5523
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 1,696
- 1,591
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.
Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.
Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.
Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015.
Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.
Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu, alisema.
Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.
Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?
Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo... Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?
Waliopata mgawo
Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.