Jakaya Kikwete ulifanya la maana kuzindua mwenyewe miradi yako ya mwishoni mwishoni, la sivyo Watanzania wasingejua ukweli

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,197
2,000
Kuna miradi mikubwa mitatu (Signature projects) ambayo JK aliamua kuizindua mwishoni mwa utawala wake.
Miradi hiyo ni

1. Mwendokasi DSM
2. Daraja la Kilombero
3. Hospitali ya Benjamin William Mkapa iliyoko ndani ya Campus ya chuo kikuu cha UDOM

Miradi yote hii, JK aliizindua kuelekea mwishoni mwishoni kabisa mwa utawala wake.

Ninajua kuwa Documents zipo za kuonyesha kila mradi umeanza upembuzi yakinifu lini, kuanza ujenzi lini, na kukamilika lini lakini nilichogundua ni kwamba raia hukumbuka zaidi mmaliziaji kuliko mwanzilishi.

Na kwa kweli kwa maoni binafsi siyo makosa kwa mtawala kujivunia yale aliyowafanyia wananchi. Kwa mfano hata JPM atakapoondoka madarakani tutamsifu na kumshukuru sana kwa SGR na Stieglers maana kwa kweli ni miradi ya maana.

Lakini najaribu kuimagine, kama JPM angeamua kwenda na plan ya mwanzo ya kuzalisha umeme kupitia gesi yetu ya mtwara au angeamua kwenda na mpango wa awali wa kujenga SGR kupitia mkopo wa EXIM bank ya wachina ambao tayari serikali ya JK ilishakuwa kwenye mazungumzo na serikali ya China ingekuwa vipi?

Nilichojifunza kwa yaliyomkuta hayati raisi wetu BWM ambaye kwa hakika aliifanyia nchi hii mambo makubwa ila hakupenda kupigia promo kazi zake ukilinganisha na utawala huu ambao ukijenga hata stendi ya mabasi basi promo inakuwa kubwa kweli kwa kweli nampongeza JK kwa kuamua kuizindua ile miradi yake ya mwishomwisho ili ujenzi uanze au pale ilipokuwa imekamilika kuizindua yeye mwenyewe la sivyo kuna watu ambao wangekuta chakula kimeshainjikwa jikoni au kimeshatengwa mezani kufanya ugawaji tu, na sasa kwa kuwa wao ndo waliowagawia watoto basi wangeonekana eti wao ni wa maana zaidi kuliko wale waliokitafuta na kukipika!.

Aliyemshauri JK hata kuchukua helcopter na kwenda shutashuta kuzindua ujenzi wa Daraja la Kilombero alimpa mzee wetu ushauri wa maana sana!
 
kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,601
2,000
Kwavitu akivovifanya Mkapa ilikuwa ngumu kujipigua promo na Wananchi kumuelewa. Yeye alicheza vizuri Sana kwenye reforms za sera, miongozo, kanuni na Sheria mbalimbali za nchi na kuunda gvt mechanisms za kutekeleza maboresho hayo. Ni ngumu mwananchi wa kawaida kumuuelewa mtu aliyeanzisha gvt structure nzuri ya kukusanya Kodi kulinganisha na mtu anayezindua daraja.

Hawa wa Sasa wache wajipigie promo coz wanadili na vitu physical zaidi ambavo hata mtoto mdogo anaviona kuliko reforms za kisera.
 
kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,601
2,000
Hata mkataba wa ujenzi wa Daraja la Mfugale (pale TAZARA) ulisainiwa tarehe 15 October 2015 kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya JICA ya Japani wakati huo rais akiwa ni JK

Lakini leo watu wanajua aliyewajengea daraja ni Magufuli
Angeweza kuachana nao tu Kama alivopiga chini bandari ya bwagamoyo au umeme wa gesi.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,201
2,000
JK anajuta nahisi kuachia Daraja la Kigambon kuzinduliwa baadae

Speech ya kuzindua daraja lile ilimnanga sana.

Na jina la lile Daraja alistahili Kikwete.

Kikwete ana history Sana na daraja la Kigamboni, aliwahi litafutia wafadhili kutoka Kuwait zamani mno mwaka 1994 I guess alipokuwa waziri wa fedha.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,197
2,000
JK anajuta nahisi kuachia Daraja la Kigambon kuzinduliwa baadae.

Speech ya kuzindua daraja lile ilimnanga sana.

Na jina la lile Daraja alistahili Kikwete.

Kikwete ana history Sana na daraja la Kigamboni, aliwahi litafutia wafadhili kutoka Kuwait zamani mno mwaka 1994 I guess alipokuwa waziri wa fedha.
Japo haikuwa na haja kuliita lile daraja la Kigamboni jina la Kikwete kwa sababu Kikwete tayari ana daraja la mto Malagarasi.

Lakini haikuwa na maana sana kuliita lile daraja jina la Nyerere, Maana Nyerere ana majina chungu nzima nchini, vyuo, uwanja wa ndege, barabara, campus, barabara na vitu kedekede, na sasa naona tumeanzisha mbuga tumeita jina la Nyerere.

Sijui kwa nini wazee wetu akina Kinjekitile na wengineo waliopambana na mkoloni hawaenziwi!
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,289
2,000
Kuna shida gani nikisema barabara zote toka uhuru nimejenga mimi? Ebo.. acheni watu wanitukuze hadi malaika washuke chato
1596265582346.jpeg
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
2,293
2,000
Ujinga hauwezi kuwaisha baadhi yenu mpaka mnaingia kabrini,

Kwa hiyo sasa unaanza kuwakubali kwamba CCM kumbe wamefanya?

Sasa mbona huwa mnatuchosha kusema eti CCM haijafanya kitu?

Hiyo Miradi unayoisema imetoka wapi tena leo?
Nyinyi michadema mnachosha Sana, na tukiwaambiaga ninyi ni wajinga mnatutukana matusi karibu yote
 
G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,618
2,000
Kuvunja mikataba kuna consequences.

Bandari ya Bagamoyo mkataba ulikuwa haujasainiwa ndiyo maana ilikuwa rahisi kuuvunja.

Pia ujenzi wa umeme wa gesi mkataba ulikuwa haujasainiwa.

Japo haikuwa na haja kuliita lile daraja la Kigamboni jina la Kikwete kwa sababu Kikwete tayari ana daraja la mto Malagarasi

Lakini haikuwa na maana sana kuliita lile daraja jina la Nyerere, Maana Nyerere ana majina chungu nzima nchini, vyuo, uwanja wa ndege, barabara, campus, barabara na vitu kedekede, na sasa naona tumeanzisha mbuga tumeita jina la Nyerere.

Sijui kwa nini wazee wetu akina Kinjekitile na wengineo waliopambana na mkoloni hawaenziwi!
Huyu mzee kila kitu anaita Nyerere. Hata ikulu ya Dodoma anaweza kuiita Nyerere. Ila mimi sipendi tu anapotamka "Nyelele"
 
Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
405
500
Japo haikuwa na haja kuliita lile daraja la Kigamboni jina la Kikwete kwa sababu Kikwete tayari ana daraja la mto Malagarasi

Lakini haikuwa na maana sana kuliita lile daraja jina la Nyerere, Maana Nyerere ana majina chungu nzima nchini, vyuo, uwanja wa ndege, barabara, campus, barabara na vitu kedekede, na sasa naona tumeanzisha mbuga tumeita jina la Nyerere.

Sijui kwa nini wazee wetu akina Kinjekitile na wengineo waliopambana na mkoloni hawaenziwi!
Umenena vema mkuu..
 
mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,786
2,000
Ujinga hauwezi kuwaisha baadhi yenu mpaka mnaingia kabrini,

Kwa hiyo sasa unaanza kuwakubali kwamba CCM kumbe wamefanya?

Sasa mbona huwa mnatuchosha kusema eti CCM haijafanya kitu?

Hiyo Miradi unayoisema imetoka wapi tena leo?
Nyinyi michadema mnachosha Sana, na tukiwaambiaga ninyi ni wajinga mnatutukana matusi karibu yote
We dubwasha umetokea wapi unatoa maushuzi
 
mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,786
2,000
Umeelewa niloandika, au na wewe ndio hao walengwa wa hicho nilichouliza?

Kwa andiko Hilo hapo juu, linaondoa baadhi ya nyuzi zinazopinga kwamba CCM haijafanya kitu? Mbona mnaanza kuorodhesha vitu vilivyofanywa na CCM mbali na kubeza kwamba hawajawahi kufanya?
Upuuzi mtupu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom