Jamaa anataka atumie nguvu za giza kupata mke

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,269
40,054
Kuna jamaa yangu mmoja alikuja kunipa changamoto yake kwenye mahusiano; anasema kuna mrembo mmoja amempenda, na huyo mrembo anafanya kazi za ndani kwa tajiri mmoja.

Huyo rafiki yangu alimfahamu huyo mrembo, kutokana na tajiri wa huyo binti kumtuma huyu kijana mara kwa mara kupeleka mzigo hapo nyumbani. Ndipo jamaa akamuona huyo mrembo na hatimaye kuanzisha naye mawasiliano kwa njia ya simu.

Jamaa akawa ameoza kwa huyo binti, halali vizuri kutokana na kumuwaza huyo binti atampata lini. Misele ikawa haipungui kumtembelea huyo binti, mpaka tajiri wa binti akaja kushtukia jamaa ana mahusiano na mfanyakazi wake.

Jamaa ikabidi afunge safari mpaka kwa wazazi wa huyo binti huko mkoani, akaenda kujitambulisha pamoja na kuelezea dhamira yake ya kutaka kumuoa huyo binti. Wazazi walimpokea vizuri mshikaji, na akiwa huko huko wazazi wakafanya mawasiliano kwa tajiri wa binti yao.

Tajiri wa binti yao alifoka sana, kwa nini jamaa ameenda kwao kwa binti bila kumshirikisha yeye; Kwa mtazamo wa jamaa, anahisi tajiri amekuwa mkali kwa kuhisi kupungukiwa nguvu kazi iwapo jamaa atamuoa huyo binti. Kwani huyo binti amekaa zaidi ya miaka 5 kwa huyo tajiri.

Mbaya zaidi, wazazi hawana sauti, binti naye amepewa maneno mengi ya uongo kuhusu huyo jamaa; kwa sababu binti amebadilika na kumuambia huyo jamaa ana watoto wengi nje, mara anamwambia hana mapenzi ya kweli n.k

Jamaa hakuchoka, akatuma mshenga, na walipofika kwa wazazi, wazazi wakataka milioni 4.5 kama mahari. Jamaa akijicheki, ana uwezo wa kutoa milioni 1.5. Jamaa kama amechanganikiwa, ameoza kabisa kwa binti.

Sasa jamaa, anajaribu kujipanga lakini anaona ngumu kufikisha hiyo hela. Sasa ameamua atumie mbinu zingine za kivita, za kumuoa huyo binti kwa gharama ndogo.

Anataka aende kwa mtu wa kisomo (dua), amrushie maruani yule binti, ili yule binti amfuate jamaa, ampe ujauzito ili mambo mengine yaendelee.

Swali wakuu: Hizo dua huwa zinafanya kazi kwenye mazingira hayo?
 
Maake hapo kwanza...😃😃😃

Oya hata kwa ndumba lazima aolewe mtu

Ila mambo yakivunda ndo ujue umelala yooo..😂😂
 
Huyo jamaa yako / wewe anaangaika na nini wakati mchawi ni pesa?

Labda kama ana sura mbaya sana au
Mfupi sana au mchafu chafu.

Tofauti na hapo hakuna uchawi unaouzidi pesa.



Tamaa ya pesa ndio huwaponza wanawake wengi na wengine sio tu kuachwa njiani bali kuwagharimu hata maisha kama kina swalha!

Tuwege tunajifunza kupitia matukio ya wengine kwenye jamii.

Mwanamke tafuta hela yako mwenyewe kwa jambo na akili yako ya Mwanaume iwe ya nyongeza au ziada!
 
Back
Top Bottom