Jaji Warioba na Pro.Shivji wabishana kuhusu Bunge la Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Warioba na Pro.Shivji wabishana kuhusu Bunge la Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Oct 17, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Nimesoma mabishano au tofauti ya mtizamo kati ya prof Issa Shivji na Jaji warioba ktk gazeti la Raia mwema la leo. Nimeshangazwa na msimamo wa Jaji Warioba ninayemheshimu sana, nitaeleza.

  Kwa mujibu gazeti la Raia mwema la Leo wasomi hawa wawili wetofautiana juu ya wajumbe wa Bunge la Katiba.

  Msimamo Shivji;
  Akiwa katka Kongamano la Katiba Prof Shivji alisema;
  Kuna kasoro kubwa ktk sheria ya kuendesha mchakato wa katiba mpya, hasa kuhusu uundaji muundo wa Bunge la katiba. Chombo muhimu sana kuliko hata Refrendum ( kura ya maoni) ni Bunge la katiba. Linapaswa kuwa Bunge la wananchi, vinginevyo uhalali wa hiyo Bunge utakuwa na Shaka. Ni Busara kwa wajumbe wa Bunge la Katiba kuchaguliwa moja kwa moja wa Wananchi kwa ajili ya kazi hiyo maalum tu.

  Msimamo wa Jaji Warioba.
  Hata hivyo, akizungumzia hilo Mkiti wa Tume ya Mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba alimweleza mwandishi wetu akihoji; Utawapata wapi watu ( wajumbe wa Bunge la Katiba) ambao hawana maslahi na suala zito kama katiba ya nchi? Aliendelea ingawa jambo hilo siyo sehemu ya hadidu rejea kwa tume hiyo lakini ni suala la kidemokrasia pia kuwaingiza wabunge na wawakilishi kuwa sehemu ya Bunge la Katiba. Wabunge ni wawakilishi wa wananchi ni watu waliokabidhiwa pia jukumu la kutunga sheria.
  Alipoulizwa kuhusu wingi wa wabunge wa ccm ktk bunge hilo na kwamba watalinda maslahi ya chama chao alijibu, wabunge hao wametokana na mfumo wa demokrasia yetu na ndio mtazamo wa wananchi.

  My take;
  Hivi jaji Warioba hajui kuwa tunacholalamikia ni wingi wa kundi moja - wabunge, ambao nao wana maslahi lakini hatutaki wao wawe wengi huku makundi mengine ya wavua samaki, wakulima na wafanya kazi wakikosa fursa hiyo?

  2. Anaposema uwepo wabunge wengi wa ccm ni mtazamo wa wananchi, hajui kuwa moja ya sababu za kutungwa katiba mpya ni udhaifu wa Tume ya uchaguzi kutuletea viongozi wasiochaguliwa wakiwepo hao wa ccm wanaotuhumiwa kuchakachua kura wakisaidiwa na Tume.

  NB, Nadhani jaji wangu ninayemheshimu ameteleza ktk hili kama hajavutwa na ushabiki wa kichama zaidi
  .
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,289
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Mikael,
  Huyu Warioba alikuwa na misimamo isiyoyumba. Lakini tangu alivyovuruga mambo Mwananchi Gold, kila anapotaka kwenda kinyume na matakwa ya wakubwa anatishiwa kupelekwa mahakamani naye kuishia kunywea. Ondoa kabisa heshima uliyonayo kwa kibaraka huyu.
   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hii ndo mijadala ambayo inabidi iwepo . Tupingane ili tupate kitu bora katika ubishi wa kimanti. Warioba naona ameishajipa cheo kikubwa kuzidi alichonacho kwani ameishatangaza kuwa katiba itapatikana kabla ya 2015 utadhani yeye anabeba vichwa vyote vya watanzania
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Gagnija,
  Nadhani kwa jinsi ninavyo mwona siku za karibuni, nalazimika kukubaliana na wewe. No way out.
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Prof. Shivji ni kichwa, anaongea hali halisi anasukumwa na uzalendo pia waledi wa taluuma yake, Jaji warioba si wa kubeza pia anajiamini tatizo lake ni njaa, anasukumwa na tumbo. kama Jaji Warioma angekuwa na uzalendo asingekubali Tume yake watumie billion40 kwa miaka mitatu tu!

  Jaji Wariomba ni lazima afute matakwa ya waliomchagua kuwa pale, lakini akumbuke dunia inamuangalia atajishushia heshima yake aliojijengea tangu ujana wake... bado ana mapungufu
   
 6. j

  juju man Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  warioba,tumza heshima yako na usijaribu kutumiwa kwa maslahi ya wachache...dhambi unayoipanda itakutafuna wewe na kizazi chako....na taifa kwa ujumla...THINK BIG
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  sioni wa kuwamini wote wanapaswa waseme na kufanya mambo yanayoaminisha watu right away from hapa.Hakuna kumpa mtu blank cheque.Niwaonanvyo kila mmoja ana ajenda yake ya siri ila wana disguise kama wazalendo.Shivji anajipambanua kama undisputed intellectual ila si kweli kuwa mara zote ata balance knowledge yake,hisia zake zilizojificha na uzalendo. Nipo comfortable zaidi na warioba pamoja na njaa zake/ujamaa mchanganyiko wake kma si bangi za utotoni.Sijui kama Shirvji angekutana na Jussa kama angembana vyema kupitia njia halali hadi Jussa kujiona mjinga.Jussa alichobaki nacho ni kwenda kwa mabwana zake wakampe majibu after days.Im sure Shivji angemsaidia Jussa zaidi kupitia ufahamu wake.Kama kawaida angetoa somo la kuwalegeza wenzangu na mimi (bara)tusiojua sheria za katiba, halafu huku akimpa Jussa Leading questions(wa abuse laws km wapendavyo wazenj).

  Bado kuna malengo yanaweza fichika kwa wote wawili,sioni haja ya mtu kuwapa nguvu zaidi kwani by the time wana conclude malengo yao mtakuwa hamna nguvu tena ya kukataa credibility yao na hiyo kuyakataa waliyosema.
   
 8. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Tena huyo warioba mawazo yake sasa yanonesha dhahiri kua ana upeo mdogo kwa sasa...Maana CCM wao ndio wanaotaka katiba isiyokua na upeo wala maslahi kwa wanannchi halafu tena ukapeleke suala kama hili bungeni tena hapo kutapatikanika haki hapo mbona huyo warioba anachanganyikiwa sasa
   
 9. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0


  Kwa hoja hii niliyoleta leo, namuunga mkono shivji. Maoni yake yako very objective. Ninajaribu kutenganisha kesi ya kuku na mpaka wa kesi ya mpaka wa Shamba - ni vitu viwili tofauti. Kwa hiyo, ktk sakata hili prof Shivji yuko sahihi, kama ulitoufautiana naye kuhusu muungano ni jambo jingine tofauti
  .
   
 10. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,801
  Likes Received: 2,572
  Trophy Points: 280
  Bunge la katiba litakuwa na wajumbe 600, ie wabunge wote wa muungano,wakilishi wote wa baraza la wakilishi pamoja na wajumbe 180 wa kuteuliwa na Rais moja kwa moja ambo 1/3 kutoka Zanzibar. Hapa tumekwisha, hasa Wanzibari ambao watakuwa na wajumbe kupungua theluthi moja ya wajumbe wote. Zanzibar would have secured better deal EA ambapo kila nchi kubwa ndogo inayo wajumbe sawa kwenye vyombo yva maamuzi. Kwa hali hii tunatengeza katiba ya "CCM" no,no siyo ya Jamhuri. Kinimacho kinaendelea!
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Wala sipingani na malelezo kuwa yupo sahihi.Ila unaonaje hawa jamaa wakiwa sahihi na si sahihi alternatively kwa mambo tofauti katika katika kipindi cha mchakato mzima?Sijakataa wote wenye sababu zenye uzito wapewe haki yao,ila nani hajui mara nyingine sheria na haki ni vitu tofauti?

  Ninachoweza kusema na ndicho ninachotaka kusema ni kwamba,hawa jamaa wapewe sifa just pale wanapofanya chema.Praising them too much kutatupelekea waingize agenda zao ambazo hatutopenda matokeo.prof Shivji ni mpana sana ktk fani yake,lakini hakumaamnishi sana uzalendo wake, nia yake kuwa na vipimo hivyohivyo.Nadhani kama tunavyojituma hakikisha kuwa chama kinachoingia basi kifuate misingi ya nchi na si kuja na misingi yake, ndivyo basi hawa wasomi wetu watapaswa ishi kwa wanachodeliver na si walichowahi deliver.Bado namna bora ya maisha ya watanzania yanaweza yasitegemee umahiri wa yeyote katika sheria,kujenga hoja au lah.Kwani maisha halisia ni tofauti sana, na nadharia nyingi za kitauluma.

  Kwa walio wengi prof ni undidputed king,na hawana room ya ku question "motive behind".Watanzania tumekuwa tukianguka kwa vile tunamitazamo ya kinazi juu ya puplic figures zetu.Ndio maana hajutujui kwanini akina Chenge waliingia mikataba waliyoingi, kwanini UWT,polisi,wanasiasa, wasomi wa REDET,Bunge na wengine wanatumia THE BEST OF THEIR ABILITY TO DEFEND THOSE WHO KILL OUR NATION.Kama ni issue ya kuwepo na nani na kutokuwepo ni suala la watanzania wote, ila mwisho wa siku si practical kihivyo ,kwani watakaofinalize ni wachache wenye taaluma zao na wanaweza badili upepo sana, na tukitumia wawakilishi bado pia wanaweza pitisha tusivyovipenda.So wote wanapingana vitu visivyo perfect pande zote.Zaidi ni dhamira baada ya weledi katika kufanikisha.Wenye nia njema ktk wadau ndio watafanya vitu vitakavyokuwa fahari kwa taifa na uazao wao.Washenzi hawataangalia hivyo kwani hawaoni fahari kufanya chema.Sioni haja ya kuwa na kambi,ila kuongeza mawazo mema na pengine tunaweza kuwa na mseto wa makundi,hata hayo wanayobishania hawa jamaa.Wao wanapingania segment tuu za options tulizo nazo,sijui nani kawapa mamlaka ya kuona hayo tuu ndio yanatosha.
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Wote sioni pa kuwaamini,wasomi wetu wamekuwa watu wa hovyo sana na huwa wanakosa sana consistency ktk kumaintain integrity.Tufikie mahali tusiwe kazi yetu ni kujenga ma super star katika nchi ambao baadaye wanakuja kuwa out of our control.

  Mark my words.Tanzania ni nchi ya surprises, ipo siku unajikuta ukisema "fulani nilikuwa namuona....kumbe....".Ila itakuwa too late.Huu ubishi wao ni comedy tuu.watanzania tunahitaji zaidi ya haya,tunahitaji vitu vinavyowork na si vitu vyenye nadharia nzuri na weledi wa kitaaluma halafu hazifanyiki.

  Hembu tuende mbali zaidi ili hawa watu wawe nao wakitakiwa prove vitu zaidi kama wengine wasio na majina.Na yote wayafanyayo yasio ni leseni ya kuelekea kwa wasioguswa.
   
 13. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  The whole thing kuhusu mchakato wa katiba mpya is full of contradictions and uncertainties. What will be achieved is really a big mystery!
   
 14. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,801
  Likes Received: 2,572
  Trophy Points: 280
  One thing is certain, what will be achived is anything but peoples katiba.
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Hujawa wazi, kwa kifupi kati ya hao wawili kwenye hoja hii wewe unakubaliana na nani na kwanini? Baada ya hapo mimi nitakuwa kwenye nafasi nzuri kujibu hoja yako. Na tubase kwenye hoja hii tu
  .
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hapa tuko pamoja, ila kuwa out of control pia inatokana na sisi watz wasomi na wasio wasomi kutojiamini na kuwapapatikia watu wenye majina makubwa. No wonder kila mtu anataka kuwa kigogo ili aheshimiwe - small God. Hata hivyo, with time na hizi shule zetu za kata mambo yataboreka.
   
 17. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,910
  Likes Received: 12,090
  Trophy Points: 280
  Ukweli husemwa:

  Sija bahatika kuyasoma hayo majibizano na tofauti ya mitizamo yao kwenye gazeti, lakini kwa yale uliyoyaandika na maoni yako, inaonekana hujamtendea haki Jaji Warioba.

  Tatizo letu Watanzania, pale tunapomuona mtu anasema mambo mengi tunayoafikiana nayo kimaslahi au kiitikadi, basi hata yale mengine atakayoyasema ambayo ni pumba tunayaona ni mchele. Tumejengeka tabia ambayo pale tunapomwamini mtu fulani, basi tunakuwa kama vipofu wa fikra kwa kile akifanyacho.


  Tunatakiwa tujenge tabia ya kujongea kila jambo kwa walakini ili tuweze kubainisha kwa undani sababu zilizoko nyuma ya kila jambo kabla ya kulikubali.


  Kama Jaji Warioba alivyosema, 'Utawapata wapi watu ( wajumbe wa Bunge la Katiba) ambao hawana maslahi na suala zito kama katiba ya nchi'.

  Pro Shivji anasema haya kwa vile labda ana motive behind lakini vilevile kauli zake nyingi zinaonyesha kama anajaribu kuidhalau tume ya katiba.  Kumbuka wabunge ni wawakilishi wa wananchi ambao wanachaguliwa na wavua samaki, wakulima na wafanyakazi. Kwa mantiki na mchanganuo huo, lazima tu watakuwa ni wengi.


  Tatizo kubwa ambalo Watanzania linatusumbua katika mchakato mzima wa katiba ni kutanguliza maslahi ya kiitikadi kwanza badala ya uzalendo.


  Hatutaki kujifunza kutokana na makosa mengi ambayo tumechangia kuifikisha nchi hapa ilipo.


  Hebu tujaribu kuwa wazalendo kwa hili.
   
 18. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama ni sahihi sana kwa Jaji Warioba kudai kwamba composition ya bunge tulilo nalo sasa ambalo wabunge wengi ni wa ccm ndio mtazamo ama matakwa ya wananchi kwa sasa.

  Sababu mojawapo ya kushinikiza uwepo wa katiba mpya ni pamoja na mapungufu makubwa yaliyopo katika katiba ya sasa ambayo kwa namna moja ama nyingine imepelekea wakati mwingine tume ya taifa ya uchaguzi kumtangaza mshindi ambaye si chaguo la wananchi. Tunayo mifano ya baadhi ya wabunge ambao hadi leo hii hawathubutu kukanyaga majimboni mwao, na kama wakienda wanafanya hivyo wakiwa na escort ya polisi, wengine wanakwenda kwa kificho na hawajawahi kufanya japo mkutano wa hadhara mmoja tangu watangazwe kuwa washindi.

  Na kwa vyovyote vile uwingi wa wabunge wa ccm katika bunge la katiba ni wazi kwamba tutakwenda kuletewa katiba ya ccm na si katiba ya wananchi kama tulivyotarajia. Kwahiyo ni muhimu katika hali hiyo wananchi wenyewe tupewe nafasi/mamlaka ya kuchagua wabunge/wawakilishi wetu katika bunge la katiba. Inawezekana kabisa kumpigia kura (kumchagua) mbunge mwaka 201o lakini miaka miwili baadae yaani 2012 tunagundua kwamba hajakidhi matarajio yetu, hawakilishi matakwa yetu na tungekuwa na nafasi bila shaka tungeweza kumuweka pembeni kwahiyo hoja ya Jaji Warioba inakuwa haina mashiko sana.

  Nakubaliana na hoja ya Jaji Warioba kwamba mojawapo ya kazi ya wabunge ni kutunga sheria lakini ni muhimu azingatie kwamba hii ni sheria ya kipekee, hii ni sheria mama, hii ndio nguzo/ mhimili wa sheria nyingine, na ndio maana haitungwi hovyo hovyo, ina utaratibu wake maalum na tofauti, na ndio sababu ikaundiwa tume maalum anayoingoza yeye kwa ajili ya kukusanya maoni ya wananchi kitu ambacho ni tofauti na utaratibu wa utungaji wa sheria nyingine.

  Katika hili ninakubaliana moja kwa moja na mawazo ya Prof.Shivji kwamba wananchi wenyewe ndio wanatakiwa kuchagua wawkilishi wao kwa ajili ya bunge hili maalum la katiba. Jaji Warioba katika hili inabidi aachane kabisa na mambo ya kuweka uccm katika jambo hili muhimu kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu kwani katiba nzuri na inayotokana na matakwa ya wananchi wenyewe ndiyo itakayotuletea demokrasia pana na ya ukweli, lakini pia ndiyo itachagiza maendeleo ya nchi yetu kwa miaka mingine 100 au hata 200 ijayo.
   
 19. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kwani yeye aliacha lini ukada wa CCM? Maana ameshakuwa mpaka waziri mkuu!
  Siamini kama ataweka pembeni maslahi ya chama chake.
   
 20. b

  bdo JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa (Warioba) hata huko kwao Bunda hakutakiwa kuwa (MB)kwa mambo yake yasiyoeleweka, hivi walipomteua walitumia vigezo gani?nilishangaa yeye kuwa mwenyekiti wa Tume na Jaji Augustino Ramadhani(alistahili kuwa mwenyekiti)instead akapewa umakamu
   
Loading...