Jakaya Kikwete analima lakini Graduates kutwa na bahasha za khaki kutafuta Sehemu za Kujitolea

...siogopi kilimo blaza ila naona mkuu anakichukulia poa, watu wanalia, na ukiwa siriasi ni gharama sanaaa unless ulime vituta viwili vitatu...
hakunakisicho na gharama duniani...kila kitu kina uchungu na utamu wake
 
Acha ungese,wewe mwenyewe hujawahi kulima unaleta pumba pumba zako.
Mkuu Mimi Situkanani na Wahuni wa Mitaani nazungumzia Nina Experience Mimi Pia Nina Degree Mbili Tofauti si wakaida kama Unavyonifikiria Ni Mtu ninayethubutu.
 
Sasa nilisoma nilime...ujue msitake kutulazimisha wote tulime mimi naenda chuo nikawe muhandisi wewe unaniambia nilime eti kisa fulani analima..

.Katika maisha kila mtu ana ndoto zake sijawahi hata mara moja kuwaza kulima ntapambana na bahasha zangu kila mahala mpaka nitimize adhma yangu...

Nchi inakosa economic diversification kisa stereotypes na mikumbo ya kishenzi kama hio. leo hii hadi proffesor anafuga kuku
Kwani Kufuga Kuku ni dhambi Jamani Watu wa Moshi Mtakua Mnafahamu Kule Maeneo ya Shanty Town karibu na kwa Reginald Mengi Kuna Mtu anafuga Kuku Eneo la Ekari Tatu ame lifence yule ni Billionnere watu wanakusanya Mayai zaidi ya Trey 350 anauza Kuku naona Ana supply Moshi na Arusha.

Kwa akili yako Professor akifuga Kuku ani Mjinga

Hii Mentality mliyonayo hamtaendelea kama Unaona aibu Kufanya Mishe za Kilimo au Ufugaji Nenda Sehemu ambayo hawakujui

Degree haipo kwenye Paji la Uso so hawawezi kukugundua njooni tulime mabishoo wa Mjini.
 
Tuamke tukaanze Kilimo wakuu hali ni mbaya siyo lazima wote mkaajiriwa. Mimi Roho huwa inaniuma Mtu anavyokuja na Kuandika thread nataka Sehemu ya Kujitolea bila Malipo hebu Imagine Sehemu hiyo unayojitolea vipi kama ungekua umeanzisha Kilimo cha Ekari Mbili za Vitunguu au ungekua unamiliki mgahawa kwa Pesa ulivyotumia kununulia Galaxy S7


Si sifa Asubuhi kuvaa Kiminini na high heels au Kuchomekea shati tayari kwenda kutumwa tena bure kuna Projects ulipiga Mara Mbili Kipato cha Mfanyakazi wa Halimashauri anayeanza Kitakua Mara Mbili

Nakumbuka mwaka 2016 Mfanyakazi wa Halimashauri mwenye Degree za Kawaida kama Uhasibu, Sheria ilikua ni 716,000/= before statutory deductions

Hapo Piga
NSSF= 10%
NHIF=3℅
Workers Comp=1℅
HESLB=15℅
Tax=25 Plus 14℅ ya Level 3

Aisee huyu Jamaa anaweza Kujikuta kwa Mwaka anapokea Tsh. 6,500,000 kwa mwaka kama Mshahara

Kuna Project sitazitaja ukizikodolea Macho unaweza kupiga Mara 3 ya hizo Pesa kwa mwaka wa 1.


Mimi mwenyewe nataka Niache Kazi tukapambane nimechoka Kutumwa.

Leo Rais Jakaya Kikwete alikua anakagua shamba lake Msoga.
View attachment 510659 View attachment 510660 View attachment 510661

Uzi huu nitauongezea Nyama Usiku Nikitulia najua Reactions za watu zitakua negative sana.

UPDATE 2 (Vitu nilivyojifunza)
Baada ya Kusoma Comments za Matusi ya Baadhi ya watu nimelia nimetoka Mafua ni Flue Mtindo Mmoja.

Kwa Kuangalia tuu mwandiko physiologically Ni Majibu ya watu wenye Hasira waliotapeliwa na Waalimu wao wa Vyuo.

Kitu kingine nilichogundua watu hawajui hata Ukubwa wa Ekari Moja Ukoje anaanza gharama za Kulima sijui Tsh. 50,000/= Daah yaani hata Kilimo cha Ekari 2 ya Viazi Mviringo au Vitunguu unataka Ufahari wa mtu akulimie?

"Mtoto wa Masikini'' Nimesikitishwa na Phrase hii imekua ikitumiwa na Wengi yaani wanaona Umasikini ni Sifa badala ya Kujinasua. Mimi binafsi Maneno hata ya aliyekua mkuu wa Mkoa wa Morogoro yalinitisha Dr. Ambaye ni Mkuu wa Mkoa anasema yeye ni ""Mtoto wa Masikini"" niwakumbushe tuu kuna Umri ukifika hata Kama huna wazazi wote hautakiwi kujiita ''Yatima'' hili naona ni jina linalotumika kwa Watoto wadogo.


Mentality za Wengi wanataka Kuanza na Kilimo cha Ekari 100 wakati hata Ekari Moja hajawahi Kuthubutu.

Kila Kitu kina Gharama zake na Uncertainties zake Sasa unajua Kabisa Nyanya na Mvua haziendani huo ndo Muda wako wa Kuzilima sasa kwa sababu zinakua Chache wewe unakuja Kulima wakati wa kiangazi wakati kila mtu amelima Mwisho kitakua chakula cha Nguruwe.

Kumtumia Rais Jakaya Kikwete wengi wamechukulia jinsi lilivyo hawajawaza Kua nimemtumia JK kama Kuonesha kuwa Kilimo si Kazi ya Kudharaulika kama wanavyofikiri baadhi ya Graduates.

Ni kweli uliondoka Kijijini Taangu ulivyomaliza darasa la 7 unarudi Likizo Ukiwa na Kakimini kako na High heels unatingisha tutako au kama Mwanaume Umechomekea kishati chako huku umenyoa Kiduku Mimi Leo kukuambia Ulime utaniona Kama nimechanganyikiwa.

Raia/graduates wengi wamepanic ni Lazima kwa sababu tumeingia New Era tusijifananishe na Wakati wa JK amemaliza Chuo wakati kuna Chuo Kikuu kimoja tuu UDSM watu mpaka mwanzoni Mwa miaka ya 2,000's ulikua ukimaliza Chuo unasubiri Barua ya Post na si kwenda watu hawa walikua hawatembezi Bahasha za Khaki wala kupambana kwenye Interview Leo hii Nyinyi wenyewe mashahidi ikitangazwa Kazi mnavyokua wengi, Yote haya ni Maendeleo ya Elimu huku sekta nyingine zikiwa bado so Nchi kama za Nigeria wenzetu walishazoea hii Hali Mimi ni member wa Forum Moja maarufu ya Nigeria Najichanganyaga Kuchukua maujanja.

Tofauti za Mitazamo zisitufanye Kudharauliana Kuna Baadhi ya Members unagundua tuu kasoma Heading halafu Moja kwa Moja akaenda kuporomosha Matusi kuna Comment ya ""Tukiwa wote wakulima nani atanunua''' ni Wazi huyu mtu hajasoma hata maneno niliyo yabold hapo juu akaingia Moja kwa Moja Kwenye Matusi.

Inferiority Complex ni Kubwa sana na sijui tutaiondoaje mtu anajikuta anaogopa tuu na Kuanza Kusifikia Kilimo Balaa, Kilimo nomaaa, Kilimo Kigumu Sanaaa! Leo hapa hata Ukimwambia Mtu Chukua Laki 5 nenda kachichimbie Singida Nunua Tetea 40 ambao hawajaanza Kutaga na Jogoo 6 ambao hawajaanza Kuwika Lazima Watu watakuja Kusema Unajua Kufuga wewe Kufuga ni Gharama, Kufuga kunahitaji Mtaji, Kufuga Ni Kipaji! Those kind of blah! blah! and excuses wakati Kuku wa Kienyeji wanajitafutia wenyewe hata kama ukikosa pesa ya Kuwanunulia Pumba Siku hiyo na dawa zake Nyingi hasa za tumbo ni 3,500= na Ile ya Matone hadi 7,000/=.


Sasa Kaa Pambanua Mwenyewe Uendelee Kusubiri Mpaka Utakapokua Rais then Ustaafu kama Kikwete ndo Ulime au Uchakarike na Kiasi Kidogo ulichonacho Ku extend capital.
Nasubir nistaafu ndo ntalima
 
Ulie andika hii mada kua mwelewa. Kilimo anacho fanya Jakaya sicha kawaida. Kimezungatia taratibu zote za kilimo ambazo ni ghali sn. Mtu katoka chuo hzo pesa anaztoa wap pengine kwao hata shamba hamna. Tatizo ni aina ya elimu inayo tolewa Tz graduates siwa kulaumu.
 
Yaani watu wanadhani utalala tu uamke na ekari mia mbili,hawajui kuwa lazima uanze chini ili ufike juu...

People have to change the Mindset
Acha waendelee kuona haiwezekani mkuu

Kwanza ni vigumu sana mtu kufanikiwa kwa mtaji wa kupewa au kukopeshwa
Hasa kwa kuanza na mtaji mkubwa.
 
Hahaha...kweli aisee maana nilikuwa nahitaji utaalamu wa vitunguu bhana,nikaeenda halmashauri kwa afisa kilimo,si kaniingiza mkenge....kuanzia hapo nawa consult wakulima tu wana ujuzi wa kutosha kuliko graduates(baadhi)

....Uko sahihi, yaani ni much better ku consult several farmers utaambulia kitu kuliko hawa wataalamu wetu wa kilimo. Mtaalamu wa kilimo hata heka mbili hana, ananunua mahindi, mchele n.k just like someone in Dar???
 
Angekuwa mtoto wa kikwete ndio analima ningeshawishika lakni kumbe ni mzee kikwete aliyekula ujana kwenye kiyoyozi na ofisini wala sishangai.
Kilimo chahitaji mtaji acha nasi tuutafute ofisini tutalima uzeeni

Saa nyingine mtu akisema eti JK analima kisha ndio anatolea mfano huwa simuelewi. Umemuona JK yuko shambani na aina ya nguo alizovaa utadhani anaenda pub. Ni wakulima wangapi wanauwezo alio nao JK?

Tushawishiane kuhusu kilimo lakini sio kumuonyesha JK eti ndio tuvutiwe kulima.
 
hakunakisicho na gharama duniani...kila kitu kina uchungu na utamu wake
...uko sahihi kabisa boss, akini kulinganisha na nini..? unaposema kulima ni afadhali kulikokuzunguka na bahasha nakataa kabisa...
 
....Uko sahihi, yaani ni much better ku consult several farmers utaambulia kitu kuliko hawa wataalamu wetu wa kilimo. Mtaalamu wa kilimo hata heka mbili hana, ananunua mahindi, mchele n.k just like someone in Dar???

Ndio hao waliojaa toop maofisini....kwa kweli ni mzigo tu wa bure kwa kuwepo ofisini
 
Unafananisha vitu visivyofanana. Nadhani ungejikita zaidi katika kutoa njia za kupata mitaji mikubwa ili uweze kufanya vitu vikubwa zaidi.
 
Duuuh..

Save hela za bando,within no time utapata hela ya mbegu etc

Guys people start from scratch!! Mimi ilinibid nijinyime haswaaa ili kuweza kuanza na bado najinyima ili nifike somewhere......kwangu every cent counts....yaani ninanua mfano bando kwa bajet maalumu,ikiisha kabla ya muda niliopanga sinununui unless iwe muhimu sana...

Hata kupiga simu ambazo hazina tija niliacha sijui kuongea umbea flani hivi,story hazina tija,blablaaaa sina ....

Mfano pia vijana wengi wanatumia hela nying kustream movies na kushinda Instagram...Guys ukilimit haya mstumizi tu bila kupunguza kwingine unapata pesa ndani ya muda mfupi tu

Tuamke jamani...nnnn
Asante dada TATIANA nakupata sana yani,,, endelea kumwaga nondo…!!!!
 
Back
Top Bottom