Jaji Warioba: Viongozi wa siasa bila kujali itikadi zao, wakae pamoja na kutafakari namna ya kulinda amani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,639
2,000
Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewapongeza viongozi wa dini nchini kwa jitihada zao za kudumisha amani na haki nchini na kuwataka viongozi wa siasa bila kujali itikadi za vyama vyao kukaa pamoja na kutafakari namna ya kulinda amani ya nchi.

Aidha Jaji Warioba alisema yapo mambo yanayohitaji kuzingatiwa ili kudumisha hali ya amani.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jana, Jaji Warioba ambaye alishawahi kuwa Waziri Mkuu nchini alisema ipo haja ya kujiuliza masuala yanayowezesha amani.

“Amani ni tunda la haki, penye haki kuna amani lakini bila amani huwezi kuwa na haki za binadamu,” alisema Jaji Warioba na kuongeza kuwa vurugu zinazoleta uvunjifu wa amani zinatokana na shughuli za siasa, jambo ambalo ni changamoto kubwa.

Alisema vyama vya siasa vinatakiwa kufanya tathmini inavyopata wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi kwa kuwa ni eneo ambalo linahitaji kufanyiwa maboresho ili haki itendeke na hivyo amani iendelee kutawala.

Alisema kazi ya kuhubiri amani ingepewa viongozi wa siasa kama inavyofanywa na viongozi wa dini nchini, jambo litakalosaidia kuimarisha amani na haki za binadamu kwa kuwa matatizo mengi yanatokana na shughuli za siasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga alisema katika kuadhimisha siku hiyo wanaendelea kuhamaisha wananchi kupambana na matukio ya ukatili dhidi ya watoto hususani ukatili wa kingono unaosababisha pia ukatili wa kisaikolojia, mimba na ndoa za utotoni.
 
mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,514
2,000
Nchi za kijamaa na haki za binadam wapi na wapi, me naona kwa rank Tz tupo vizur...
1. China
2. Russia
3. Cuba
4. N Korea
Balaa tupu
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
9,878
2,000
Nchi za kijamaa na haki za binadam wapi na wapi, me naona kwa rank Tz tupo vizur...
1.China
2.Russia
3.Cuba
4. N Korea
Balaa tupu
Sasa mbona Magufuli kila anapokwenda anakuwa na ulinzi mkubwa sana kama wa Bush alipoenda Iraq.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
106,788
2,000
Waungwana mkipata nafasi na kama mna bundle la kutosha msikilizeni Warioba clip iko hapo juu kwani ameongea mambo ya msingi sana kuhusu muelekeo wa Nchi yetu na mambo mazito. Tatizo ndani ya maccm hakuna atakayemuunga mkono kwa kumuhofia huyo anayejiita mwendawazimu. Yaani Warioba kapiga madongo mazito sana kuhusu haki za binadamu Nchini na huu uchaguzi FAKE wa October 28, 2020.

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,873

Huyu jamaa atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,627
2,000
Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewapongeza viongozi wa dini nchini kwa jitihada zao za kudumisha amani na haki nchini na kuwataka viongozi wa siasa bila kujali itikadi za vyama vyao kukaa pamoja na kutafakari namna ya kulinda amani ya nchi.

Aidha Jaji Warioba alisema yapo mambo yanayohitaji kuzingatiwa ili kudumisha hali ya amani.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jana, Jaji Warioba ambaye alishawahi kuwa Waziri Mkuu nchini alisema ipo haja ya kujiuliza masuala yanayowezesha amani.

“Amani ni tunda la haki, penye haki kuna amani lakini bila amani huwezi kuwa na haki za binadamu,” alisema Jaji Warioba na kuongeza kuwa vurugu zinazoleta uvunjifu wa amani zinatokana na shughuli za siasa, jambo ambalo ni changamoto kubwa.

Alisema vyama vya siasa vinatakiwa kufanya tathmini inavyopata wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi kwa kuwa ni eneo ambalo linahitaji kufanyiwa maboresho ili haki itendeke na hivyo amani iendelee kutawala.

Alisema kazi ya kuhubiri amani ingepewa viongozi wa siasa kama inavyofanywa na viongozi wa dini nchini, jambo litakalosaidia kuimarisha amani na haki za binadamu kwa kuwa matatizo mengi yanatokana na shughuli za siasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga alisema katika kuadhimisha siku hiyo wanaendelea kuhamaisha wananchi kupambana na matukio ya ukatili dhidi ya watoto hususani ukatili wa kingono unaosababisha pia ukatili wa kisaikolojia, mimba na ndoa za utotoni.
Tatizo tulilonalo kwa sasa ni kuamini kwamba usalama na amani ni kazi ya vyombo vya dola pekee, kana kwamba raia hawahusiki!!! Tukumbuke tu bila raia hakuna ufanisi kwa vyombo hivyo na bila vyombo hivyo hakuna amani wala utulivu.
TUKIYAWAZA MABAVU TUANGALIE YALIKOTUMIKA KAMA WALIFANIKIWA!!!
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,744
2,000
Hahaha muongo sana huyu babu, wakati yanatokea alikuwepo sasa anajidai kuongea as if naye hakuwepo humu.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
106,788
2,000
Na wanawe akina Kippi wasahau teuzi. Kanifurahisha sana kwa kusema ukweli naona hata waliohudhuria waliguswa na ukweli wake kuhusu hali ya haki za binadamu Nchini. Natamani kungekuwa na wastaafu wengi wenye UTHUBUTU kama yeye.
Huyu jamaa atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Bupa2009

Member
Sep 15, 2020
61
125
Daaah😭😭😭. Siyo nalia kwa kupoteza MB zangu, no! Nalia kwa kuona kuwa babu huyu ambaye hana cha kupoteza kaamua kusimama kwenye UKWELI. UKWELI ambao haina shaka yoyote. Ukweli ambao sioni kama wenye mamlaka waweza kuufuata.

UKWELI ambao kama wenye mamlaka wataamua kuufuata basi itakuwa DAWA ya kuliponya TAIFA

Siyo uponyaji ule wa kinafiki wa akina ZITTO na Maalim Seif kule visiwani ulioegemea zaidi katika maslahi binafsi kuliko maslahi ya nchi.

Mzee Warioba, baba 😭😭😭, maneno yako yataishi milele, kiukweli watu wa Mara ninaamini ukiachilia mbali akina Mwita Waitara etc ni wakweli na wawazi

Hapana mashaka hata kidogo KATIBA haifuatwi, na sisi wananchi wala hatubaguani bali viongozi wa kisiasa ndiyo wanaopandikiza UBAGUZI kwa wafuasi wao.

Bila shaka, hawa viongozi hawana nia njema nasi, na ndiyo maana wamekuwa wakihubiri AMANI badala ya HAKI

Wanahubiri AMANI huku wanaua, wanatesa watu, wanawaweka watu mahabusu, wanapiga watu

Imekuwa rahisi sasa kumkosoa m/mungu kuliko viongozi wa sasa, wanataka tusifu tu.

Viongozi wote wa serikali za mitaa waliopatikana katika UCHAGUZI wa 2019 wapo katika wakati mgumu kuongoza maeneo yao, ni ukweli usiofichika kwamba wanakataliwa na wananchi

Kiukweli, baba😭😭😭, RASIMU yako ndiyo ilikuwa na itakuwa muarobaini wa haya yote yanayoendelea katika Taifa letu.

M/mungu akulinde mzee, akupe afya njema ya mwili na AKILI kwa ujumla

Binafsi nimekuelewa saaaana mzee wangu, KWELI wew ni KIONGOZI.

Unaonyesha njia, watapotea tu watu wa kuifuata njia ila mimi naifuata babaa 😭😭😭
 
  • Love
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
106,788
2,000
Nimeshangaa kwa kweli kwa ujasiri aliouonyesha na hawa wasikilizaji wameguswa sana na ukweli wake na sidhani kama walitegemea angetiririka kiasi hicho. Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu na afya njema. Natamani sana kungekuwa na wastaafu wenye ujasiri kama Warioba lakini wote wameufyata wanamuogopa huyo anayejiita MWENDAWAZIMU.

Yaani watu wamekuwa wapole saaaaaana wakisikiliza madini kutoka kwa baba huyu. Kwa kweli ana nafasi yake PEPONI

UKWELI HAUKOSEWI, INAPOBIDI LAZIMA USEMWE.
Baba huyu kaamua kuusema. Wala siyo mnafiki kaonyesha hisia zake juu ya mambo yanavokwenda na kutoa suluhisho.
 
  • Love
Reactions: BAK

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,873
2,000
Daaah. Siyo nalia kwa kupoteza MB zangu, no! Nalia kwa kuona kuwa babu huyu ambaye hana cha kupoteza kaamua kusimama kwenye UKWELI. UKWELI ambao haina shaka yoyote. Ukweli ambao sioni kama wenye mamlaka waweza kuufuata.

UKWELI ambao kama wenye mamlaka wataamua kuufuata basi itakuwa DAWA ya kuliponya TAIFA

Siyo uponyaji ule wa kinafiki wa akina ZITTO na Maalim Seif kule visiwani ulioegemea zaidi katika maslahi binafsi kuliko maslahi ya nchi.

Mzee Warioba, baba , maneno yako yataishi milele, kiukweli watu wa Mara ninaamini ukiachilia mbali akina Mwita Waitara etc ni wakweli na wawazi

Hapana mashaka hata kidogo KATIBA haifuatwi, na sisi wananchi wala hatubaguani bali viongozi wa kisiasa ndiyo wanaopandikiza UBAGUZI kwa wafuasi wao.

Bila shaka, hawa viongozi hawana nia njema nasi, na ndiyo maana wamekuwa wakihubiri AMANI badala ya HAKI

Wanahubiri AMANI huku wanaua, wanatesa watu, wanawaweka watu mahabusu, wanapiga watu

Imekuwa rahisi sasa kumkosoa m/mungu kuliko viongozi wa sasa, wanataka tusifu tu.

Viongozi wote wa serikali za mitaa waliopatikana katika UCHAGUZI wa 2019 wapo katika wakati mgumu kuongoza maeneo yao, ni ukweli usiofichika kwamba wanakataliwa na wananchi

Kiukweli, baba, RASIMU yako ndiyo ilikuwa na itakuwa muarobaini wa haya yote yanayoendelea katika Taifa letu.

M/mungu akulinde mzee, akupe afya njema ya mwili na AKILI kwa ujumla

Binafsi nimekuelewa saaaana mzee wangu, KWELI wew ni KIONGOZI.

Unaonyesha njia, watapotea tu watu wa kuifuata njia ila mimi naifuata babaa
Ngoja na mimi nimsikilize
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom