Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.

Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.

Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."

Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"

Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.

Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.

Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."

Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"

Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."

Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"

Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"

Nikasema,
"Sawa"

Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.

Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH

ushauri wenu tafadhali
Acha huo upuuzi we mwanao utakubali akae miaka minne yote uchumba tuh kuolewa ni heshima na baraka mwache mtoto wa watu aolewe huyo muuni alikua anampotezea muda tuh kwan tunayo mifano mingi mtaan uchumba miaka kumi afu mtu haji kuoa huyo mtu
 
Eti utoke kufanya kazi ua utendaji tarafa kama anavyosema japo ni afisa tarafa, kwenda kufanya kazi sheli ..... daaaaa hatari sana. Kwa usawa huu utoke serikalini uende sheli? Ambayo siku 2 tatu unafukuzwa.

Anyway tumetofautiana
Yaan mie napatwa na mashaka kwa maelezo ya OP, dogo anahudumia familia ya mwanamke ipasavyo, anamuhudzmia mkewe kwa gharama za juu na kiwango, sasa inakuaje ke na wazaz wake wamkubali huyo jamaa mwingne? Hapa km sio ushirikina bas kna namna ipo.

Mie nimewaza kitu flan ila ngoja nitazame tyuuh hii ngoma lol.
 
Sijajua.,
Ila Ndo alkua alituambia sisi watu wake wa karibu katika stori maana Kuna kipind watu walimtania Sana mazingira ya ukwen kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmmmmh kiukweli wee muulize vizuri dogo kuna jambo lipo katkat ya huyo mwanamke na huyo dogo ambalo nyie wengine hamlijui, ndo lililozua haya yote. Serious yaan
 
Wale wazazi wake Ni wapumbavu,
Na inaonekana msemaji mkubwa was ile familia Ni mama mtu.

Mzee wao namuona Kama zimeruka ruka Kias flan, ana upole flani hivi wa kizoba zoba.

Tangu uyo binti kaenda kutolewa mahali kwao alikwenda na uyo mdg wake na hawajarudi wote kule Hadi leo Hii.



Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuuh kwa style hii Dunia haitaishiwa maajabu lol.
Vipi au huyo rafiki yenu B ndo ana mkwanja kumzidi dogo?
Maan inashangaza mno hii situation lol
 
Acha huo upuuzi we mwanao utakubali akae miaka minne yote uchumba tuh kuolewa ni heshima na baraka mwache mtoto wa watu aolewe huyo muuni alikua anampotezea muda tuh kwan tunayo mifano mingi mtaan uchumba miaka kumi afu mtu haji kuoa huyo mtu
Pia hili lipo sana.
 
Aisee!
Squid%20Game%201.jpg
 

DeepPond

Acha kujisumbua mkuu, inaonekanwa hujawaelewa wanawake bado.
Wanawake hawana mapenzi na mwanamme, wanawake hujiegeza kwa mwanaume kwa ajili ya maslahi ya malengo yake tu, nayo ni either
Pesa
Kuolewa
Kugongwa
Show of
kupata Msaada wa aina yoyote ule ukiwa wa kwenye masomo au kazi au hata kusaidiwa kushonewa nguo kwa haraka bila ya kusumbuliwa na mshoni.

Anapokosa kutimiza malengo yake kwako lazima atatafuta plan B na kukukimbia. Na siku zote yeye atakaua na thousand words ya kujitetea kujifanya hayupo hatiani.

Mwamabie mskaji wako a move on, na wale huyo mshkaji mwengine msitengeneze nae bifu kwa ishu za hawa viumbe.

KIla unapozidi kukua ndipo unapoanza kuwaelewa hawa viumbe.
 
Mara nyingi mwanamke hudate na mwanaume anayempenda lakin huolewa na mwanaume aliye tayar kuoa.
 
Mkuu DeepPond nalizungumza hili kwa sababu nimelipitia mwaka jana mwishoni, kama mdogo wako. Kwa hiyo ushauri wangu unaweza ukawa ni ushauri mzuri kwa mdogo wako.

"Huyo mwanamke hata kama atakubali kurudi kwa mdogo wako, mdogo wako ataonekana dhaifu kwa sababu ameshindwa kuendelea bila huyo mwanamke."

Cha msingi mwambie huyo dogo aondoke hata hapo Dar kama mpo Dar, aende mkoa mwingine akatulize akili kwanza. Mwambie kwamba kama kuumia akubali kuumia tu, kwa sababu ataumia sana itafika sehemu hataumia tena. Wazungu wanasema kulia ni ku "Let it all out" haswa kama ulimpenda sana mpenzi wako. Kwa hiyo kama analia si kitu cha ajabu kila mtu analia anapokumbwa na sintofahamu.

Cha msingi awe mvumilivu na akishamtoa moyoni amini kwamba hatakuja kuumizwa na mapenzi tena. Vilevile mshauri ajipe muda mrefu hata two years wa kuwa single na asipoteze muda kutafuta mwanamke mwingine kwa haraka.

Hii kitu watu wanachukulia utani lakini hawajapitia scenario kama hii. Cha msingi kutowaamini watu sana ulimwengu umebadilika, tusipende kuweka matarajio makubwa sana wa watu ama vitu. Madhara yake ndiyo haya.
Nawe ilikuaje mkuu? Tupe kidogo
 
Ajidhuru kwa kipi sasa?yaani mwanamke kaondoka mwenyewe katoa chupi huko kanogewa kaamua kuhamia kabisa halafu dogo ajidhuru kweli??atakua mpumbavu Nambari moja kumtia hasara mamake kwa nyege za mtu mwingine
 
Uwezekano wa kuendelea kimapenzi kati ya dogo na huyo mwanamke ni mkubwa sana baada yakusoma UPDATE. Hayo ndio madhala ya uchumba wa muda mrefu mmoja kuachwa nakubaki na maumivu.
Chamsingi dogo a move on tu, atampata mwengine watakayeishi kwa raha mustarehe.
 
Miaka 4 mingi unakaa na mtu husomeki wacha akaolewe zake, oooh sijui amalizie nyumba sijui nini kwani angemuoa asingeishi huko aliko, mwanamke aliona upepo hausomeki akaona ajiongeze. Ushauri kama mwanaume uko na mdada unaona kabisa anafaa kuoa basi muoe haraka sio kumpotezea miaka 4 ilihali kuna watu wanakutana 6 months na wanaoana. Amuache
Mwenzie alowe
 
Kwa namna huyo bint alivyo kujibu, kuwa uyo B sijuh tangu Zaman sijuh nini nini. Ukitazama ni kwamba walikuwa kwenye penzi muda tuu hao watu.

Hapo usikute tayari sijuh Wame peana ad mimba so Wana oana ili mambo Yao yaende..

Mwambie dogo aaachane na uyo bint akilazimisha uyo bint ndio itakuwa mlango wake wa kifo
 
Ni jamaa zangu wawili wameingia katika SINTOFAHAMU kubwa sana kwasababu ya mwanamke,

Nmewaza hapa mpaka kichwa kinaniuma sahivi.

KWA KUANZIA,
Ni kwamba mimi pamoja na hao jamaa zangu wawili sote Ni wafanyabiasha wa bidhaa Aina Moja.
Ofisi zetu ziko jirani pia (mji ule ule), Mara kwa mara husafiri pamoja kufata Mzigo, husaidiana hapa na pale mmoja wapo anapokua amekwama n.k

Kiukweli, Kwa sasa wote Tumekua marafiki Tena zaidi ya ndugu maana ukaribu wetu una mwaka wa 10 na zaidi Sasa.

Mimi na brother (Namuitaga brother coz katupita wote kiumri) wote tumeoa .

Ila Dogo wetu uyu
(tunamwitaga dogo coz wote tunamzidi kiumri) hajaoa bado ila ana mchumba wake wakike wamedumu miaka 4 Sasa na alkua alkua anategemea mwakani afunge nae ndoa baada ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake ya kuishi na familia.

Kama unavojua marafiki watatu tuloshibana miaka na miaka huamua kuziunganisha familia zetu pamoja na mwaka Jana mwezi Kama huu Tuliunganisha familia zote 3 (mimi na familia yangu, brother na familia yake, Dogo na mchumba wake) tukaendelea wote tukapanda gari Moja kwenda kutalii pamoja MIKUMI na kurudi pamoja.

Boxing day ya mwaka huu nayo tulipanga itukute wote SERENGETI tukaenjoy na familia zetu.

KILICHOTOKEA JANA,
Nikiwa njian asbh naelekea bank, nkapita ofsin Kwake nkaona pamefungwa.

Wakat wa mchana Tena narudi nkaona bado pamefungwa,

Ikabid nimpigie
"vipi dogo mbona ofsin ufungui leo ndugu yangu?"

Dogo akanambia anamatatizo makubwa , Kama naweza niende nyumban kwake,
Anamaongezi na Mimi na kuna kitu kinamchanganya Sana kichwani anajihisi anatamani TU aage dunia.

Nilipofika akaanza kinisimulia,
" kaka Mchumba wangu wa miaka yote J kanisaliti, wiki ijayo ni ndoa yake anaolewa na mtu mwingine, Na keshalipiwa mahali tayar".

Dah! Moyo ulienda mbio Sana sikuamini maneno Yale.

Nkamwambia
"Acha masihara wewe, iyo haiwezekan"

Akasema
"wee kama huamini mpigie rafiki yake wa karibu Mama P akwambie kila kitu maana mimi kila nikipiga simu yangu hapokei, nilipomtafuta shoga Ake mama p ndo kanieleza kila kitu"

Basi nikaendelea hewan kumcheki uyo mama p,
Kwa maelezo ya mama p

"Shemeji Mimi mwenyewe mwanzoni sikuamini nilichokiona, J.pili ilopita shoga angu J alinialika kua analipiwa mahali nihudhurie shughuli yake, nikajua rafiki ako ndo atakua anahusika.
Nilifika tukapika na kumpamba mwali kwa ajili ya ugeni wa washenga kuleta mahali nikastuka kuona mhusika Ni rafiki yenu B"

"Kwaiyo Mimi sijui Nini kinaendelea nikajua masihara, Ila baadae mashehe wakachoma ubani na Dua mbalimbali na Dua ikawa ni kuombea baraka uchumba wa B na J"

Dah! Wakuu ,
Kiukweli moyo ulistuka sana, nikawaza mambo mengi Sana tuloshea na Kaka etu uyu.
Inawezekanaje kaka B amuoe J wkt Ni shemeji yake kabisa Yule na wanaheshimiana Sana.

Inakuaje kuaje amfanyie mwenzetu ishu Kama hiyo.

Basi inabidi nimkatie uyu mdada simu nikampigia uyu brother etu Kama ni kweli hizi habar.

Jamaa bila hata hofu akanambia,
"Hizo habari Ni kweli, J namuoa mimi na amekubali kabisa kusilimu na atakua MKE wangu wa pili."

Nkamwambia,
"Brother Unakosea sana, uyo Ni mchumba wa Dogo uyo na wewe unalifahamu Hilo na Wana mwaka wa 4 huu Sasa"

Akasema,
"Kaka Mimi mambo yao hayanihusu, nnachojua washaachana nakwasasa nnachojua Mimi na J ndo tunapendana na mahali nishalipa tayar. Na ndoa Ni mwezi huu mwishoni. Kama mnaweza nisapoti sawa kama hamtapata nafasi haina shida ntalimaliza TU mwenyewe"

Nkamwambia,
"Brother Unakosea Sana, wee sio wa kumfanyia hivyo Dogo, ukzingatia Dogo ndo alkua anamtegemea uyo awe MKE wake wa Kwanza maishani mwake, na wewe Umeshaoa tayari na unajua kila kitu khs Hawa madogo tangu mwanzoni"

Akasema,
"Kaka , sahivi Mimi Sina MDA wa kulijadili hili, Kama Kuna malalamiko Basi amlaumu mwanamke wake maana yeye ndo anataka kuolewa na Mimi. Na Mimi Sina tatizo na Hilo. Mchana mwema Kaka, kuna mahali nawai."

Kisha akakata simu.

Dah!
Kiukweli Maneno Yale yaliniumiza Sana.

Dogo nahisi yalimuumiza zaidi mpaka akawa anabubujikwa na machozi pamoja na kamasi utadhani mtoto mdogo maana simu ilikua loudspeaker MDA ule.

Sahivi
Nmewaita jamaa zetu wengine wawili waje hapa kwa Dogo wamuweke sawa, maana Hali nnayomuona nayo asijekaa peke Ake akajidhuru.

Nmeaga naenda kufunga Ofisi narudi tukae nae kufikirie tunamshaur vipi kuhusiana na ili.....

USHAUR WENU kwenye hili Ni muhimu Sana wakuu,

Natanguliza shukran
Kaa mbali na huyo bloo atakutombeaa mkeo,sio mtu mzuri huyo
 
Back
Top Bottom