Jaka Mwambi huyoo kaenda Urusi sasa

jaka-mwambi-2007-02-22.jpg

Usimsahau Brother Ditto labda na yeye atapelekwa Saudia. Hivi kweli tuna raisi hapa au tumempa mtu nchi aichezee??

Sijakuelewa hapa lawama zako zinabase upande gani? kuhusu uteuzi wa Jaka Mwambi ama?
Kwa taarifa yako Jaka Mwambi ni Jembe huyu jamaa na PM wa sasa ngoma Draw kwa wanaomjua huyu watasema, hiki ni kizazi cha akina Jeneral Ulimmwengu wanatumia kili sana na busara kwenye maamuzi. kwangu mi naona angeweza kumtumia kwa kazi za ndani kuliko kumpeleka mahali kama Urusi lakini kwa Captain Jaka Mwambi pia Urusi panamfaa kwa manufaa ya Kiusalama zaidi maana huyu ana medani za Kijeshi ambapo hawa tunawatumia pia.
 
FMES,
1. Sifa za Jaka ni zipi zilizompeleka maana yeye sio dipolomat?
2. Kama kuna wataalamu kuliko Jaka huko Moscow, yeye anafuata nini?

Mkuu ni Mabalozi wangapi unawajua wewe ambao ni Ma Diplomats ukitoa wachache kama akina Cisco Mtiro - Malaysia na wengineo, haya
Aliyekuwa mkuu wa JKT Mh. Balozi Makame Rasheed?
Aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Mh Balozi M.Lumbanga?
Mh. Mwanasheria Balozi Maajar taja yeyote hapo uniambie!!
Unapomteua mtu inategemea na nyie kama nchi mnafdaidikaje na uhusiano na nchi unayokwenda kuna mahala watu wanakwenda kwa ajili ya misaada ya Kijeshi na Usalama kama Urusi nk
si lazima mtu awe Diplomats na ndio maana siku hizi wakiteuliwa wanakwenda Chuo Cha Diplomasia kupigwa msasa kidogo ndio wanaondoka.
 
Field Marshall ES said:
Seif Idd, alikuwa balozi, Mwambi alikuwa Capatin wa JWTZ, lakini wote waliishia kuweza kuifanya kazi ya unaibu katibu mkuu wa CCM taifa, kazi ambayo kwangu ni kubwa sana kuliko ubalozi wa Urusi, sasa nashangaa mtu kama wewe kutoelewa hilo mkuu, kwamba akiwa CCm taifa alikuwa ni mmoja wa watengeneza sera zetu za taifa, kwa hiyo kama ni qualifications zingeulizwa huku, lakini sio sasa wakati tayari amesha-function kwenye CCM taifa, kwa kweli ni weak argument, hasa ukielewa kuwa kina Liundi walienda kuwa mabalozi kwa kukimbiza mwenge tu, under Mwalimu.

Mwambi, from Captain wa JWTZ, mpaka kuwa naibu katibu wa CCM taifa, unasema hawezi kuwa balozi wetu Urusi I am lost?

Field Marshall ES,

..Tunachozungumzia hapa ni majukumu ya Mabalozi. Kwa mtizamo wangu, katika zama hizi za ushindani, majukumu hayo yanapaswa kutekelezwa na wataalamu wa diplomasia na mashirikiano ya kimataifa.

..Jaka Mwambi amekuwa mtumishi wa CCM wa muda mrefu na ndiyo maana akapanda ngazi mpaka kuwa Naibu Katibu. Anakielewa vizuri Chama kuliko masuala ya Diplomasia.

..Majukumu aliyowahi kubeba Jaka Mwambi ni ya kisiasa ndani ya CCM. Hapa tunazungumzia majukumu ya kidiplomasia na mashirikiano ya kimataifa.

..Umezungumzia sera. Tanzania tunayo sera yetu ya Diplomasia na Mashirikiano ya Kimataifa. Walioshiriki katika kutunga sera na muongozo huo ni Wataalamu wetu wa pale Mambo ya Nje. Ushauri wangu ni kwamba hao ndiyo wapewe nafasi wakatekeleze sera na muongozo huo.

..Kwamba Mwalimu aliteua mkimbiza mwenge kuwa balozi, au Mkapa aliteua Mkuu wa JKT ubalozi, haihalalishi Kikwete kufuata mifano hiyo mibaya. Kikwete aliahidi kuendeleza na kuiga mazuri na siyo mabaya ya awamu zilizopita.
 
Mimi naona hii ni kupeana nafasi tu za kula kwa watu wale wale- lini hasa tutawapa nafasi watendaji wengine wasiokuwa katika wigo wa Kamati Kuu ya CCM. Muungwana hana tafauti na hao walipita kabla yake na naona kazidi kufanya madudu.
 
sema wewe maana nikisema mimi watasema oh jamaa ni mpinzani tu kila mara lakini ya kuandika ni haya haya ambayo wao wanasema ni ya upinzani maana Srrikali haina kitu cha ku support.
 
Lunyungu,

..Jaka Mwambi alikuwa Katibu wa Vijana wa TANU wakati Kikwete akiwa Mwenyekiti walipokuwa Tanga School.
 
Lunyungu,

..Jaka Mwambi alikuwa Katibu wa Vijana wa TANU wakati Kikwete akiwa Mwenyekiti walipokuwa Tanga School.

Uwezo was Jaka ni upi na kauonyesha wapi muda wote akiwa Tanzania alikuwa jeshini akakimbilia kwenye chama .Uwezo upi na usalama upi anao utafuta toka Russia ? Usalama ni watuhumiwa wopte wa EPA na BOT kufikishwa mahakamani ndiyo jambo la maana .Mengine yote ni hadithi za kupeana kula hakuna cha umakini wala nini .Mtandao mwendelezo .
 
..Jaka Mwambi amekuwa mtumishi wa CCM wa muda mrefu na ndiyo maana akapanda ngazi mpaka kuwa Naibu Katibu. Anakielewa vizuri Chama kuliko masuala ya Diplomasia.

Mkuu joka,

1. CCM iko hivi:- mwenyekiti, makamu, katibu, naibu katibu, hao watatu wa kwanza wasiokuwepo naibu katibu ndiye anashika utawala, unasema kuwa hana uwezo wa kuwa balozi wetu Urusi?

2. Mkuu joka, katiba yetu iansema wananchi tunamchagua rais, na kumpa power kikatiba kuwachagua wasaidizi wake wa kumsaidia kazi zake, ikiwa ni pamoja na kumuwakilisha nje ya nchi kwa niaba ya taifa letu, leo amemchagua kiongozi anayemuona kuwa anafaaa kumuwakilisha Urusi, kwa niaba ya taifa letu,

Now who are you kum-question rais wetu wa jamhuri's judgement? Je una kifungu chochote cha katiba yetu kinachoweza kukupa a back up mbele ya watu walioenda shule kama hapa JF?

3. Mara ya mwisho kutokea ishu kama hii, ilikuwa Makweta, alikwenda kwa Mkapa akiwa rais na kumuambia kuwa msaidizi wake mmoja wa anayeitwa Kumchaya, hafai, Mkapa akamjibu kuwa kama unayosema ni kweli, basi asiyefaaa ni mimi rais niliyemchagua, guess what umewahi kumsikia tena Makweta kwenye cabinet?

The lesson hapa ni kama huna back-up, kikatiba usiende kumchezea simba sharubu!
 
Nimesoma analysis zote kwa karibu sana kuanzia kwa FMES mpaka kwa Rev, na nimemalizia na Pundamillia.

Tuweke maslahi pembeni. What are the credentials needed to be a leader or diplomat in Tanzania? Kwa Tanzania education doesn't count, sababu PhD ya Balali didn't make him wised decision maker, or experience ya Lowassa and Meghji didn't make them smart leaders neither.

We all suffer from side effect of poor constitution. Utaangalia kila maumivu tunayoyapata yanasababishwa na katiba yetu mbovu. We don't have check and balance ndio maana Mkapa alidiriki kuchagua vimada wake kuwa wabunge and JK pick his home boyz kuwa wawakilishi wa Board of External Trade(BET). Sasa hata kama tutalia kwamba why Balozi hana experience ya diplomasia ni kazi bure, sababu katiba inamruhusu JK kuchagua hata mwanae Ridhiwani akawa mbunge wa kudumu UN.

Katiba mbovu inasababisha Tanzania iendeleee kupumua kwa kutumia machine, sababu leo hata tukichagua upinzani 100% raisi anaweza kuja na kusema anavunja bunge sababu hana convidence nalo. This is side effect ya katiba yenye viraka, katiba inayonuka rushwa, na katiba ilijoaa ubabaishaji wa serikali ya chama kimoja.

Mabolozi wetu wengi ni watalii, wanaongeza mzigo mzito kwa watanzania masikini kabisa kule Mashewa, Mlalo na Bungu. Imagine leo pale Dar kuna shule yenye wanafunzi 150 kwa darasa na madawati 15 per class. While, Balozi wenu pale DC anacheza tuu na ma Duvelle na kunywa expensive wine kila giza linapoingia. Balozi ambaye ameshindwa kukordinate nguvu za watanzania states nzima ili wawe productive kwa nchi yao. I dont know what different does it make if they have PhD or certificate from Forodhani cooking school. They're selfish and wamelaaniwa na Mungu, there is nothing human being can do about. Muda mwingine natamani hata kuchallange PhD zao na experience zao, maana zinadhalilisha watendaji bora wenye the same qualification.

We need Balozi ambae ataweza kutransfer new technology, new economic reform, new ideas kutoka nchi anayo wakilisha, ambazo tukizichanganya na zetu then wananchi wetu wataweza kujipatia matibabu kwa mifuko yao, wataweza kununua mbegu za kisasa kwa kilimo chao, wataweza kuwapeleka watoto wao kwenye public and private schoool kwa pesa zao. That is what we need, and not mabalozi boga ambao ndio walishadadia kuingiza nchi kwenye deal ya RICHMOND.

Hatuitaji mabalozi ambao kwenda kwao ng'ambo ni kujiongezea vimada na kulala late pasipo kuangalia maendeleo ya taifa. One of the embassy which need to feel shame ni UBALOZI WA TANZANIA DC, that is a shame and shame and shame embassy in our life time history.

We need new katiba and that is the only way forward.
 
mkuu FMES,
Umeelezea sana kuhusu huu uteuzi,lakini kuwa memba ambao hupenda kupinga kila kitu, na wanaweza hata kubishana na misahafu. Huwezi kuwabadili misimamo yao... Tuliokuelewa tumefahamu, hao wabishi achana nao vilevile
 
Back
Top Bottom