Jakaya Kikwete kupata tuzo ya Mo Ibrahim?

Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,384
257
Mh. JK amekuwa na bahati ya kutunikiwa shahada za juu za PhD kuwazidi maraisi wengine wa JMT waliomtangulia. Mwl. JK alipewa shahada kama hiyo na chuo kikuu cha kilimo Sokoine kwa mchango wake katika Rural development.
Akipokea hiyo shahada mwalimu alisema ameipokea kwasababu 2. Moja kutambua umuhimu wa mkakati maendeleo vijijini na pia kwa sababu ya heshima ya Edward Sokoine ambaye chuo hicho kimepewa jina kwa heshima yake.
Mpaka sasa Jakaya Kikwete ameshawazidi Ben na Ali katika kujinyakulia hizo shahada. Sijajua vigezo vinavyotumika kumtunuku shahada zote hizo. Lakini nadhani kama wasomi wote hao wametambua mchango wa Jakaya katika ustawi wa nchi hii na Afrika kwa ujumla.
Mwaka 2009 na 2010 nishani ya Mo ilikosa mshindi, kama kweli wakuu wa vyuo vyetu wametoa hizo shahada kwa vigezo stahiki, je, tutegemee JK kuwa mshindi wa nishani ya Mo mwaka 2016?
 
Mwaka 2009 na 2010 nishani ya Mo ilikosa mshindi, kama kweli wakuu wa vyuo vyetu wametoa hizo shahada kwa vigezo stahiki, je, tutegemee JK kuwa mshindi wa nishani ya Mo mwaka 2016?

Maybe posthumously.......................
 
Labda kama kutakuwa na jambo la pekee atakalolifanya kipindi hiki lakini kwa yale aliyofanya kipindi kilichopita, itakuwa ni mwujiza kutunukiwa nishani hiyo. Kwa tabia zetu hizi za kujipendekeza, kutunukiwa degree na wateule wake wa hizi taasisi za elimu za humu nchini kunaweza kusiwe na maana yoyote kuashiria utendaji kazi wake.

Kwa nini huko nyuma haikuwa inatokea hivyo? Ni kutokana na mfumo wa uendashaji wa vyuo vikuu. Siku za huko nyuma, Mkuu wa Vyuo Vikuu alikuwa ni Rais mwenyewe, na asingekuwa rahisi kwake mwenyewe kupendekeza yeye apewe degree ya heshima. Siku hizi wateule wa Rais ndiyo huwa wakuu wa vyuo, ambao ni wanasiasa.
 
Nakusalimu mbogela labda kwa kuwa ameweza kuwa mgeni rasmi kwa uzinduzi wa airtel kwani matokeo moja wapo ya ufisadi wa celtel, je unakumbuka celtel hawakuwalipa ttcl kutumia minara yake? wakati celtel ikiwa mali ya Ibrahim mo? tutafakari NO FREE LUNCH AT ALL
 
JMK anastahiki kupata hiyo tuzo. Ni bahati mbaya hutolewa kwa Marais wastaafu pekee.

JMK anastahiki pia hizo PhD alizotunukiwa, ni mengi aliyoyafanya na anayoyafanya.

Ni kiongozi anaestahili kila sifa ya uongozi, mchapa kazi asiechoka, anakubalika ndani na nje ya nchi.

Mstahamilivu, Mcheshi, Mnyeyekevu, Mjasiri.

Mengi yaliowashinda viongozi wa Tanzania waliopita, kwake kayaweza.

Katatuwa mambo kadha wa kadha kiufanisi mkubwa kabisa.

Leo Tanzania tunaona hata vigogo kama Mramba wakifikishwa mahakamani. Huu ni ujasiri wa hali ya juu. Leo tunaona hata wanaombeza yeye anawafanyia mzaha na kuwaambia "mtarudi". Kudos JMK
 
Hawa wanaompa phd za heshima wanajipendekeza kwake ili vibarua vyao visiote nyasi.otherwise hamna vigezo vyovyote kumfanya ajazwe ma phd yote hayo.
Pia taasisi ya mo inafuatilia vizuri sana yanayotokea ktk kila nchi hivyo si rahisi kwa jk kuingia hata kumi bora atakapostaafu kwani kazi kubwa aliyofanya ni kuwapa ulinzi wa kutosha mafisadi.
 
JMK anastahiki kupata hiyo tuzo. Ni bahati mbaya hutolewa kwa Marais wastaafu pekee.

JMK anastahiki pia hizo PhD alizotunukiwa, ni mengi aliyoyafanya na anayoyafanya.

Ni kiongozi anaestahili kila sifa ya uongozi, mchapa kazi asiechoka, anakubalika ndani na nje ya nchi.

Mstahamilivu, Mcheshi, Mnyeyekevu, Mjasiri.

Mengi yaliowashinda viongozi wa Tanzania waliopita, kwake kayaweza.

Katatuwa mambo kadha wa kadha kiufanisi mkubwa kabisa.

Leo Tanzania tunaona hata vigogo kama Mramba wakifikishwa mahakamani. Huu ni ujasiri wa hali ya juu. Leo tunaona hata wanaombeza yeye anawafanyia mzaha na kuwaambia "mtarudi". Kudos JMK

Kikwete hakumpeleka Mramba wala wale watuhumiwa wa EPA mahakamani kwa hiari yake. Ukweli ni kuwa baada ya Dr Slaa kuanika ufisadi wa Alex Stewart, EPA, Meremeta, Tangold, n.k.; wahisani waliipa sharti serikali ya Kikwete kuwa wasingetoa hela yao mpaka waone hatua zilizochukuliwa dhidi ya mafisadi. Baada ya hapo Kikwete na serikali yake wakaandaa haraka haraka kesi zisizo na nguvu za kuwatia wahusika hatiani ili waweze kupata fedha.

Hakuna jambo kubwa ambalo Kikwete anaweza kujivunia kufanya zaidi ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ndiyo maana hata ninyi mnaomwunga mkono mnasema tu, 'mengi amefanya' lakini mnashindwa kuorodhesha hayo aliyoyafanya ili tuyaone kuwa ni mengi na makubwa kiasi gani. Talk quantitavely with data, vinginevyo ni porojo.
 
According to Mo Ibrahim Foundation, the prize is awarded to African heads of state who deliver security, health, education and economic development to their constituents, and who democratically transfer power to their successor. So as to be able to know if JK qualifies or not, you have to weigh up his chances for each of the categories.
 
JMK anastahiki kupata hiyo tuzo. Ni bahati mbaya hutolewa kwa Marais wastaafu pekee.

JMK anastahiki pia hizo PhD alizotunukiwa, ni mengi aliyoyafanya na anayoyafanya.

Ni kiongozi anaestahili kila sifa ya uongozi, mchapa kazi asiechoka, anakubalika ndani na nje ya nchi.

Mstahamilivu, Mcheshi, Mnyeyekevu, Mjasiri.

Mengi yaliowashinda viongozi wa Tanzania waliopita, kwake kayaweza.

Katatuwa mambo kadha wa kadha kiufanisi mkubwa kabisa.

Leo Tanzania tunaona hata vigogo kama Mramba wakifikishwa mahakamani. Huu ni ujasiri wa hali ya juu. Leo tunaona hata wanaombeza yeye anawafanyia mzaha na kuwaambia "mtarudi". Kudos JMK

Anawavumilia mpaka mafisadi wanamchakachua! Anawachekea mpaka wanamrudi na watendaji wake wanamdanganya! Amezidi kucheka cheka naye hamwezi kumwonya? Bahati mbaya kwake tuzo ya Mo haiangalii wanaojichekeshachesha tu inaangalia utendaji wa Rais wakati alipokuwa madarakani!
 
jmk anastahiki kupata hiyo tuzo. Ni bahati mbaya hutolewa kwa marais wastaafu pekee.

Jmk anastahiki pia hizo phd alizotunukiwa, ni mengi aliyoyafanya na anayoyafanya.

Ni kiongozi anaestahili kila sifa ya uongozi, mchapa kazi asiechoka, anakubalika ndani na nje ya nchi.

Mstahamilivu, mcheshi, mnyeyekevu, mjasiri.

Mengi yaliowashinda viongozi wa tanzania waliopita, kwake kayaweza.

Katatuwa mambo kadha wa kadha kiufanisi mkubwa kabisa.

Leo tanzania tunaona hata vigogo kama mramba wakifikishwa mahakamani. Huu ni ujasiri wa hali ya juu. Leo tunaona hata wanaombeza yeye anawafanyia mzaha na kuwaambia "mtarudi". Kudos jmk

bahati mbaya kwa jk bodi ya mo ibrahim imejaza watu makini sana na wanaoheshimika duniani .hawadanganyiki.
 
JMK anastahiki kupata hiyo tuzo. Ni bahati mbaya hutolewa kwa Marais wastaafu pekee.

JMK anastahiki pia hizo PhD alizotunukiwa, ni mengi aliyoyafanya na anayoyafanya.

Ni kiongozi anaestahili kila sifa ya uongozi, mchapa kazi asiechoka, anakubalika ndani na nje ya nchi.

Mstahamilivu, Mcheshi, Mnyeyekevu, Mjasiri.

Mengi yaliowashinda viongozi wa Tanzania waliopita, kwake kayaweza.

Katatuwa mambo kadha wa kadha kiufanisi mkubwa kabisa.

Leo Tanzania tunaona hata vigogo kama Mramba wakifikishwa mahakamani. Huu ni ujasiri wa hali ya juu. Leo tunaona hata wanaombeza yeye anawafanyia mzaha na kuwaambia "mtarudi". Kudos JMK

Dar Es Salaam: Ujasiri unaongela hapa ni ule wakusema Mramba ni JEMBE nini? Uliwahi kujiuliza kama mtu anayepelekwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma nastahiri kupewa tena uongozi?

Mo Ibra prize is open for any President in office, but getting it is difficult like developing African countries!

kama atakubali na kusimamia kuandikwa kwa katiba mpya na kuongeza haki na uhuru wakati wa uchaguzi 2015, Je. Haitamuongezea credit kwa ajili ya hiyo nishani
 
Political willy ni utata kwa hawa watawala wetu. They cant walk the talk, wewe si umeona huyu anaejiita mtoto wa mkulima anakataa gari then anaamuru apewe mtu mwingine -hii kweli ni sawa ni political will kweli au unafiki wa waziwazi. Hata wapewe shahada 100 bila utekelezaji hii ni kumpigia mbuzi gitaa. Walete katiba mpya, walete makazi bora, walete mikataba yenye maslahi ya 50% kwa kila upande, watoe ellim bure and afya bure,
 
Atapata hiyo Mo Ibrahim Award siku ambapo jua litachomoza magharibi!

Huyu Kikwete si mmojawao ambao iwapo matokeo ya uchaguzi ni tete kwake angefanya kama Kibaki, na gbagbo? Angelazimisha kutangazwa mshindi na kuapishwa usiku usiku?

Mo Ibrahim huwa anawachukia sana viongozi wa namna hiyo!
 
Yoote yanawezekana! kwani hujaona this year Tanzania ranks where well beautified? regardless of the many issues that seemed wrong on the ground! au nyie watu hamja-notice hicho kitu? i doubt the credibility of Mo Ibrahim Index!
 
Hivi hizo tuzo zina faida gani kwa mwananchi wa chini aaaghrrr apewe asipewe has nothing to do with me ila kuna watu wako concern ajabu utafikiri amepewa tiketi ya kwenda ahera LOL!.
 
Dar Es Salaam: Ujasiri unaongela hapa ni ule wakusema Mramba ni JEMBE nini? Uliwahi kujiuliza kama mtu anayepelekwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma nastahiri kupewa tena uongozi?

Mo Ibra prize is open for any President in office, but getting it is difficult like developing African countries!

Kuhusu Mramba, kama wananchi wake alipogombania Ubunge wangemkubali hilo sio tatizo la JMK. Jee, aliendelea kuwa waziri baada ya kupelekwa mahakamani?

Katika siasa za Tanzania tumesikia kuna mtu yupo jela na kachaguliwa bila hata ya kuwepo kufanya kampeni. Hilo la Kikwete kumpigia debe Mramba wakati wa kampeni lisikustuwe sana, kwani kama CCM ya huko kwao ilimpitisha kwenye kura za maoni basi ndiye aliekuwa mgombea halali kwa wakati huo.

La tuzo ya Mo, inawezekana ikawa kama ulivyosema, sina ubishi katika hilo.
 
Back
Top Bottom