Jaji warioba: Tumejipanga kuwa na katiba mpya 2014 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji warioba: Tumejipanga kuwa na katiba mpya 2014

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Sep 4, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [​IMG]Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba (kushoto) akiongea na Mawaziri wa Katiba na Sheria kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Mathias Chikawe (kulia) na Abubakar Khamis Bakari (kulia kwa Jaji Warioba) nje ya ofisi za Tume mara baada ya Mawaziri kutembelea ofisi za Tume leo (Jumatatu, Sept. 3, 2012). Katikati ni Naibu wa Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki na wengine ni watendaji kutoka Tume na Wizara za Katiba na Sheria (Picha na Tume ya Katiba).Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema imejipanga kukamilisha majukumu ndani ya muda uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 na hivyo nchi kuwa na Katiba Mpya ifikapo mwezi Aprili, 2014.

  Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewaeleza Mawaziri wa Katiba na Sheria kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa pamoja na changamoto zilizopo, dhamira hiyo ya Tume ipo palepale.
   
Loading...