Jaka Mwambi huyoo kaenda Urusi sasa

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
RAIS Jakaya Kikwete jana alimwapisha mwanasiasa mkongwe nchini, Jaka Mwambi, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.

Kabla ya uteuzi wa Mwambi, Balozi wa Tanzania Urusi alikuwa Patrick Chokala.

Rais Kikwete pia alimwapisha Mohamed Haji Hamza kuwa Balozi, na George Mlawa kuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kutokana na uteuzi huo, Haji Hamza anakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Zanzibar.

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, walikuwa miongoni mwa viongozi wa serikali walioshuhudia viapo hivyo Ikulu, Dar es Salaam.

Mabalozi wapya wameahidi kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kutotoa siri bila idhini ya Rais.

Balozi Mwambi alisema uteuzi huo ni changamoto kubwa kwake, hasa kwa kuzingatia utekelezaji sera ya serikali ya diplomasia ya uchumi. Mwanasiasa huyo aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa katika mikoa kadhaa nchini na mara ya mwisho alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.

Kamishna Mlawa aliapa kuwa wakati anatekeleza majukumu yake hatatoa siri bila kibali cha tume.

Rais aliwapongeza mabalozi wapya na Kamishna Mlawa kwa uteuzi huo na akamweleza Haji Hamza kuwa awe na imani kuwa ataweza kumudu changamoto mpya zinazomkabili.
 
Mwambi anapoenda URUSI JE TANZANIA ITANUFAIKA VIPI ?
ASISAHAU KUWAKUMBUSHA URUSI MAHUSIANO YAO NA YETU...WATUFUNGULIE VYUO...WASOMESHE MADAKTARI WETU...WAENDELEZE VIWANDA VYETU...WATUJENGEE MAHOSPITALI......MAJI...BARABARA.....UMEME....! OOOH URUSI ULIYEKUWA KIPENZI CHA TANZANIA KUMBUKA MAHUSIANO YAKO NA UTUTENDEE KAMA HAPO MWANZO ENZI ZA MWALIMU...!
 
Huyo Jaka Mwambi ni mjumbe wa NEC CCM sasa sijui kila kikao cha NEC atakuwa anakuja kutoka Urusi?
 
Sitashangaa Lowassa na Rostam wakipewa posts hivi karibuni...Rosta balozi US, EL - Zimbabwe
 
Sitashangaa Lowassa na Rostam wakipewa posts hivi karibuni...Rosta balozi US, EL - Zimbabwe

jaka-mwambi-2007-02-22.jpg

Usimsahau Brother Ditto labda na yeye atapelekwa Saudia. Hivi kweli tuna raisi hapa au tumempa mtu nchi aichezee??
 
Mwambi anapoenda URUSI JE TANZANIA ITANUFAIKA VIPI ?
ASISAHAU KUWAKUMBUSHA URUSI MAHUSIANO YAO NA YETU...WATUFUNGULIE VYUO...WASOMESHE MADAKTARI WETU...WAENDELEZE VIWANDA VYETU...WATUJENGEE MAHOSPITALI......MAJI...BARABARA.....UMEME....! OOOH URUSI ULIYEKUWA KIPENZI CHA TANZANIA KUMBUKA MAHUSIANO YAKO NA UTUTENDEE KAMA HAPO MWANZO ENZI ZA MWALIMU...!

Mawazo tegemezi na omba omba mtaacah lini ? Urusi wenyewe njaa kali demokrasia hakuna bado unasema kwamba .............................
 
Mwambi anapoenda URUSI JE TANZANIA ITANUFAIKA VIPI ?
ASISAHAU KUWAKUMBUSHA URUSI MAHUSIANO YAO NA YETU...WATUFUNGULIE VYUO...WASOMESHE MADAKTARI WETU...WAENDELEZE VIWANDA VYETU...WATUJENGEE MAHOSPITALI......MAJI...BARABARA.....UMEME....! OOOH URUSI ULIYEKUWA KIPENZI CHA TANZANIA KUMBUKA MAHUSIANO YAKO NA UTUTENDEE KAMA HAPO MWANZO ENZI ZA MWALIMU...!

........Chingwanji yaani umeniwahi...........kweli kabisa haya mawazo mengine ya kuwa omba omba sijui yatatutoka lini.........

....mahesabu please.......au kuna mtu kaiba na antumia ID yako!!!
 
mwalimu anapofundisha darasa la wanafunzi 70....hutokea baadhi ya wanafunzi wachache ambao pindi test itolewapo na mwalimu yule yule kwa mada ile ile hupata maksi za chini mno....kwa wanafunzi wakiulizwa na wazazi husema mwalimu hakufundisha....wakiulizwa na mwalimu husema hatukukuelewa kwani uliingia kipindi hakikuwa chako hivyo minds zetu hazikuwa tuned ktk somo lako nk.....ili mradi LILILOTOLEWA NA MWALIMU HALIKUELEWEKA VYEMA KWA WANAFUNZI HAWA.......(let me put the flesh)
WE ADOPTED SOCIALISM FROM USSR......KUTOKA NCHI HII NDIPO TULIPOPATA MAWAZO YA KUJITEGEMEA (ujamaa &kujitegemea).......NOW JAKA IS GOING THERE WHILE THE POLICIES OF THESE TWO COUNTRIES HAVE CHANGED ALOT FROM WHEN THEY JOINED TIES....! ITS NOW ECONOMIC DI[PLOMACY........!ITS ALL ABOUT HOW RELATIONSHIP OF THESE TWO COUNTRIES CAN BENEFIT TANZANIA &VICE VERSA....!
AT HOME WE HAVE OUR PROBLEMS......ROADS....HOSPITALS...WATER...ELECTRICITY...ADUCATION.....INDUSTRIES....TRANSPORT....AND MANY MORE!
HOW RUSSIA IS GOING TO BENEFIT US...?
IS IT CLEAR SIRS....!
 
Nampongeza Bw. Jaka Mwambi kuteuliwa kuwa balozi huko Urusi, namtakia utendaji mwema ktk majukumu yake ya kila siku.

Hivi jamani Balozi anatakiwa kuwa na sifa gani? au mtu yeyote anaweza kuteuliwa tu kwa kadri Rais atakavyo amua?

Mimi nadhani ubalozi si nafasi ya kisiasa, ni wadhifa unaopaswa kuambatana na utalaam. Yaani awe na elimu inayohusiana na masuala ya kimataifa au kupandishwa vyeo Maafisa ubalozi.

Wenzetu wa Kenya (licha ya matatizo yao pia) lakini hata wakuu wa wilaya (DCs) ni watalaam siyo wanasiasa. Rais anamteua DC kutoa ktk orodha ya watalaam wa kada hiyo.

Madaraka ya Rais ni makubwa mno.
 
Mkuu Nziku,

Heshima mbele, ubalozi kwa kawaida ni nafasi maalum kwa ajili ya rais kuwapa waliomsaidia kushinda uchaguzi, the matter of fact sisi bongo ni moja kati ya nchi chache sana duniani ambao angalau tunajali qualifications,

Kuna nchi kama USA, mwananchi mmoja tajiri alimchangia Bush kwenye kampeni, na kudai anataka ubalozi Italy, mwingine alidai ubalozi wa Kenya, ili atuime muda mwingi kwenda mbugani, na hawa walisema nia zao mbele ya public, na Bush aliposhinda wakawa.
 
Muu are you saying to justify something or you are serious na maneno yako ? Hebu lete majina ya hawa mabalozi tuone .Pia si lazima tufuate what US they do .Sisi ni Taifa huru na tuna maamuzi ya namna ya kuendesha Taifa letu .Nadhani kuwa Balozi isiwe asante but mtu awena uwezo na qualifications fulani .
 
Mkuu Nziku,

Heshima mbele, ubalozi kwa kawaida ni nafasi maalum kwa ajili ya rais kuwapa waliomsaidia kushinda uchaguzi, the matter of fact sisi bongo ni moja kati ya nchi chache sana duniani ambao angalau tunajali qualifications,

Kuna nchi kama USA, mwananchi mmoja tajiri alimchangia Bush kwenye kampeni, na kudai anataka ubalozi Italy, mwingine alidai ubalozi wa Kenya, ili atuime muda mwingi kwenda mbugani, na hawa walisema nia zao mbele ya public, na Bush aliposhinda wakawa.

sawa mkuu Field Marshall ES, Urais unamarupurupu mengi, tuombe tuwe tunapata marais wanaoweza kuyatumia madaraka yao vizuri.
 
MESAGE TO JAKA!
Tell the russians about our kilimanjaro.....victoria...serengeti....!
Tell them about the vast land we have,they can come and invest in agriculture........irrigation etc! hoping that they have ujamaa spirit they cant do like what "boers" and others are doing to our country especially "bogus treaties"
 
Inasikitisha kuona watu waliosoma diploamsia na kufanya kazi balozini kwa miaka mingi, au waliofanya kazi MOFA na kupata uzoefu wa diplomasia na ushirikiano a kimataifa kwa miaka mingi wanaachwa halafu kazi za ubalozi zinakuwa zawadi za kisiasa kama alivyosema FMES.

Regardless kama nchi nyingine wanafanya hivyo, it is wrong and one day it will backfire.

Mkuu mmoja kasema huyu bwana mjumbe wa NEC sasa vikao atahudhuriaje? Pius Ng'wandu ilibidi auteme ubalozi wa Tanzania Japan baada ya watu kumlalamikia kwamba yeye kama mbunge asingeweza kuwawakilisha watu wa jimbo lake akiwa Japan.What about this case?
 
hope atachukua uamuzi wa busara .....!
 
Mwambi anapoenda URUSI JE TANZANIA ITANUFAIKA VIPI ?
ASISAHAU KUWAKUMBUSHA URUSI MAHUSIANO YAO NA YETU...WATUFUNGULIE VYUO...WASOMESHE MADAKTARI WETU...WAENDELEZE VIWANDA VYETU...WATUJENGEE MAHOSPITALI......MAJI...BARABARA.....UMEME....! OOOH URUSI ULIYEKUWA KIPENZI CHA TANZANIA KUMBUKA MAHUSIANO YAKO NA UTUTENDEE KAMA HAPO MWANZO ENZI ZA MWALIMU...!

Statements kama hizi ndizo zinazohalalisha matokeo ya utafiti wa Dr.Watson.
 
si kweli kwamba ubalozi ni zawadi kwa waliochangia mtu ashinde urais. japokuwa ni kweli baadhi ya nchi huteuwa watu mabalozi kama zawadi na wengine kama adhabu au kuwaondoa njiani watu wanaowaona tishio kisiasa.

hata hivyo nchi huwa makini katika uteuzi wa mabalozi katika nchi wanazoziona muhimu kisiasa na kiuchumi. mara nyingine sifa ya balozi unayempeleka nchi fulani huweza kuashiria uzito wa uhusiano kati ya nchi husika.

hii mambo ya kusema zawadi naona inakuwa taabu sasa kwani kuna mahali nimesoma mtu kapewa uwaziri kama zawadi kwani alikuwa timu ya ushindi.

chokala anakwenda wapi? au ndo matokeo ya masuala ya ukraine au ugombea urais. nauliza tuu
 
Mimi kwa mtazamo wangu nadhani kuteuliwa kwa Jaka Mwambi ni zawadi ambayo amepewa na kuachwa kwa Chokala ni matokeo ya Kugombea kinyang'anyiro na maswala ya Ukraine pamoja na kwamba kwa kipindi chake alichokaa Moscow pamekuwa nauhusiano mzuri wa Tanzania na Urusi katika nyanja ya elimu.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kuvunjika kwa uliyokuwa Soviet Union ni watanzania wengi (watoto wa walalahoi) walifaidika sana kwa elimu ya Urusi. Matokeo yake yako wazi maana popote utakapokwenda nchini tanzania iwe ni kweney yaliyokuwa mashirika ya umma, serikalini na makampuni binafsi lazima utamkuta mtu aliyesomea Urusi including Makamu wa Rais Dr. Shein (kama mnabisha fanyeni utafiti). Hii ilitokana na siasa ya Urusi ya kuzisaidia nchi changa maana ni watoto wa wakubwa wachache waliweza kupewa ufadhili wa kusoma nchi za Ulaya Magharibi ikiwepo Marekani.

Katika karne hii mambo yamebadilika mno na hata hivyo Tanzania bado ina vingi tu vya kufaidi kutoka Urusi kama uhusiano utarejeshwa. Ikumbukwe kuwa Urusi sasa hivi ni kati ya 7 top ecoomies in the world ikiwa mbele ya Italy na France, kwa hiyo yale mawazo ya kuwa Urusi haina kitu naomba wabongo wawe makini na kujaribu kuthibitisha kwa takwimu na siyo kusema tu kuwa Urusi ina nini....kwani Tanzania ina nini?

Nikirudi kwenye mada, naomba Jaka Mwambi aitumie hii nafasi ili kurejesha uhusiano wa kiuchumi maana warusi Technology wanayo na si matapeli kama wamarekani au nchi za Ulaya Magharibi (anyepinga amuulize Mkapa ambaye mwishoni aliona upuuzi akawaomba Wachina kutujengea uwanja wa kimataifa) na ndiyo maana sasa hivi wamarekani wanapiga sana kelele kuhusu demokrasia ya Urusi kwa kuijengea picha mbaya lakini warusi wenyewe wanajua wanachokifanya. Huwezi kuamnini kuwa baada ya kuvunjika kwa Soviet Union Urusi ya leo ndiyo ilirithi madeni yote ya nje (pamoja ya World Bank na IMF)ya hizo republic zingine lakini kwa kipindi cha miaka 10 tu iliweza kulipa madeni yote in advance kutokana na uchumi wao ulivyokua haraka.

Mungu ibariki Tanzania...kuna siku tutafika tu!
 
Putin aliifikisha hapo Urusi maana alikuwa kiongozi mwenye uchungu na mapenzi na nchi yake. Hakukubali kuacha mihimiri ya uchumi wa nchi kubaki mikononi mwa wageni, aliamini nchi yake ina wataalamu wa kutosha hivyo akuwatumia ipasavyo maana ndiyo wanaojua matatizo ya nchi na si kutegemea wataalam kutoka nje kama ilivyo kwetu. Hivyo aliweza kulipa madeni yote kwa kipindi kifupi na kutokana hilo. Alijua kama umdeni unapoteza uhuru wa kuamua kile unachokitaka. kwa lugha nyingine unabaki mtumwa wa yule anayekudai. Leo Tanzania ikiamua kutumia raslimali zetu kabla hazijaisha, nina imani hali bora ya maisha kwa kila Mtanzania inawezekana, nasema hali bora kimaisha maana hicho ndicho Watanzania tunachohitaji sana.
Dhana ya kutoa post za ubalozi kama zawadi inaweza isilisaidie Taifa hivyo sitaki kuamini kuwa ndicho kigezo kinachotumika. Kama Mtanzania ningeshauri Rais wetu azingatie uwezo wa kikazi na uadilifu kwa wateule wake. Yaani wewe upewe ubalozi wakati hujui lolote linalohusiana na post yako, kisha unitegemee mimi ofisa wako nifikiri kwa ajili yako!! Siyo rahisi! kila mtu anatakiwa kutimiza yaliyo penye job description yake maana analipwa mshahara kutokana na hayo aliyokubali kuyatekeleza.
 
Back
Top Bottom