Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
RAIS Jakaya Kikwete jana alimwapisha mwanasiasa mkongwe nchini, Jaka Mwambi, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.
Kabla ya uteuzi wa Mwambi, Balozi wa Tanzania Urusi alikuwa Patrick Chokala.
Rais Kikwete pia alimwapisha Mohamed Haji Hamza kuwa Balozi, na George Mlawa kuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kutokana na uteuzi huo, Haji Hamza anakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Zanzibar.
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, walikuwa miongoni mwa viongozi wa serikali walioshuhudia viapo hivyo Ikulu, Dar es Salaam.
Mabalozi wapya wameahidi kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kutotoa siri bila idhini ya Rais.
Balozi Mwambi alisema uteuzi huo ni changamoto kubwa kwake, hasa kwa kuzingatia utekelezaji sera ya serikali ya diplomasia ya uchumi. Mwanasiasa huyo aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa katika mikoa kadhaa nchini na mara ya mwisho alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara.
Kamishna Mlawa aliapa kuwa wakati anatekeleza majukumu yake hatatoa siri bila kibali cha tume.
Rais aliwapongeza mabalozi wapya na Kamishna Mlawa kwa uteuzi huo na akamweleza Haji Hamza kuwa awe na imani kuwa ataweza kumudu changamoto mpya zinazomkabili.