Elections 2010 Jakaya anaelekea kudesa sera za slaa bara dogo la mawaziri

Lalashe

Member
Nov 4, 2010
84
1
Pamoja na Sera za msomi Dr. Slaa kuwa nzuri na Mkwere Kikwete kuzikubali, atakuwa na ubavu wa kujitenga na mafisadi na kuteuwa baraza dogo la mawaiziri pamoja na speaker wa bunge ambaye si fisadi? Wanajamii mmelisikia hilo kupitia vyombo vya habari vya chama cha majambazi? Na je Kikwete anaweza kujitenga na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma?
 
Uteuzi wake wa mwanzo hautupi imani; kwani Mh. Werema tangu ateuliwe hajajipambanua kama mtu makini. Itakumbukwa alimpelekea rais mswada wa gharama za uchaguzi ili auwekee sahihi wakati umechakachuliwa. Kama hiyo haitoshi, ushauri wake kuhusu marekebisho ya katiba yaliyoifanya Zanzibar kuwa nchi yanatia shaka. Na hivi juzi juzi alishindwa kuishauri serikali vizuri kiasi kwamba Shein akaapishwa kuwa rais wa zenj. huku bado akiwa makamu rais wa Tanzania, jambo ambalo ni kinyume na katiba.
 
Mie sio nshomile ila nimekuelewa vizuri mkuu ! Aksante
 
Hilo ni kweli nadhani raisi wetu si makini katika maamuzi yake hivyo tutegemea mambo ya ajabu na aibu kutoka kwake labda utokee muujiza katika Brains za mtu wetu?
 
Hilo ni kweli nadhani raisi wetu si makini katika maamuzi yake hivyo tutegemea mambo ya ajabu na aibu kutoka kwake labda utokee muujiza katika Brains za mtu wetu?
Hakuna muujiza utakaotokea, na tusitegemee mabadiliko kutoka kwa huyu rais.
 
KAA LA MOTO-Ni kweli sijaenda shule hata la nne sijafuzu. Nafasi ya kwenda shule nimekosa kutokana na ukweli kwamba utawala uliopo ulininyima nafasi ya kwenda shule na kuwa na elimu kama wewe. Lakini usijali najitahidi kujisomesha madarasa ya watu wazima ili siku moja nami niwe kama wewe usiyefanya makosa. Ninachoomba kwako ni msaada ili nijikomboe kutokana na hali ambayo hata mimi ninaichukui na inanikasirisha sana.
 
2005 Sikumpa Kura Yangu JK; 2010 Sikumpa Kura Yangu JK. Kwa Sababu JK Ni Chekibobu. Siwezi Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Bora Nife Tu, Kuliko Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Chekibobu Hastahili Kuwa Rais wa TZ. Ndiyo Maana Tuna Matatizo Mengi Kwa Sababu ya Huyu Chekibobu JK.
Hii msg yako inamrengo flani wa ki anti-fisadi! inaonekana ulikuwa unataka kughani...Ebu tupe sifa za Chekibobu!
 
Akidesa tu ndio kifo cha CCM sababu watakua wanaendesha gari ambalo hawalijui vizuri, kumbe limetegwa alarm wasione pa kulidisable likawazimikia. Sera zote walizoziiga toka upinzani zimewashinda
 
Byenda, you have a valid point: kwa uteuzi wa kwanza, JK hana jipya! Let's just wait and see atadesa kiasi gani!
 
nadhani baraza lake la mawaziri litakuwa na sura kama hii:
rais atafuta baadhi za wizara na zingine kuziunganisha na atakuwa na baraza dogo sana!!!!

1) waziri mkuu-
2) mambo ya nje na uhusiano wa EA-
3) fedha na uchumi-
4( sheria na katiba (mambo ya ndani kufutwa)-
5) ulinzi-
6) elimu-
7) kilimo, mifugo na uvuvi-
8) kazi na maendeleo ya jamii-
9) afya na mazingira-
10) ardhi, mawasiliano na miundo mbinu-
11) madini, mali asili na utalii
12) utamaduni,wanawake, na watoto

Wizara kama habari na michezo azifute na kila wizara iwe ina msemaji wake huku michezo ikisimamiwa na vilabu vyao.
Mambo ya ndani ifutwe na kazi zake zifanywe na wizara ya katiba na sheria.

Hakuna haja ya kuwa na mawaziri wadogo kazi zao zifanywe na makatibu wakuu na kwa hakika serikali itawajibika vilivyo na kupunguza gharama!!!

ombi langu kwa rais ni kuwa awajumuishe wapinzani ktk serikali yake ili kujenga umoja wa kitaifa na kwa kuanzia ampe Lipumba wizara ya fedha na uchumi huku dr. Slaa apewe wizara ya sheria na katiba!!!
 
KAA LA MOTO-Ni kweli sijaenda shule hata la nne sijafuzu. Nafasi ya kwenda shule nimekosa kutokana na ukweli kwamba utawala uliopo ulininyima nafasi ya kwenda shule na kuwa na elimu kama wewe. Lakini usijali najitahidi kujisomesha madarasa ya watu wazima ili siku moja nami niwe kama wewe usiyefanya makosa. Ninachoomba kwako ni msaada ili nijikomboe kutokana na hali ambayo hata mimi ninaichukui na inanikasirisha sana.
 
Na je Kikwete anaweza kujitenga na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma?
Lalashe, wewe unaweza kujitenga na wewe mwenyewe?! Kama ukiweza basi Kikwete naye ataweza kujitenga na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma. Na habari ndiyo hiyo
 
nadhani baraza lake la mawaziri litakuwa na sura kama hii:
rais atafuta baadhi za wizara na zingine kuziunganisha na atakuwa na baraza dogo sana!!!!

waziri mkuu-
mambo ya nje na uhusiano wa ea-
fedha na uchumi-
sheria na katiba (mambo ya ndani kufutwa)-
ulinzi-
elimu-
kilimo, mifugo na uvuvi-
kazi na maendeleo ya jamii-
afya na mazingira-
ardhi, mawasiliano na miundo mbinu-
madini, mali asili na utalii
utamaduni,wanawake, na watoto

wizara kama habari na michezo azifute na kila wizara iwe ina msemaji wake huku michezo ikiwa chini ya waziri wa utamaduni. Mambo ya ndani ifutwe na kazi zake zifanywe na wizara ya katiba na sheria.
hakuna haja ya kuwa na mawaziri wadogo kazi zao zifanywe na makatibu wakuu na kwa hakika serikali itawajibika vilivyo na kupunguza gharama zake!!!

ombi langu kwa rais ni kuwa awajumuishe wapinzani ktk serikali yake ili kujenga umoja wa kitaifa na kwa kuanzia ampe lipumba wizara ya fedha na uchumi huku dr. Slaa apewe wizara ya sheria na katiba!!!

Don't ever think of it, Dr. Slaa awe chini ya huyo mkwere!!!!!! Kamwe hawezi kukubaliana na hilo
 
KAA LA MOTO-Ni kweli sijaenda shule hata la nne sijafuzu. Nafasi ya kwenda shule nimekosa kutokana na ukweli kwamba utawala uliopo ulininyima nafasi ya kwenda shule na kuwa na elimu kama wewe. Lakini usijali najitahidi kujisomesha madarasa ya watu wazima ili siku moja nami niwe kama wewe usiyefanya makosa. Ninachoomba kwako ni msaada ili nijikomboe kutokana na hali ambayo hata mimi ninaichukui na inanikasirisha sana.
Usijali mimi ni mwalimu wa upe nilimaliza darasa la kumi la zamani. Nitakusaidia when in need.
 
Back
Top Bottom