Libya
JF-Expert Member
- Nov 11, 2016
- 783
- 1,918
======
Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha DSM (UDSM) amefika hosteli za chuo hicho ‘Hostel za Magufuli' kwa ajili ya kukagua mazingira ya Hostel kabla ya kuanza kuwapokea wanafunzi ambao wanatarajiwa kuendelea na masomo yao June 01, 2020.Ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali imeuhakikishia uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa hosteli za Magufuli ni salama baada ya kutumika kuwahifadhi watu walioingia nchini kutoka nje waliokuwa karibu na wagonjwa wa Covid-19.
Mstaafu Kikwete amesema Serikali imemuhakikishia kuwa Hosteli hizo ambazo zilibadilishwa matumizi na kuwa Karantini kwa Watu wanaotoka nje ya Nchi ikiwa ni hatua ya kupambana na corona, zipo salama tayari kwa matumizi.