Jakaya Kikwete kajenga kiwanda chake kwenye makazi ya watu Mbagala

MWANASHERIA

Member
Aug 20, 2010
84
11
baada ya kumuandama benjamini mkapa na mgodi wake wa makaa ya mawe, kikwete amejenga kiwanda chake cha cement hapa mbagala.

kinachotuumiza wananchi ni kwamba hiki kiwanda kipo kwenye makazi yetu, kinyume kabisa na kanuni za ujenzi wa viwanda vya aina hii, hata ukiangalia viwanda vingine vyote vya cement vipo mbali sana na makazi ya watu.

mpaka hapo tunasikitikia afya zetu, sijui nani atakifunga hiki kiwanda. Tufakufa kwa cancer siku si nyingi.....

eeeee mungu tuokoe na kiwanda cha kikwete sisi wakazi wa mbagala..
 
Tupe data zitakazosaidia wanajamii forums kuwanusuru wananchi wa huko Mbagala. Jaribu kujenga hoja yenye vielelezo ili kuipa uzito hoja yake tafadhali.
 
Mkuu,
Poleni sana.!
Kakijenga lini tena?
Ulivyoongea inaonyesha tayari kiwnda kishaanza kufanya kazi, hadi madhara yanaonekana!
Lakini kama mtu anashiriki kwenye madili makubwa kama ya richmond/dowans unategemea nini?
Watalipah hela zetu wakiondolewa madarakani!
 
Kiwanda hiki kilianza kujengwa miaka ya tisini na saba, wakati wa ujenzi niliwaona wamanga ndo walikuwa wasimamizi na wawekezaji fulani uchwara, mbona kiwanda kipo njiani kabisa, nashaanga tulivyokuwa slow ku react ktk issue kama hizi!
 
ooh, sikujua kama wadau hamjui kuwa ana kiwanda cha CEMENT, ndo maana nimeiweka bila maelezo makubwa. Ni kwamba hicho kiwanda mnachokisikia cha CEMENT kuwa kitaanza kufanya kazi siku si nyingi, na hata yeye mwenyewe KIKWETE amekiongelea sana, kwamba kitasaidia bei ya CEMENT kushuka, ila tu hajawahi kusema kuwa ni cha kwake.

KIPO HAPA MBAGALA, bado hakijaanza kazi kinategemewa kuanza Marchi Mwanzoni (SIJUI NDO WANATAKA HELA ZA DOWANS ILI AMALIZIE HARAKA?) Ila mabomba yake ya Moshi tayari yameshaanza kututisha ukizingatia tumeshaona moshi mkubwa wenye sumu unaotoka kwenye kiwanda cha Twiga kilichopo WAZO HILL.

SIJUI TUFANYEJE ILI KUPINGA HIKI KIWANDA KUANZA KAZI, NAJUA TATHMINI ZA MAZINGIRA ZITAKUA HAZIJAFANYIKA, SI KIWANDA CHA MKUBWAAAAAA..
 
Tuletee picha ikiwezekana.
Elezea kirefu kikombagala ipi?
 
Mmmmh hi nayo kali, kama kiwanda cha Cement kinaweza kujengwa Mbagala. Si wangeenda kwenye mapoli yako mengi tuu jamani?? Huku ni kuuwana "slowly"
 
SIJUI TUFANYEJE ILI KUPINGA HIKI KIWANDA KUANZA KAZI, NAJUA TATHMINI ZA MAZINGIRA ZITAKUA HAZIJAFANYIKA, SI KIWANDA CHA MKUBWAAAAAA..

umeshaanza kufanya la maana peleka na habari zako kwenye vyombo vya habari na mjikusanye wakazi wote wa huko mjitokeze mpinge hatua hii tena unaweza ukawerekodi watoto wako wanakohoa na kupata evidence kutoka kwa madaktari athari za huo moshi
 
Ndo maana tunashangaa, na tunashindwa kuelewa kwamba ukiacha kutunyima huduma muhimu za kijamii kama maji, umeme, zahanati, shule nzuri na pamoja na kutuibia raslimali za taifa bado JK kaamua kutuua kwa CANCER wananchi wa MBAGALA, sijui tumemkosea nini sisi masikini.

Na kama tumemkosea, angetuambia basi tumuombe msamaha.
 
Jamani eh, Kikwete anaweza kuwa na matatizo yake kama binadamu wengine yeye siyo Malaika/Nabii. Hili la kusema eti kiwanda cha Mbagala cha CEMENT ni cha kwake ni uzushi mtupu - tusilete mambo ya kuweka chumvi wakati mwingine kwa kutafuta public sympathy na publicity STUNT kwa kuwa tunajuwa akitajwa Kikwete tu, basi watu watakuja juu kwa kumlahumu, tusisite kumsema pale anapokosea mambo fulani lakini siyo vizuri kumzulia MAMBO.

Kwa nini nasema hivyo:

  • Kiwanda hiki ni mali ya TANGA CEMENT nadhani wakishirikiana na WACHINA au mitambo ya kuzalisha CEMENT imeagizwa kutoka UCHINA, sasa hapo Kikwete anusikana vipi!

  • Kuhusu vumbi linalo tokana na uzalishaji wa CEMENT, mimi ningeshauri wakazi wa Mbagala wawashinikize wajenzi wa kiwanda hicho kwamba vumbi hilo liidhibitiwe kwa njia ya ku-spray maji kwenye vumbi hilo kwa pressure kubwa badala ya kuliachia lipitie kwenye Chimney, wakitekeleza hilo basi wakazi wa huko watakuwa SALAMA, na actually athali za vumbi hilo halitakuwa confined Mbagala tu linaweza kusaambaa popote upepo unapo elekea kama hawataweza kulidhibiti kwa njia niliyo eleza hapo juu.

  • Wakati wa kuwabana ni sasa hivi kabla hawaja anza kuzalisha CEMENT, mkichelewa tu basi watawaletea visingizio chungu mzima, kumbuka WAZO Hill bado kiwanda chao kinatoa vumbi hewani bila ya udhibitu wowote na sijawahi kusikia wanachukuliwa hatua yoyote na wahusika wa mazingira - chunga sana.
 
Kiwanda hiki ni mali ya TANGA CEMENT nadhani wakishirikiana na WACHINA au mitambo ya kuzalisha CEMENT imeagizwa kutoka UCHINA, sasa hapo Kikwete anusikana vipi!

Unao ushahidi gani kuwa hiki kiwanda kipya ni mali ya Tanga Cement? Hiki kiwanda kinaitwaje anyway?
 
SIJUI TUFANYEJE ILI KUPINGA HIKI KIWANDA KUANZA KAZI, NAJUA TATHMINI ZA MAZINGIRA ZITAKUA HAZIJAFANYIKA, SI KIWANDA CHA MKUBWAAAAAA..

Inavyoonyesha, NEMC walikipiga stop kufanya uzalishaji wa cement baada ya tathmini yao ya mazingira. Soma habari chini.

The National Environmental Management Council (NEMC) confirmed on Friday that the company plans to import clinkers from China or India or any other country it decides and process the materials at their factory.

NEMC also confirmed that it has already - since some two years back - issued an Environmental Impact Assessment (EIA) certificate to the company for production of other materials, but not production of construction cement.
 
Ndo maana tunashangaa, na tunashindwa kuelewa kwamba ukiacha kutunyima huduma muhimu za kijamii kama maji, umeme, zahanati, shule nzuri na pamoja na kutuibia raslimali za taifa bado JK kaamua kutuua kwa CANCER wananchi wa MBAGALA, sijui tumemkosea nini sisi masikini. Na kama tumemkosea, angetuambia basi tumuombe msamaha.
Hamjamkosea kitu, ni roho tu ya ufisadi. Next time chagua Chadema tupambane na mafisadi hawa.
 
Unaposema kiwanda ni cha Tanga Cement then UNADHANI wanashirikiana na Wachina nilifikiri una evidence ya kutosha kumbe hamna kitu, ni vema ukatumbia kipo wapi na tanga cement wanashare kiasi gani na hao wachina wanashare kiasi gani.
 
ooh, sikujua kama wadau hamjui kuwa ana kiwanda cha CEMENT, ndo maana nimeiweka bila maelezo makubwa. Ni kwamba hicho kiwanda mnachokisikia cha CEMENT kuwa kitaanza kufanya kazi siku si nyingi, na hata yeye mwenyewe KIKWETE amekiongelea sana, kwamba kitasaidia bei ya CEMENT kushuka, ila tu hajawahi kusema kuwa ni cha kwake.

KIPO HAPA MBAGALA, bado hakijaanza kazi kinategemewa kuanza Marchi Mwanzoni (SIJUI NDO WANATAKA HELA ZA DOWANS ILI AMALIZIE HARAKA?) Ila mabomba yake ya Moshi tayari yameshaanza kututisha ukizingatia tumeshaona moshi mkubwa wenye sumu unaotoka kwenye kiwanda cha Twiga kilichopo WAZO HILL.

SIJUI TUFANYEJE ILI KUPINGA HIKI KIWANDA KUANZA KAZI, NAJUA TATHMINI ZA MAZINGIRA ZITAKUA HAZIJAFANYIKA, SI KIWANDA CHA MKUBWAAAAAA..

Poleni usiulize dawa dawa ni kuandamana tuu
 
Unao ushahidi gani kuwa hiki kiwanda kipya ni mali ya Tanga Cement? Hiki kiwanda kinaitwaje anyway?

Kwani huyo aliyeleta hii habari anaushaidi? au porojo tu hata kama tunapinga tupinge kwa hoja na ushahidi na si kupandikiza chuki
 
Munashangaa hilo, mbona kajenga hoteli (Bilila) kwenye pitio la Wanyama Serengeti na pia amechukua jengo la TANAPA na ameliuza na TANAPA wamepewa miezi 6 kuhama
 
Back
Top Bottom