Jaji Warioba: Vita ya Rushwa haiwagusi/inawakwepa viongozi wa Serikali

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Jaji Joseph Warioba amesema vita dhidi ya rushwa na ufisadi inayoendelea nchini inawagusa wafanyabiashara na watumishi pekee, lakini inawazunguka viongozi.

Jaji Warioba, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Kero ya Rushwa iliyoundwa Januari 17, 1996 na Rais Benjamin Mkapa, alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusu miaka 20 baada ya kifo cha muasisi wake, Julius Nyerere.

Nyerere anaonekana kuwa kioo cha viongozi ambao hawakupenda rushwa na ambaye aliasisi Azimio la Arusha ambalo kwa kiasi kikubwa lilidhibiti viongozi kujiingiza kwenye uovu huo.

Pamoja na msimamo huo wa Nyerere na mikakati yake, Jaji Warioba anasema rushwa ilikuwepo, lakini anaona Serikali ya sasa imejikita kupambana nayo ila imesahau viongozi.

“Kwa upande wa rushwa kama kuna kitu kinanifanya nishabikie Serikali hii ni kupiga vita rushwa, ufisadi, kurudisha uadilifu, kurudisha nidhamu na kulinda rasilimali za Taifa,” alisema Jaji warioba ambaye alikuwa Waziri Mkuu kati ya mwaka 1985 na 1990.

“Sasa naona jitihada zinazofanywa za kupiga vita rushwa na ufisadi. Ni jitihada nzuri, lakini bado hazitoshi.

“Haya mambo huwezi kuondoa nafasi ya uongozi kama unapambana na rushwa. Na mpaka sasa, hii vita inaonekana inapita pembeni, ina deal (inashughulika) na wafanyabiashara na watumishi wa umma. Inaonekana kama viongozi hawahusiki ni wasafi, mimi siamini.

“Huwezi kuwa na nchi ambayo kuna rushwa na ufisadi, lakini viongozi wake wote ni wasafi na itafika mahali kama kweli tuko serious (makini) tuone tunapambana na rushwa na ufisadi ndani ya uongozi.”

Tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani imejikita katika kupambana na ufisadi, wakwepa kodi, watakatishaji fedha na wahujumu uchumi.

Vita hiyo imekumba watumishi waandamizi wa serikali na wafanyabiashara, huku viongozi wakiadhibiwa kwa kutumbuliwa au kutakiwa kujiuzulu pale panapoonekana udhaifu katika majukumu yao.

Lakini Jaji warioba anaona bado vita hiyo haijashika vizuri.

“Kenya inatoa dalili nzuri kwamba hata wakubwa wanashughulikiwa,” alisema Jaji Warioba.

“Sasa hapa bado. Katika mfumo wetu wa siasa na hasa za uchaguzi kuna rushwa nyingi tu.”

Chanzo: Mwananchi
 
Kama Makonda yeye hiyo taasisi ya PCCCB ni toothless bulldog.
Haimuhusu wala haiko kwenye hadhi yake kabisa. Maana anayofanya waziwazi ingekuwa mwingine tumeshamsahau kabisa.
Ila kwa vile yeye ni mtoto mpendwa labda asubiri mfalme atakapo achia ufalme kwa hiari au kwa nguvu ndio atakapo shukiwa kama mwewe.
JINAI HAINA EXPIRED DATE
 
Rushwa kwa viongozi ilikwamisha hata KATIBA.
 
Attachments

  • IMG-20141102-WA0010.jpg
    IMG-20141102-WA0010.jpg
    56.6 KB · Views: 1
  • Screenshot_20191002-115937.png
    Screenshot_20191002-115937.png
    112.4 KB · Views: 1
Mh.Ex-PM Judge Joseph Sinde Warioba,I known you for yourworks and deeds back then. But, the Tume ya Mabadiliko ya Katiba which you chaired is the recent. It was been a big up from the begging,however it went into usual waste bin of unknown at the expense of our tax money.
I always ask myself of what has become of we Tanzanians.
Don't we have anything to do to rescue the whole situation?
 
Because of
 
Attachments

  • IMG-20141102-WA0010.jpg
    IMG-20141102-WA0010.jpg
    56.6 KB · Views: 1
Mh.Ex-PM Judge Joseph Sinde Warioba,I known you for yourworks and deeds back then. But, the Tume ya Mabadiliko ya Katiba which you chaired is the recent. It was been a big up from the begging,however it went into usual waste bin of unknown at the expense of our tax money.
I always ask myself of what has become of we Tanzanians.
Don't we have anything to do to rescue the whole situation?
Tafadhali nisaidie kutafsiri hii kitu hapa!
 
Mh.Ex-PM Judge Joseph Sinde Warioba,I known you for yourworks and deeds back then. But, the Tume ya Mabadiliko ya Katiba which you chaired is the recent. It was been a big up from the begging,however it went into usual waste bin of unknown at the expense of our tax money.
I always ask myself of what has become of we Tanzanians.
Don't we have anything to do to rescue the whole situation?

Umeandika broken ya aina yake.. Vyeti vyako lazima vikaguliwe upya aiseee.
 
Back
Top Bottom