Jakaya Kikwete: Rais muungwana anayelipa ubaya kwa wema...

Wewe umejifunzia wapi hizi sheria? Unaelewa maana ya "absolute powers" au unaitafsiri tu unavyotaka wewe? Unadhania kwa nini kuhusu watu ambao wamesemekana ni corrupt Raisi anasema wacha sheria ichukue mkondo wake? Kama unampenda Raisi wetu sema hivyo lakini usimpe nguvu ambazo hata yeye mwenyewe atakuambia hana.

Haya kama raisi wa JMT hana absolute Powers niambie ni kitu gani ambacho raisi wa JMT hawezi kufanya, au ni uamuzi gani ambao hawezi kuchukuwa kama Raisi wa JMT au ni Amri gani ambayo anaweza kuitoa na ikapingwa mahali fulani ndani ya JMT !
 
Ungekuwa muungwana asinge wadhulumu walimu fedha za uhamisho, malimbikizo ya mshahara, fedha za likizo na matibabu, kuto wapandisha madaraja nk. Na mwalimu atakaye unga mkono serikali dhalimu kama hii basi ...
 
Jana katika mkutano mkuu wa CCM ambapo kulikuwa kuna kubadirishana kijiti kati ya Mwenyekiti mstaafu ndugu JK na Mwenyekiti mpya ndugu JPM, nilivutiwa sana na jinsi Watu walivyoconfess wema ambao ndugu Kikwete amewahi kuwatendea katika maisha yao

1) Wa kwanza alikuwa ndugu Mrema aliyesema wazi kuwa miaka kadhaa iliyopita yeye na mkewe wamewahi kusafrishwa na kulipiwa na serikali ya JK kwenda kutibiwa India, mzee Mrema alitoa kauli hiyo alipopewa kuzungumza machache

2) Wa pili alikuwa ni ndugu cheyo naye aliyeelezea kwa shukrani kuwa alikatiwa tiketi First Class na serikali ya JK kwenda na kurudi kutibiwa ng'ambo

Ifahamike hawa watu hawakuwa na marupurupu ya kulipiwa moja kwa moja na serikali lakini kutokana na utu na ukarimu wa Raisi wa wakati huo walitendewa wema huo

Hao ni watu ambao Wamekuja wazi kuzungumza wema na utu wa ndugu Kikwete lakini pamoja na hao, kuna wengine ambao si wanansiasa lakini wameguswa na Mzee Kikwete

kwa mfano
1) Mwanadada Ray C, ambaye alipewa msaada na mzee JK ili aachane na madawa ya kulevya
2) Mtu kama Diamond Platinumz aliyepewa platform ya kujulikana nchi nzima baada ya kukubaliwa kuwa katika timu ya kampeni ya mzee JK mwaka 2010, Wakati huo Diamond alikuwa hana jina jina kubwa, lakini kupewa kwake nafasi huku akiwa msanii underground, kulisaidia kufanya mziki wake usikike hadi huko vijijini na hatimaye kumpa fanbase kubwa

Hapo sijazungumzia, misiba ya watu wa kawaida ambayo JK alihudhuria kuwapa pole na kuwatia moyo wafiwa
Hakika Tutakukumbuka Ndugu JK kwa moyo wako wa utu
 
Katika Tanzania huru naweza kusema kuwa serikali ya kikwete ndio iliyokumbana na misukosuko panda teremka nyingi na hata kuyumbisha uhai wake kwa wingi kuliko marais wote walotangulia.

Amekumbana na upinzani mkali wa ndani ya chama chake, ndani ya serikali na zaidi kutoka kwa wapinzani wake hasa CHADEMA huku bara na CUF kule Zanzibar.

Lakini ameendelea kula na kucheka nao kana kwamba hakuna kilichotokea... Wapo walosema hawamtambui kama ni rais halali, wengine wakasema wanamnyang'anya uenyekiti wa chama wengine wakasema wamemchoka tu kwa kuwa hajafanya lolote tangu aingie madarakani lakini ameendelea kucheka nao...

Kweli ukubwa ni jalala na daima usilipe ubaya kwa ubaya...
YAA NI KWELI JK ANASTAHILI
 
Back
Top Bottom