Jakaya 2011 hiyo: Zile ahadi vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya 2011 hiyo: Zile ahadi vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Julius Kaisari, Jan 25, 2011.

 1. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Aisee chalii, kumbuka yale maahadi uloyatoa wakati unaomba kula, ndugu kufumba na kufumbua 2012 hiyo,..au utimilize sifa yako ya sanaa,pale tbc1 uwambie watanganyika ulikuwa unawazuga,maana hawatakufanya chochote.. Ndiyo..siulipiga mafix mchana kweupe?, ndiyo siunakumbuka wanaccm walikusifu umbumbu ule,eti Handsome rais kijana,ukafikiri utautumia huo kwenye uchumi? Ndiyo,siulifikiri wazungu ukipiga hodi na kuchekacheka watakupa mafweza? Ona sasa budget yenyewe hiyo,imekubumia! Mwaka huu unalo..hadi tukung'oe, peoplesssssssss powerrrrrrr!..
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ahadi zenyewe za Dr. Jakaya Mrisho Kikwete hizi hapa: Tukumbushane kwa ajili ya kuwajibishana mwishoni mwa safari:

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora

  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini

  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga

  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga

  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma

  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini

  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma

  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera

  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera

  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini

  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini

  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera

  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera

  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera

  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya

  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera

  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza

  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye
  20. vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza

  21. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita

  22. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba

  23. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro

  24. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini

  25. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa

  26. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea

  27. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya

  28. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga

  29. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa

  30. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na

  31. kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro

  32. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini

  33. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora

  34. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu

  35. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini

  36. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo

  37. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara

  38. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma

  39. Kulinda haki za walemavu- Makete

  40. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini

  41. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha -Arusha

  42. Kutengemeza Barabara za Juu (Ubungo, Magomeni, Tazara, Chang'ombe/Nyerere Rd) - Dar es Salaam

  43. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu - Shinyanga Mjini

  44. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora

  45. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini

  46. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida - Dodoma

  47. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-

  48. Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga

  49. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini

  50. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .

  51. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido

  52. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro

  53. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na
  54. kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara

  55. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini

  56. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini

  57. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa

  58. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa

  59. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo
  60. hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa

  61. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda

  62. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara

  63. Kujenga Majengo ya Wamachinga (Machinga Complex) Matano (5) - Dar es Salaam

  64. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo, Iringa

  65. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar

  66. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar

  67. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti

  68. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma

  69. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma

  70. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma

  71. Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma

  72. Hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi - Dar es Salaam

  73. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara

  74. Ujenzi wa kiwanda cha dawa ya kuua viluilui vya Mbu - Kibaha

  75. Hospitali ya Tumbi kuwa ya Mkoa - Kibaha

  76. Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la Viwanda - Kibaha
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hatatekeleza ahadi 10 tu kati ya hizo zote 76
   
 4. olele

  olele JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  kuna owongo unaozungumza,ila huu unapayuka, sijui kwa nini watu hawakuelewa.
   
 5. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Mi nikiangalia mlolongo huo na hali ilivyo,naishia kucheka..Jakaya hana hata mshipa wa aibu..au ndo usanii wenyewe..ninawasiwasi kama kitafanyika kitu. Ujue kwa nadharia za uchumi, kwakuwa budget ya 2010/11 inaoneka kufail utekelezaji,ni wazi vipaumbele vyake vitasogezwa budget ya 2011/12,na ukumbuke kati ya hizo projects,au zote zahitaji trilions,je kiuhalisia,zipo??kujenga International Airport Bagamoyo! Teh teh teh.. Amakweli wonders never cease!
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Msanii ni msanii tu, after all kwani atarudi tena kuja kuwapigia magoti kuwaomba kura, ishakula kwa wabongo kwa kuamini mafix yele!!!:heh:
   
 7. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  anajua hata asipotimiza 2015 hatakuwepo knye kuomba kura
   
 8. escober

  escober JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  inabidi tuwe tunatick kila ahadi inayotimizwa ili next election tuwe na sababbu zingine za kuishangaza ccm
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,438
  Likes Received: 19,798
  Trophy Points: 280
  hatatimiza ahadi hata moja
   
Loading...