Jakaya Kikwete analima lakini Graduates kutwa na bahasha za khaki kutafuta Sehemu za Kujitolea

Uliotoa post yako haujitambui na hauna mawazo critical ya kuweza kumshawish mtuu!! Una matatzo saana ww ila kiukweli hauwez mlingansha jakaya ktk kilimo na graduate fresh from colege
 
Kilimo ni kamari ya hatari sana. Usiandike vitu pasipo kuvifanyia utafiti. Kila mtu anatamani kulima akidhani ni kujiajiri lakini wakati wa mavuno mambo huwa ya huzuni sana.

Ni lazima utofautishe kulima kama mlango wa kutokea na kulima kwa kujifurahisha ukiwa umeshatoka. Mzee JK halimi ili atake kutoka. Hata tembo wakipitia hilo shamba hataumia kama graduates asiye na kazi atakavyoamua kulima kwa kuwekeza resources zake zote akitegemea kutokea hapo.
 
Uliotoa post yako haujitambui na hauna mawazo critical ya kuweza kumshawish mtuu!! Una matatzo saana ww ila kiukweli hauwez mlingansha jakaya ktk kilimo na graduate fresh from colege
Mkuu Soma acha Kurupuka Cheki Nilivyosema Unaweza Kuanza na tetea 40 na Majogoo 7 kwa Kuuza Laptop yako ukaenda Kuishi nje ya Mji uza Na Smartphone yako Hao Kuku Kijijini Unawaachia tuu haina haja ya Pumba ningazungumzia Bei Rahisi ya Dawa za Kuku wa Kienyeji.

Imagine hao Wakitotoa Kila Mmoja watoto 8×40=320 Kama Unatumia Dawa Vizuri ambazo si Bei nategemea Unaweza Kuponesha Kuku 300

Wakulima wanauza 17,000-23,000
Wastan Umeuza Kwa 18,000×300= 5,400,000 no Unaweza Kusema Ngoja Nisiwauze Wote nitawauza Jogoo na baadhi ya Teta nitabaki na Ku
Project hii Kwenye Second year, na third year itakuletea pesa Nyingi Mimi Kutokana Na Elimu niliyoipata Kitu chochote ninachokifanya huwa nakiita Project na Nakitengea Mda Kama Kuku nikifuga kwa Miaka 3 nikauza Wote hakika nitapata pesa nyingi.

Ila kwa Kuwa wewe unataka Kuwa Rais Ustaafu ndo Ulime sisi ngoja tuhangaike!
 
Kilimo ni kamari ya hatari sana. Usiandike vitu pasipo kuvifanyia utafiti. Kila mtu anatamani kulima akidhani ni kujiajiri lakini wakati wa mavuno mambo huwa ya huzuni sana.

Ni lazima utofautishe kulima kama mlango wa kutokea na kulima kwa kujifurahisha ukiwa umeshatoka. Mzee JK halimi ili atake kutoka. Hata tembo wakipitia hilo shamba hataumia kama graduates asiye na kazi atakavyoamua kulima kwa kuwekeza resources zake zote akitegemea kutokea hapo.
Hata wazee wa Kale walisema jembe halimtupi mkulima Kuna Mabonde na Mito mingi sana Tanzania na yanafaa kwa Kilimo.
 
Watu wakisikia shamba... Kilimo.... Kujiajiri kwa njia ya kilimo wanachukuia poa sana... Ok ni sehemu nzuri sana ya kujiajiri lakini huwezi kwenda shambani ukiwa empty mfukoni... Mimi nasema kwa hali ya sasa hivi hata ukiwa na m1 uliyoilimbikiza haitakutosha.

Tusitiane moyo kinafiki hapa.. Mtu unakodi shamba, unakodi mashine ya umwagiliaji, utahitaji vibarua wa kukusaidia, utahitaji trekta ya kulima, utahitaji watu wa kukusaidia kupalilia, wewe mwenyewe utahitaji kula, utahitaji madawa na mbolea n.k alafu uje uniambie 1m {mathalani} inatosha.. Jamani kilimo sio lele mama kinahitaji mtaji mubashara... Jk si wa kumfananisha na graduate hata siku moja.

Labda kama mtoa uzi alimaanisha graduate wa urais na hapa tz tunao watu kama hao watatu tuu....... Teh teh
 
Pepo tokaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..
Stress tulizonazo bado unataka kutuongezea zakwako.
Uyo mheshimiwa kwanini ameanza kulima baada ya kustaff
 
Trol nimekuelewa sana sana! shida nilizopata baada ya kuhitimu law 2014, zimenifanya nitafute namna ya kujiajiri. nimeanza kulima mahindi eka kadhaa mkoa fulani, na mwaka huu nitakodi eka 15 ili mwakani nilime, then nitakuwa ninaongeza eka kila mwaka had ziwe 200. eka moja kulima had kuvuna inanigharimu laki moja tu. najua kuna watakao kuja kuniponda kwa gharama nilizotaja, ila ukwel ndiyo huo. nipo porin na digrii yangu
 
Mkuu nakuombea kwa Mungu Kila Laheri Pia Nakushauri Ongeza Mazao ya Biashara Alizeti Unaweza Kuchanganya na Maindi ngoja watembeze Bahasha.
 
Mkuu nakuombea kwa Mungu Kila Laheri Pia Nakushauri Ongeza Mazao ya Biashara Alizeti Unaweza Kuchanganya na Maindi ngoja watembeze Bahasha.

Msimu huu nimechanganya alizeti, na mwakani nitachanganya na mbaazi pia. Asante sana.
 
SAFARI BADO SANA. Ndivyo ninavyoweza kusema kuwa bado tuna safari ndefu ya kuendelea kuelimisha walioelimika, watu wenye shahada na uzamili. Hapa mara kadhaa nimekuwa nikijiuliza nini maana ya msomi. Nilipokuwa chuo nilimnukuu mwalimu wangu aliyesema "university, sio mahali pa kusoma kile tu ulichoenda kusomea bali ni sehemu pa kupata maarifa mengi yahusuyo Universe".

Hapa naanza kuamini kwanink wasomi wengi hasa tuliomaliza siku za karibuni tusivyojua nini maana ya elimu lakini kubwa zaidi ni Universe education. Mleta mada binafsi nimekuelewa. Nilipohitimu chuo mwaka 2015 na kukaa mtaani kwa takribani miezi 9 bila kazi nikaamua kujichanganya kuendesha bajaji, shahada nimeacha ndani na wala sifikilii kuwa kuna ajira za ualimu mbeleni na wala sifuatilii kitu hicho. Vijana wenzangu wasomi wakawa wananishangaa kwamba na huyu naye anaendesha hivi vitu badala ya kusaka ajira hata private. Hawajui tayari nipo private napiga hela wao wanataka kuona upo ofisini.

Nimeendesha bajaji takribani miezi kadhaa nimefanya mambo makubwa kiasi cha kuhama nyumbani na kwenda kupanga huku nikiwa na vitu vya thamani ndani. Nageuka nyuma naona wenzangu bado wameshika bahasha wanatoka kwa mama na baba wengine kwa washkaji (getto). Mlet mada amekuja na mada nzuri sana ukisoma kwa utulivu wa akiri kama upo kwenye UE, ukitafakari na kuichambua ndipo utaona utamu wake.

Mleta mada kaja na mada inasema TUAMKIE KILIMO. Hajasema kilimo cha aina gani, ama tikiti au muhogo. Watu wametililika kwa jazba ya kukosa ajira.

Dhana ya kilimo ni kubwa na pana, kuna kilimo cha kulima shambani lakini kuna kilimo cha kufuga ndege mfano kuku, au wanyama kama nguruwe, mbuzi nk. Watu mnaanza kukoment gharama za kilimo hicho pasi na kujua ni kilimo gani, kwa mfano ukiamua kulima kilimo cha mbogamboga kwa saizi kuna aina ya ulimaji ambalo huitaji ekari hata moja ili ulime mboga na bado ukapiga hela, rejea BUSTANI KICHUGUU (kwa mfano tu), kama hiyo haitoshi kuna ufugaji wa kuku ambao kwa kuku mmoja tetea unaweza pata kwa sh elfu 10 hapa ukiwa na laki sio chini ya kuku 10 kwa kufanya biashara za naomba nipunguzie. Ufugaji wa kuju hauna gharama sana hasa ufugaji wa kuku asilia ambao mayai yake ni gharama sana mtaani kuliko yale ya kuku wa kisasa.

SASA NASTAJABIA KWANINI WATU HAWATUMII UBONGO KUFIKIRI, KUNA TOFAUTI GANI KATI YA WATU MLIOCHANGIA HAPA TENA WASOMI WA SHAHADA MSIFANANISHWE NA BASHITE AMBAE TUNAMTUHUMU KUFOJI VYETI.
NA NYIE MLIO NA VYETI MBONA VIAZI TU KICHANI. nimeandika mengi najua mtakuja na matusi mengi mengi lakini ukiona unataka kutukana ni heli upite kimya maana sipendi kuboreka na komentk zisizo na staha hata kama hatufahamiani naomba tuheshimiane. NIMEMALIZA. nazidi kupiga pesa kozi nimejiongeza nyie endeleenj kuzunguka na bahasha.
 
Hata wazee wa Kale walisema jembe halimtupi mkulima Kuna Mabonde na Mito mingi sana Tanzania na yanafaa kwa Kilimo.
chnagamoto za kale na za sasa hazilingani. Kwa sasa kilimo kinahitaji mtaji. Huko kale ardhi ilikuwa na mbolea na hakukuwa wadudu wengi wanaoharibu mazao. Leo ukipanda tu mazao yakiota lazima uanze kupulizia madawa kuua wadudu na utitiri, hapo hujagusa mbolea na vifaa vingine.

Kama hujajihusisha na kilimo unaweza ukaandika vyovyote unavyoweza maana mentality ya watu ni kuwa kulima ni kufukia mbegu tu contrary to reality.

bila mtaji wa maana kwa sasa utalima chakula cha kujikimu wewe na familia yako tu
 
Toa mchanganuo kwenye laki tano (500,000 au 1,000,000);
1. Bei ya mbegu,
2.Bei ya kukodisha shamba ekari moja au mbili na
3.Bei ya madawa na mbolea.
Pia kama mimi nipo Dar nataka shamba Arusha, Moro au Mbeya gharama za usimamizi wa shamba na muangalizi/msimamizi zitakuwaje? Tafadhali tufafanulie vizuri. Kumbuka pia kuna athari za mabadiliko ya hali ya hewa, je umejipangaje kukabiliana na climate change katika kilimo?
 
Aiseeee I'm inspired.....ngoja ninoe panga niende zangu shamba miee
Hivi alishika jembe au alishikiwa,kingine Elewa kwa hadhi yake kwenye kulima ni tofauti n'a mkulimaa wa magole huko kwanza ana acsess ya pembejeo etc....syo mbaya naona sahv mahindi atapiga nao maana alilimaga nanasi kipindi fulani ikala kwakeeee....

Ova
 
Back
Top Bottom