Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 ulitoa matokeo yaliyokupa weweushindi wa kimbunga wa asilimia 80 na ushee. Waliokupigia kura zilizokuwezesha kuingiaIkulu ni watanzania waliokuamini na kukupa dhamana uwaongoze. Hapa sitakikukubaliana na "marafiki zako" wanaodai kuwa wao ndio waliokuingiza Ikulu. Miminamini kuwa umeingia hapo kwa maamuzi yako wewe binafsi, watanzania, na, barakaza Mwenyezi Mungu. "Marafiki zako" hao wameanza kujisema hadharanikuwa wao ni WAUAJI (rejea thread ya Membe kuwa Muangalifu: Adui yako humjui), na kama hilo halitoshi, wanakuhusisha wewe ktk DHAMBI hiikubwa kuliko dhambi nyingine yeyote. Wanafanya hivi kwa sababu weweunawakaribisha "mahali patakatifu" kunywa nao chai na kuwasikiliza wanayokuambia.Kuna baadhi yao wamesikika wakisema kuwa wao wanatoka ktk kabila yenye damu yakuua. (Kabila hilo halipo katika bara la Afrika lililojaa ustaarabu na heshima kwa maisha ya binadamu wengine), hivyo wao kutoa roho ya mtu sioissue kabisa. "Marafiki" hawa wakija kwako wanakuwa watiifu nawanyenyekevu kama masista pale Vatican, lakini wakitoka tu hapo Ikulu, wanarudiktk damu yao ya asili. "Marafiki" hawa wameisha gundua kuwa huna msaada kwaokwani wanazongwa na matatizo lukuki toka kwa wenye nchi, lakini hawapati msaadawako. Wewe unalijua hilo kwani unashindwa kuwasaidia kwa kuhofia reactions yawaliokudhaminisha Ikulu. Kitendo cha wewe kuwasaidia kitakutenganisha nandugu zako wa kweli (hawa ni marafiki zako waadilifu). Ukiwapoteza tu nduguzako hawa, basi ujue kuwa "marafiki zako" wanafiki ndio watakaokuwa wa kwanzakukutenda kwani hutakuwa na pa kwenda. Nimesoma sana vitabu vyote vya dini zetu Tukufu,bado sijaona sehemu inayokuagiza wewe kama Kiongozi wa juu kabisa ktk nchiKUWATETEA watu wachache wanaolihujumu Taifa ambalo wananchi wake wamekuamini nakukupa dhamana ya KUWALINDA. Rudi tena ktk dini yako na ujiulize, je, upo Ikulukwa akili ya kuwatetea marafiki zako wanaohujumu mali za wananchi ambao nimasikini? Jibu utakalolipata LIFANYIE kazi bila kuchelewa. Imani ya watanzaniakwako inapungua kila kukicha, hii ni kwa sababu wanaona mambo yanakwendakinyume na walivyokutegemea. Wananchi hawakutegemea kama ungeendelea kukaakimya huku ukiona wazi kuwa Chama chako kinahujumiwa, familia yako inahujumiwa,marafiki (ndg zako) wanahujumiwa, na nchi unayoiongoza inahujumiwa. Kibayazaidi ni kuwa, wanaofanya hujuma hizo ni marafiki zako ambao badounawakaribisha Ikulu. TAFAKARI, CHUKUA MAAMUZI. Taifa zima lipo nawe, unaogopanini? Hivi unadhani ukimaliza muda wako wa kutawala bila kuwachukulia hatuazinazostahili hawa marafiki zako utaishi kwa amani? Usidanganyike hata chembe,utasakamwa mpaka na majirani zako, utakuwa mpweke, utabaki peke yako. Ulipokuwa unagombea mwaka 2005 wananchi walikufananishana Hayati Julius Kambarage Nyerere, wakajenga imani kubwa kwako kutokana namisimamo yako, umakini wako, na ukaribu wa familia yako na ya Mwl. Nyerere.Wakajua kuwa umebeba siri ya uongozi toka kwa marehemu Mzee Mrisho, na Hayatibaba wa Taifa, Mwl. J. K. Nyerere. Sifa ya wazee hawa sote tunaijua, lakini siohivyo unavyofanya. Unawaumiza watetezi wako wa kweli. Wewe ni MTAWALA,TAFADHALI TAWALA NCHI HII. Waliokupa dhamana hawana pa kwenda kwa sasa,usiwaache jangwani, Mungu atakuuliza, umewaacha wapi na vipi waja wangu?