Jakaya Kikwete aliwezaje kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja?

JOESKY

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
816
2,032
Wasaalam ndugu wana jamvi!!

Nimefikiri kwa marefu na mapana bila kupata majibu ya baadhi ya maswali yahusuyo utawala wa Dr Jakaya Kikwete enzi za utawala wake. Ni miaka kadhaa imepita sasa toka mzee wetu arudi kijijini kwao Msoga kuendelea na maisha yake ya kawaida baada ya kumaliza muda wake wa kuongoza.

Kuna vitu vingi na vikubwa mno vilifanyika enzi za Jakaya Kikwete lakini havikuzuia mambo mengine kwenda sawa bin sawia.
Kuna nyakati mambo yalikuwa yanakwama lakini yanatatulika ndani ya muda mfupi mambo yalikuwa yanakaa sawa.

Mfano wa vitu ambavyo alivimudu Jk pasi na kuteteleka ni pamoja na:

- Nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kila ufikapo mwaka mpya wa bajeti

- Ajira za uhakika pasi na urasimu

- Miundo mbinu ya barabara

- Ujenzi wa madarasa na shule za kata

- Ujenzi wa zahanati na hospitali

- Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

- Uwekezaji wa pesa kwenye tafiti mbali mbali zihusuzo mambo ya Uchumi kwa ujumla

- Vikao na semanars kwa maafisa wa idara mbalimbali(hawa wote walipata posho zao bila bughuza?)

*NA MENGINE MENGI.

Lakini nchi ilienda na Mzunguko wa pesa mtaani ulikuwa mkubwa biashara zilikuwa zinakua kila uchao kukaongeza wimbi la wafanyabiashara na wawekezaji wa nje na ndani ya mipaka ya nchi yetu. Mashirika na makampuni yalinawiri kwa utajiri na yalitoa ajira kwa ukubwa usio kifani.

Sasa swali langu kwa awamu hii pamoja na kubana matumizi na uzibaji wa mianya ya Rushwa kwa ukali wa hali ya juu ni nini kinachofanya tusione matunda ya huo mfumo? kama mishahara ya watumishi imebaki constant bila kuongezwa tokea JK aondoke???_Suala la ajira lipo wazi sitaki hata kuligusia kwa kifupi hakuna ajira za uhakika awamu hii lakini bado kunaonekana kuna uhaba na umasikini mkubwa kwa taifa na mtu mmoja mmoja??

Nawakaribisha mezani tutete!!
 
Yule mzee wa Msoga alikuwa bomba sana aisee.Alijali Sana uchumi wa wananchi.
Nikiri hata mimi kweli alikuwa bomba sana, kila mtu alimwacha afanye anavyotaka, majambazi yaliba mchana kweupe, banki zilivamiwa hadharani na wazi, mafisadi yaligawana pesa kwa magunia, rushwa ilikuwa waziwazi na watumishi ilikuwa ni halali kuingia kazini akiwa kachelewa au haingii kabisa kazini
 
Yule kazi ya Urais aliiweza, kuifurahia na haikuwa mzigo kwake

Huyu mwingine mchato kila siku si mwasikia aropoka na kudai kazi hii ni nzito na hata hafurahi kabisa kazi hii so tuendelee kuvumilia tu kwa sababu ya ujinga wetu na uoga wetu
 
Katika kipindi cha huyu mzee aisee niliokota sana pesa kwangu elfu 5, 10, 20, 50 hata laki,... hazikunipiga chenga.

Naweza toka mishe gafla nakutana na pochi au waleti zimejaa minoti hatari.

Kipindi kile pesa zilikuwa nje nje na mzunguko ulikuwa mzuri sana. Ila toka huyu mkulu aingie madarakani pesa kubwa niliyookota ni mia tano huwezi amini.

Hiyo inaleta tafsiri kuwa hali ni ngumu sana sasa hivi, hata mzunguko wa hela umekuwa finyu sana kiasi kwamba hata mia tano ukiwa nayo unailinda kama mboni ya jicho.

Abarikiwe sana huko alipo huyu mzee kikwete japo na yeye hakuwa perfect ila itoshe kusema alikuwa bora sana.

Kwangu mimi huyu alikuwa bora sana kuliko huyu mpenda sifa na mapambio.

Ni mtazamo tu.
 
Si tuliambiwa huyu wa sasa yuko bize ananyoosha nchi kwanza na kuongeza vitega uchumi ndipo baadae ajira na mishahara viwe maradufu.
 
Mnaolalamika maisha magumu mlikuwa wapigaji tu kipindi cha JK. Eti "naweza toka mishe ghafla nakuta pochi imejaa minoti". Hivi pesa inaweza kuwa rahisi kiasi hicho mahali gani pengine wapi duniani? Siyo kipindi cha JK watu walikuwa wanajilia rushwa wanavyotaka.
 
Lkn pia neno UFISADI lilikua maarufu sana enz hizo ........

Pia uchumi ulishuka sana
 
Napendekeza katiba irekebishwe agombee tena tupate unafuu wa maisha. Nina imani atarekebisha madhaifu machache yanayozungumzwa kuhusu yeye. Ikumbukwe kuwa "No one is perfect".
 
Back
Top Bottom