Jaji Warioba: Vita ya Rushwa haiwagusi/inawakwepa viongozi wa Serikali

my PM umeongea ukweli ILA UMEKUWA MNAFIKI MNO,wewe kama hili umeliona umechukua hatua gani au kama mwenye njaa yeyote ni kukimbilia kwenye press na kujifanya shujaa,ngoja tujikumbushe umeacha legancy gani nyuma yako baada ya kuitumikia nchi hii kama PM?NA UTEUZI WAKO WA UJAJI ulikuwa within kisheria ?je mapendekezo yake ya katiba mpya yaliishia wapi?
 
Hujui alipoishia?
 
Huyu mzee kasema kweli, hiyo vita inalenga wafanyabiashara na kama ni wanasiasa, basi ni wa upinzani. Kimsingi ni vita ya rushwa ya kukomoana.

Hakuna Siku umewahi kuwa ' Neutral ' hasa katika ujengaji wako wa Hoja na unachokijua Wewe ni kuonyesha tu Chuki zako zilizopitiliza kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano, Rais Dkt. Magufuli na Chama cha Mapinduzi. Badilika Ndugu kwani wapo hata Wapinzani ( wana CHADEMA ) Wenzako tupo nao Mitaani japo huwa ' wanakosoa ' kama Wewe ila kuna mengine mazuri ya Serikali hii huwa wanayapongeza. Mbona Mimi ni Shabiki mkubwa tu wa CCM ila kuna muda huwa nawapongezeni Wapinzani ( hasa CHADEMA ) na kuna muda vile vile huwa nakisema Chama changu cha CCM yote ikiwa tu ni sehemu yangu ya kuleta Afya ya Kidemokrasia ndani ya Tanzania yetu.
 
Hili lipo wazi kabisa. Ruge's deal la more than 300billions liligusa top people kwenye serikali. Na hiki ndicho kinampa Ruge jeuri ya kugoma kukiri kama wengine.
Namwombea Luge sana na ngome hivyohivyo huwezi toa bank kuu billion 305 bila viongozi wa juu kuhusika hata rais kujua,na katika hizo yeye alichukua shear zake na akalipa ushuru wakapokea bila kuuliza imetokea wapi au kujali ni ya unga wizi au source ni nini?wakati Kenya matumizi yao.Leo wanaleta fyoko wanafanya montego ya kuchukua zote.viongozi walio idhinisha hawapo hawaguswi.
 
Hakuna Siku umewahi kuwa ' Neutral ' hasa katika ujengaji wako wa Hoja na unachokijua Wewe ni kuonyesha tu Chuki zako zilizopitiliza kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano, Rais Dkt. Magufuli na Chama cha Mapinduzi. Badilika Ndugu kwani wapo hata Wapinzani ( wana CHADEMA ) Wenzako tupo nao Mitaani japo huwa ' wanakosoa ' kama Wewe ila kuna mengine mazuri ya Serikali hii huwa wanayapongeza. Mbona Mimi ni Shabiki mkubwa tu wa CCM ila kuna muda huwa nawapongezeni Wapinzani ( hasa CHADEMA ) na kuna muda vile vile huwa nakisema Chama changu cha CCM yote ikiwa tu ni sehemu yangu ya kuleta Afya ya Kidemokrasia ndani ya Tanzania yetu.

Kwanza nashukuru kwa ushauri mujarabu, sina sababu ya kusifia maana wanaomsifia ni wengi sana, wengine wanasifia kikwelikweli, wengine wanasifia ili wapate chochote, wengine wanasifia kwa ajili ya hofu na wengine wanasifia kama bendera fuata upepo, hao wote hujatosheka nao unataka na mimi nisifie? Sio kwamba sioni mazuri machache, bali hayo mazuri machache kwangu ni wajibu wao,hivyo kusifia ni hisani isiyodaiwa, hayo mabaya ndio nimejikita kuyasema ili yasiwepo na hali iwe bora zaidi. Kwa ww kuwasifia cdm au kuwakosoa huo ni uamuzi wako, sina popote ninapotaka ww uwasifie au ninaposhinikiza cdm isifiwe ili kubalance na ukosoaji.
 
Mzee amenena. Mungu ambariki. Ikitokea vita ya rushwa ikaingia kwa viongozi serikalini, wengi wataikimbia nchi hii pamoja na majigambo yao ya sasa
Na kuna mmoja habari zake zitakapo wekwa hadharani watasahau kuwa alikuwa anaonekana malaika na mlezi wa wanyonge. Subiri tuu muda utafika, hata kama anatengeneza mazingira eti asiondoke, thubutu!
 
Attachments

  • IMG-20141102-WA0010.jpg
    IMG-20141102-WA0010.jpg
    56.6 KB · Views: 1
  • IMG-20141102-WA0010.jpg
    IMG-20141102-WA0010.jpg
    56.6 KB · Views: 1
Rushwa haitaisha kamwe kama viongozi hawatamulikwa Mali za kufuru wanazozipata kwa muda mfupi huku maskini wakizidi kukamuliwa kwa kodi.

Ni lazima Mali zote zijulikane ni za nani na yuko wapi na amezipata wapi na ni nani waliokua wanamhonga mtumishi huyo au kiongozi huyo.

Najua kwa dhati kabisa Mkuu wa nchi ana nia ya dhati na anatamani Tanzania liwe taifa lenye watu wenye maadili mema .
Lakini Maadili mema ni Lazima yaanzie kwa Viongozi wa Chama na serikali.
Maadilimema ni lazima yawe yanatimizwa na watu wenye hofu ya kutenda uovu. Watu wanaochukizwa na kila uovu ikiwemo Wizi wa Kura, Rushwa kwenye Chaguzi, Upendeleo wakati wa uchaguzi n.k.

Kiongozi anayesaidia kuiba kura za umma hawezi kuacha kuiba fedha za umma .
Nini kinamsababisha Kiongozi aibe kura au abadilishe matokeo ya MTU "A" ili ampe MTU "B" kama sio kukosa uadilifu na kujiwekea mazingira ya kujenga himaya na kundi la wala Rushwa wasio na MTU wa kuwapinga au wasiyempenda ?
Nchi ni Mali ya wote lakini kuna kundi LA wala Rushwa na wabadhirifu au wachotaji wa fedha na Mali za umma limeamua kujinufaisha kupitia Chama na serilkali.
Ndio mana unaona Chama kikikongwe Miaka mitano sasa muda wote ni mikutano na makongamano na mavitenge na maskafu yao shingoni.Hao hawaoni shida za watanzania wote zaidi ya wao kula bata huku wananchi wakibanwa kwa kodi za kujiletea maendeleo.

Mh. Rais angeanza kuwabana kabisa hao viongozi kwa kuunda tume ya kuchunguza Mali zao.
Waangalie Kila idara.
Ni aibu sana kwa watanzania kuwa na kundi LA watu wa chache wenye kumiliki 80 % za Mali zote zinazoonekana lakini wakiwa wamejificha kwenye uongozi na madaraka ndani ya chama na serikali Huku wananchi wanyonge wakibaki kuwa 80%!

Ni lazima tukubali kuwa nchi hii imetafunwa vya kutosha na viongozi wa chama na serikali .
Sasa tuamue moja tuendelee kuwapigia makofi wezi na wengine wanakimbilia kujificha kwenye makanisa na misikiti kama walivyofanya Wakati wa Kuelekea uchaguzi wa 2015.
Leo wameanza tena kukimbilia kwenye nyumba za ibada.

Sheria ya maadili ya uongozi wa umma ingefanyiwa marekebisho kabla ya sheria ya uhujumu uchumi mana bila kuwa na Viongozi wanaohujumu uchumi huwezi kuwa na wahujumu uchumi.

Wahujumu uchumi dunia nzima wanapata nafasi ya kukwapua kwa kushirikiana na viongozi. Hawa ni kuanzia wakuu wa idara zote na vyombo vyote .
Kila idara INA wapiga dili bila kujali.
Wakuu wote wa Idara zote na taasisi zote na vyombo vyote waliostaafu na waliopo ni mabilionea.Wana Mali zisizohesabaika. Wanaoingia wanajua utajiri wa wale wanaotoka ndio mana na wao wanafanya Kila mbinu ili waibe kwa kutumia ofisi za umma.
Hawa ndio wanaomshauri mkuu wa nchi kuwa Chama kibaki peke yake.
Siku zote wapinzani wakiwepo ndio wanaomulika wizi wa Viongozi wa umma.

Kwa sasa wanaowekwa magerezani ni wale waliokua wametumika tu kukamilisha ukwapuzi wa fedha.
Wahusika wakuu ni wale waliokua wamekaa kimya fedha za umma zikaliwa.
Watu walikaa kimya miradi ya hovyo ikafanywa .
Watu walikaa kimya mikataba ya hovyo ikaingiwa.
Wahusika wakuu wamekaa kimya kabisa na wanaendelea kutafuna hela zao walizowatumia wale ambao Leo wanaitwa wahujumu uchumi.

Mfano Sakata LA Escrow lilihusisha watu wengine sana waliokua kwenye ofisi za umma na uongozi lakini walikamatwa na kukaa gerezani ni wachache. Kuna kakundi kadogo kanakojificha kwenye uongozi ndani ya vyama na serikali huku kakiendelea kujilimbijizia Mali.
Siku hizi ni kawaida kabisa kuona MTU anakaa kwenye uongozi kwa miaka mitatu anakua bilionea bila kujali kabisa kuwa kuna sheria Kali ya uhujumu uchumi.

Kila mtu awajibike kulinda maadili na haki katika Taifa letu. Wachunguzaji ,wakamataji, wafokaji, watoa adhabu n.k nao wachunguzwe sana. Kila MTU awekewe mchunguzaji. Hata anayechunguza mana nao wanatumia mwanya wa sheria Kali kukwapua mijihela kwa wale wanaohujumu nchi yetu.
 
Kwanza nashukuru kwa ushauri mujarabu, sina sababu ya kusifia maana wanaomsifia ni wengi sana, wengine wanasifia kikwelikweli, wengine wanasifia ili wapate chochote, wengine wanasifia kwa ajili ya hofu na wengine wanasifia kama bendera fuata upepo, hao wote hujatosheka nao unataka na mimi nisifie? Sio kwamba sioni mazuri machache, bali hayo mazuri machache kwangu ni wajibu wao,hivyo kusifia ni hisani isiyodaiwa, hayo mabaya ndio nimejikita kuyasema ili yasiwepo na hali iwe bora zaidi. Kwa ww kuwasifia cdm au kuwakosoa huo ni uamuzi wako, sina popote ninapotaka ww uwasifie au ninaposhinikiza cdm isifiwe ili kubalance na ukosoaji.
Always on point. Big up
 
Huo in ukweli mchungu, tumeshuhudia kina ngeleja, tibaijuka na wenzao wanarudisha pesa walizokwiba mchana kweupe wala hawakamatwi na kuhojiwa na takukuru kamwe.pia makamba kakwiba zaidi ya bilioni Na kipande anatamba tu mtaani.kiukweli vita ya kupambana na rushwa ina macho.
 
Back
Top Bottom