Ukweli husemwa:
Sija bahatika kuyasoma hayo majibizano na tofauti ya mitizamo yao kwenye gazeti, lakini kwa yale uliyoyaandika na maoni yako, inaonekana hujamtendea haki Jaji Warioba.
Tatizo letu Watanzania, pale tunapomuona mtu anasema mambo mengi tunayoafikiana nayo kimaslahi au kiitikadi, basi hata yale mengine atakayoyasema ambayo ni pumba tunayaona ni mchele. Tumejengeka tabia ambayo pale tunapomwamini mtu fulani, basi tunakuwa kama vipofu wa fikra kwa kile akifanyacho.
Tunatakiwa tujenge tabia ya kujongea kila jambo kwa walakini ili tuweze kubainisha kwa undani sababu zilizoko nyuma ya kila jambo kabla ya kulikubali.
Kama Jaji Warioba alivyosema, 'Utawapata wapi watu ( wajumbe wa Bunge la Katiba) ambao hawana maslahi na suala zito kama katiba ya nchi'.
Pro Shivji anasema haya kwa vile labda ana motive behind lakini vilevile kauli zake nyingi zinaonyesha kama anajaribu kuidhalau tume ya katiba.
Kumbuka wabunge ni wawakilishi wa wananchi ambao wanachaguliwa na wavua samaki, wakulima na wafanyakazi. Kwa mantiki na mchanganuo huo, lazima tu watakuwa ni wengi.
Tatizo kubwa ambalo Watanzania linatusumbua katika mchakato mzima wa katiba ni kutanguliza maslahi ya kiitikadi kwanza badala ya uzalendo.
Hatutaki kujifunza kutokana na makosa mengi ambayo tumechangia kuifikisha nchi hapa ilipo.
Hebu tujaribu kuwa wazalendo kwa hili.
ni vizuri pia prof shivji angeainisha hizo hela za kufanya uchaguzi wa nchi nzima zingetoka wapi. sio kuongea tu.let we be realisticWakuu,
Nimesoma mabishano au tofauti ya mtizamo kati ya prof Issa Shivji na Jaji warioba ktk gazeti la Raia mwema la leo. Nimeshangazwa na msimamo wa Jaji Warioba ninayemheshimu sana, nitaeleza.
Kwa mujibu gazeti la Raia mwema la Leo wasomi hawa wawili wetofautiana juu ya wajumbe wa Bunge la Katiba.
Msimamo Shivji;
Akiwa katka Kongamano la Katiba Prof Shivji alisema;
Kuna kasoro kubwa ktk sheria ya kuendesha mchakato wa katiba mpya, hasa kuhusu uundaji muundo wa Bunge la katiba. Chombo muhimu sana kuliko hata Refrendum ( kura ya maoni) ni Bunge la katiba. Linapaswa kuwa Bunge la wananchi, vinginevyo uhalali wa hiyo Bunge utakuwa na Shaka. Ni Busara kwa wajumbe wa Bunge la Katiba kuchaguliwa moja kwa moja wa Wananchi kwa ajili ya kazi hiyo maalum tu.
Msimamo wa Jaji Warioba.
Hata hivyo, akizungumzia hilo Mkiti wa Tume ya Mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba alimweleza mwandishi wetu akihoji; Utawapata wapi watu ( wajumbe wa Bunge la Katiba) ambao hawana maslahi na suala zito kama katiba ya nchi? Aliendelea ingawa jambo hilo siyo sehemu ya hadidu rejea kwa tume hiyo lakini ni suala la kidemokrasia pia kuwaingiza wabunge na wawakilishi kuwa sehemu ya Bunge la Katiba. Wabunge ni wawakilishi wa wananchi ni watu waliokabidhiwa pia jukumu la kutunga sheria.
Alipoulizwa kuhusu wingi wa wabunge wa ccm ktk bunge hilo na kwamba watalinda maslahi ya chama chao alijibu, wabunge hao wametokana na mfumo wa demokrasia yetu na ndio mtazamo wa wananchi.
My take;
Hivi jaji Warioba hajui kuwa tunacholalamikia ni wingi wa kundi moja - wabunge, ambao nao wana maslahi lakini hatutaki wao wawe wengi huku makundi mengine ya wavua samaki, wakulima na wafanya kazi wakikosa fursa hiyo?
2. Anaposema uwepo wabunge wengi wa ccm ni mtazamo wa wananchi, hajui kuwa moja ya sababu za kutungwa katiba mpya ni udhaifu wa Tume ya uchaguzi kutuletea viongozi wasiochaguliwa wakiwepo hao wa ccm wanaotuhumiwa kuchakachua kura wakisaidiwa na Tume.
NB, Nadhani jaji wangu ninayemheshimu ameteleza ktk hili kama hajavutwa na ushabiki wa kichama zaidi.
Sidhani kama ni sahihi sana kwa Jaji Warioba kudai kwamba composition ya bunge tulilo nalo sasa ambalo wabunge wengi ni wa ccm ndio mtazamo ama matakwa ya wananchi kwa sasa.
Sababu mojawapo ya kushinikiza uwepo wa katiba mpya ni pamoja na mapungufu makubwa yaliyopo katika katiba ya sasa ambayo kwa namna moja ama nyingine imepelekea wakati mwingine tume ya taifa ya uchaguzi kumtangaza mshindi ambaye si chaguo la wananchi. Tunayo mifano ya baadhi ya wabunge ambao hadi leo hii hawathubutu kukanyaga majimboni mwao, na kama wakienda wanafanya hivyo wakiwa na escort ya polisi, wengine wanakwenda kwa kificho na hawajawahi kufanya japo mkutano wa hadhara mmoja tangu watangazwe kuwa washindi.
Na kwa vyovyote vile uwingi wa wabunge wa ccm katika bunge la katiba ni wazi kwamba tutakwenda kuletewa katiba ya ccm na si katiba ya wananchi kama tulivyotarajia. Kwahiyo ni muhimu katika hali hiyo wananchi wenyewe tupewe nafasi/mamlaka ya kuchagua wabunge/wawakilishi wetu katika bunge la katiba. Inawezekana kabisa kumpigia kura (kumchagua) mbunge mwaka 201o lakini miaka miwili baadae yaani 2012 tunagundua kwamba hajakidhi matarajio yetu, hawakilishi matakwa yetu na tungekuwa na nafasi bila shaka tungeweza kumuweka pembeni kwahiyo hoja ya Jaji Warioba inakuwa haina mashiko sana.
Nakubaliana na hoja ya Jaji Warioba kwamba mojawapo ya kazi ya wabunge ni kutunga sheria lakini ni muhimu azingatie kwamba hii ni sheria ya kipekee, hii ni sheria mama, hii ndio nguzo/ mhimili wa sheria nyingine, na ndio maana haitungwi hovyo hovyo, ina utaratibu wake maalum na tofauti, na ndio sababu ikaundiwa tume maalum anayoingoza yeye kwa ajili ya kukusanya maoni ya wananchi kitu ambacho ni tofauti na utaratibu wa utungaji wa sheria nyingine.
Katika hili ninakubaliana moja kwa moja na mawazo ya Prof.Shivji kwamba wananchi wenyewe ndio wanatakiwa kuchagua wawkilishi wao kwa ajili ya bunge hili maalum la katiba. Jaji Warioba katika hili inabidi aachane kabisa na mambo ya kuweka uccm katika jambo hili muhimu kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu kwani katiba nzuri na inayotokana na matakwa ya wananchi wenyewe ndiyo itakayotuletea demokrasia pana na ya ukweli, lakini pia ndiyo itachagiza maendeleo ya nchi yetu kwa miaka mingine 100 au hata 200 ijayo.
Mkuu,
Hujawa wazi, kwa kifupi kati ya hao wawili kwenye hoja hii wewe unakubaliana na nani na kwanini? Baada ya hapo mimi nitakuwa kwenye nafasi nzuri kujibu hoja yako. Na tubase kwenye hoja hii tu.
Hapa tuko pamoja, ila kuwa out of control pia inatokana na sisi watz wasomi na wasio wasomi kutojiamini na kuwapapatikia watu wenye majina makubwa. No wonder kila mtu anataka kuwa kigogo ili aheshimiwe - small God. Hata hivyo, with time na hizi shule zetu za kata mambo yataboreka.
Ukweli husemwa:
Sija bahatika kuyasoma hayo majibizano na tofauti ya mitizamo yao kwenye gazeti, lakini kwa yale uliyoyaandika na maoni yako, inaonekana hujamtendea haki Jaji Warioba.
Tatizo letu Watanzania, pale tunapomuona mtu anasema mambo mengi tunayoafikiana nayo kimaslahi au kiitikadi, basi hata yale mengine atakayoyasema ambayo ni pumba tunayaona ni mchele. Tumejengeka tabia ambayo pale tunapomwamini mtu fulani, basi tunakuwa kama vipofu wa fikra kwa kile akifanyacho.
Tunatakiwa tujenge tabia ya kujongea kila jambo kwa walakini ili tuweze kubainisha kwa undani sababu zilizoko nyuma ya kila jambo kabla ya kulikubali.
Kama Jaji Warioba alivyosema, 'Utawapata wapi watu ( wajumbe wa Bunge la Katiba) ambao hawana maslahi na suala zito kama katiba ya nchi'.
Pro Shivji anasema haya kwa vile labda ana motive behind lakini vilevile kauli zake nyingi zinaonyesha kama anajaribu kuidhalau tume ya katiba.
Kumbuka wabunge ni wawakilishi wa wananchi ambao wanachaguliwa na wavua samaki, wakulima na wafanyakazi. Kwa mantiki na mchanganuo huo, lazima tu watakuwa ni wengi.
Tatizo kubwa ambalo Watanzania linatusumbua katika mchakato mzima wa katiba ni kutanguliza maslahi ya kiitikadi kwanza badala ya uzalendo.
Hatutaki kujifunza kutokana na makosa mengi ambayo tumechangia kuifikisha nchi hapa ilipo.
Hebu tujaribu kuwa wazalendo kwa hili.
Prof ana enjoy stardom bado, anachosema km hakipingwi vile.Jinsi mnavyofunguka mtamfanya Prof na wengine kabla ya kuongea basi wawe wanatazama parameters nyingi zaidi.Si hii tabia ya kufikiria huku wanaongea,wakikosea nasi tukosee nao wakirudi nyuma nasi turudi nao.Lazima tujiwekee viwango vya kufikia kabla ya kupeleka kitu katika jamii pana kw alengo la kutaka wafuate hivyo.Likiwa na makosa mambo yaliyopo at stake ni makubwa na hayarekebishiki.ni vizuri pia prof shivji angeainisha hizo hela za kufanya uchaguzi wa nchi nzima zingetoka wapi. sio kuongea tu.let we be realistic
Sioni ubaya wa scholars kutofautiana, na mijadala kama hii ndio inayojenga. Scholars differ and that's healthy as long as there is no abuse and it's for the better of the country.