Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,090
Kuna miradi mikubwa mitatu (Signature projects) ambayo JK aliamua kuizindua mwishoni mwa utawala wake.
Miradi hiyo ni
1. Mwendokasi DSM
2. Daraja la Kilombero
3. Hospitali ya Benjamin William Mkapa iliyoko ndani ya Campus ya chuo kikuu cha UDOM
Miradi yote hii, JK aliizindua kuelekea mwishoni mwishoni kabisa mwa utawala wake.
Ninajua kuwa Documents zipo za kuonyesha kila mradi umeanza upembuzi yakinifu lini, kuanza ujenzi lini, na kukamilika lini lakini nilichogundua ni kwamba raia hukumbuka zaidi mmaliziaji kuliko mwanzilishi.
Na kwa kweli kwa maoni binafsi siyo makosa kwa mtawala kujivunia yale aliyowafanyia wananchi. Kwa mfano hata JPM atakapoondoka madarakani tutamsifu na kumshukuru sana kwa SGR na Stieglers maana kwa kweli ni miradi ya maana.
Lakini najaribu kuimagine, kama JPM angeamua kwenda na plan ya mwanzo ya kuzalisha umeme kupitia gesi yetu ya mtwara au angeamua kwenda na mpango wa awali wa kujenga SGR kupitia mkopo wa EXIM bank ya wachina ambao tayari serikali ya JK ilishakuwa kwenye mazungumzo na serikali ya China ingekuwa vipi?
Nilichojifunza kwa yaliyomkuta hayati raisi wetu BWM ambaye kwa hakika aliifanyia nchi hii mambo makubwa ila hakupenda kupigia promo kazi zake ukilinganisha na utawala huu ambao ukijenga hata stendi ya mabasi basi promo inakuwa kubwa kweli kwa kweli nampongeza JK kwa kuamua kuizindua ile miradi yake ya mwishomwisho ili ujenzi uanze au pale ilipokuwa imekamilika kuizindua yeye mwenyewe la sivyo kuna watu ambao wangekuta chakula kimeshainjikwa jikoni au kimeshatengwa mezani kufanya ugawaji tu, na sasa kwa kuwa wao ndo waliowagawia watoto basi wangeonekana eti wao ni wa maana zaidi kuliko wale waliokitafuta na kukipika!.
Aliyemshauri JK hata kuchukua helcopter na kwenda shutashuta kuzindua ujenzi wa Daraja la Kilombero alimpa mzee wetu ushauri wa maana sana!