Jaji Werema ndiye alifikiri kwa kutumia nywele. Tundu Lissu aliwazidi akili kwa kutumia kanuni

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Tundu Lissu alikuwa sahihi alipoomba kutoa hoja ya kujadili kuhusu meli iliyozama. Kanuni iko wazi:

*************
47.-(1) Baada ya Muda wa Maswali kwisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwa Shughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye Orodha ya Shughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.
(2) Hoja ya namna hiyo itakuwa ni maalumu na inaweza kutolewa wakati wowote hata kama majadiliano yatakuwa yanaendelea.
(3) Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

*************
Ukisoma hapo kwenye RED ni kwamba Tundu Lissu aliwazidi kete wabunge wote kwani inaelekea hawakuwahi kukitumia kipengele hiki cha kusimama na kuomba hoja kama alivyofanya Tundu Lissu.

Hakika hapa Jaji Werema na Job Ndugai ndio aliyefikiri kwa kutumia nywele. Semeni wenyewe.
 
Acha na hao wachumia_tumbo yaani kujipendekeza kwa jk hawana lolote zaidi ya ushabiki tu.
 
Naweza kumsamehe Naibu Spika kwaniinajulikana anatetea chama na hajui vizuri sheria/kanuni anazozisimámia. Sasa kwa huyu AG Werema, nilitegemea aelezee mambo kwa kuegemea sheria /kanuni bila kuleta kauli za kejeli. Namuomba Mh. Rais Kikwetwe auhamishie baraza la kiswahili ili aende akasaidie kutunga Misemo ya kiswahili na nahau.
 
Back
Top Bottom