambana na dhuruba za maisha yaliyoghubikwa na maradhi, mengine yasiyotibika?

  Haya ndiyo maisha ambayo kinamama wengi wanafurahia pale wanapoolewa lakini hawajui huko mbele kuna nini. Kwa kabila la Wachagga upo msemo kwamba “Samanya ekesonguo pfho’ ikimaanisha kuwa mara nyingi mtu hawezi kung’amua jambo kabla.

  Laiti mwanamama angejua kabla kwamba bwana huyu huko aendako atamtesa au atamwacha na kadhalika, si ajabu angemkwepa mapema.

  Lakini katika maisha hakuna ajuaye na mara nyingi mtu hujitosa ili mradi tu kampenda fulani kwa dhati hivyo kusubiri liwalo huko mbele ya safari. Na hakika, Maisha Ndivyo Yalivyo.

  Hata hivyo, ni muhimu kwa wenzetu kinababa kuwa wakweli na wawazi pale mwanzoni.

  Mwambie mwenzio kabisa kwamba nakuoa lakini tayari nina mwanamke mwingine katika mazingira fulani. Mpe nafasi ya kuamua kuolewa nawe baada ya kuwepo mahusiano hayo au kuamua kumtafuta mwingine.

  Hiyo itamsaidia yule aliyeamini kuwa ndiye pekee ndani ya mkataba ajue yuko na mwenzake mwingine.

  Lakini anapotambulishwa mwenzake baada ya kuingizwa ndani, huu ni usaliti usioweza kufutika kirahisi. UKWELI ni dhana muhimu katika maisha yetu ya sasa. Hilo lazima sote tulikubali na kulizingatia.

  KWA STAILI HII KWELI TUTAPONA?
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh hapo ndipo ninapochoka kabisa hivi wanaume mmepewa haki hiyo ninyi kuwaumiza wenzi wenu. Yaani ningekuwa ni mimi huyo mama..................
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mhh sis, kuna dada mmoja tunafanya nae kazi jengo moja, alikuwa na bfrnd wake, kumbe huyo mkaka ana mdada mwingine, huyu binti anashangaa kuckia bfrnd wake anaoa na alitegemea muolewaji angekuwa yeye coz ni bfrnd wa miaka nenda rudi, mwanaume kaoa na kumaliza haruc karudi kwa huyu mdada 2naefanya nae humu na wanaendelea na ufrnd wao kama kawaida, sasa najiuliza huyu dada anafikiria nini kichwani kwake, bfrnd aliekuwa anamtegemea amuoe kaoa mtu mwingine kabisa tena alijitahidi kufanya cri but ikavuja, huyu dada akachukua na likizo, alipungua sana wakati huo nadhani mawazo ya hiyo haruc ya ghafla, sasa amemrudia wa nini, na ni mdada ambaye anasumbua ndoa ya huyu mkaka kweli, mke wa mkaka ndio ana mimba ya miezi kadhaa, na yeye ni kulia tu mana mwanaume rudi yake nyumbani ni asubuhi, unajiuliza alioa ili iweje?na huyu mdada alimrudia ili iweje kama alimwaga na kuona mwingine?haaa mie kushoka kabisa na haya mambo.
   
 4. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ``Umekuwa ukiniuliza kwanini wakati mwingine sirudi nyumbani, basi leo nimemaliza mzizi wa fitna kwani huwa najichimbia kwa mchuchu wangu huyu, ndiye sabuni yangu ya roho na leo nakutambulisha rasmi kuwa ni mke mwenzio.""


  hapo pamenitoa machozi, kweli uvumilivu unahitajika sana.
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Sometimes men look like crazy!

  Halafu hii inatokana na BAD COMPANY,wanaume wana tatizo moja...............akipata kampani ya 'A WOMANIZER',na yeye atakuwa hivyo tu.kuliepuka hilo wanaume wenzangu ni bora mkajitune kuwapenda wake zenu
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Msiwalaumu sana wanaume angalieni na nyie wanawake kwa nini mnadanganyika kirahisi?
  Kuna wengine wanatahadhalishwa kabisa huyu jamaa moto wa kutea mbali utasikia mwanamke anasema ooh mnanionea geleeeeeeee haya sasa utajuuuuuuuuuuuuuuuta kuolewa na jamaa mpenda kicheche. Fanyeni utafiti sio mnakurupuka tu eti kwa vile jamaa ana Prado sijui Bajaj na hana mke basi wewe unaona umepata mwanaume.....Mtamegwa sana na kuachwa shauri zenu.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Asilimia 99 ya wanaume ni cheaters!!!! Wapo wanaofanya hayo hadi wake zao au girl friends wanagundua (hii ni asilimia kubwa) kuna ambao wanafanya ila ni kwa siri yaani wanajitahidi wenza wao wasijue kabisa. Yaani mambo yote ni mchanaa kweupe, yaani taarifa ya habari saa 2 usiku haimkuti nje, yupo home na anakula dinner na family. Sasa hawa wanaitwa the silent killers. Hapa mke/girlfriend anajisahau akijua kuwa mume/kiboy wake ni innocent tena utasikia akimtetea mbele za watu kuwa "yaani mume/jamaa yangu mimi hana mwanamke ni mimi tu". Onyo usiusemee moyo wa mwanaume/mwanamke. Wakati wote ishi kwa tahadhari.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  BAELEZEE!.........naona umeamua kuwatolea uvivu!hii ni KWA YOYOTE ANAEHUSIKA


  MH!......MAKUBWA!anyways,LONGA MWANAMUMEEEEEEEE


  lakini pia tusije tukautumia udhaifu wa mwanamke kutoziheshimu ndoa NA AFYA ZETU
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni nini kinasababisha uzaifu wa mwanamke?
  Udhaifu wa mwanamke uko wapi?
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Dada ndio huyu naye kituko na ndio hawa hawa wanaofanya wanawake tuonekane mwalimu wetu kipofu asa karudi kufanya nini? Au yake ya dhahabu
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  swity we wacha tu yani unafikiria huyu huko kichwani anawaza nini mpaka anajiachia kihivyo, unakosa jibu.
   
 12. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duh huu uzi umenikumbusha mbali!
   
Loading...