Jaji Warioba: Matamko ya viongozi hayasaidii kutatua tatizo la madawa ya kulevya

Matulo

Member
Dec 7, 2011
70
25
"Hebu niwaulize, hii ni mara ya kwanza majina kutajwa, tukianzia list of shame, si viongozi waliharibiwa heshima yao, mbona hatukuona vyombo vya habari kuwatetea watu hao"

Ni hivi, hakuna anayepinga vita dhidi ya dawa za kulevya Mzee wetu Warioba, tatizo ni appoach ya kutatua janga hilo iliyotia shaka, Hivi kweli List of shame, ambayo ilihusu kashfa tata zilizotikisa nchi, Meremeta, Kagoda etc, ambazo hadi leo imeshindikana kutoa ufumbuzi wake; utalinganisha na kutajwa jukwaani, ukihusishwa na Madawa ya Kulevya na kama ikionekana huna hatia ukaachiwa? Utasafishwa kwa sabuni gani hadi umma ukuamini tena, hasa ukiwa Mtumishi wa Mungu au Mtu mwingine mashuhuri ambaye Jamii inakuona kama kioo?

=======

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amelizungumzia sakata la vita ya dawa za kulevya na kuvitaka vyombo vya habari na viongozi watoe elimu na kufanya utafiti wa kina ili kupata suluhisho la tatizo hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumapili, Jaji Warioba alisema ni wakati mwafaka kwa kila mmoja kusoma sheria kuhusu makosa ya uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya na kuvitaka vyombo vya habari viichambue kuangalia kama inafaa au ina mapungufu.

“Jamii isi- ‘dili’ na watu walioathirika tu, mnafikiri suala ni kumfunga anayetumia dawa za kulevya au anayefundishwa kutumia dawa za kulevya?” alihoji.

Alisema kama ni utafiti ufanyike kwa wanaosababisha na walioathirika badala ya kujikita na matamko ya viongozi ambayo alisema hayasaidii kulimaliza tatizo hilo.

Jaji Warioba ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema ni vyema kama wananchi wakaelekezwa wafanye nini ili kupambana na tatizo hilo badala ya kujikita katika siasa na watu.

Alisema kwa kuwa kuna sheria inayoeleza tatizo ni nini na kuna utaratibu wa namna ya kuitumia, basi wananchi wangefundishwa ili wafahamu kitakachowasibu pindi watakapojihusisha na dawa hizo haramu.

Alisema itafutwe njia ya kushughulikia tatizo la dawa za kulevya badala ya kulumbana na kutoa matamko kwani hayasaidii kumaliza tatizo.

Sakata la dawa za kulevya liliibuliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutaja orodha ya watu wanaodaiwa kutumia au kujihusisha na biashara ya dawa hizo. Orodha hiyo iliyotolewa katika vipindi viwili tofauti, Februari 3 na Februari 13 ilijumuisha majina ya wasanii, viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wakubwa.

Miongoni mwa waliotajwa katika orodha hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, mfanyabiashara maarufu na mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga, Yusuf Manji na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima pamoja na msanii wa filamu, Wema Sepetu.

Mtindo wa Makonda kutaja majina ya watu uliibua mjadala mzito ambapo baadhi ya wabunge walikosoa kitendo hicho wakidai kuwa ni cha udhalilishaji.

Aidha Jaji Warioba hakupendezwa na jinsi vyombo vya habari nchini vilivyolishikia bango suala la dawa za kulevya na kulihusisha na siasa na kusema kwamba wapo viongozi wengi waliotajwa majina yao kwenye kashfa mbalimbali kipindi cha nyuma na kuharibiwa heshima lakini vyombo vya habari viliona ni mambo ya kawaida.

“Hebu niwaulize, hii ni mara ya kwanza kwa majina kutajwa? Tukianzia ‘list of shame,’ si viongozi waliharibiwa heshima? Mbona hatukuona vyombo vya habari kuwatetea wale walioharibiwa heshima? Kuna viongozi wengi waliharibiwa heshima lakini haikuwa ishu, leo hii kumezidi nini mpaka kutajwa hao waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya imekuwa ishu?” alihoji.

Alisema wapo viongozi (bila kuwataja) waliowahi kumuita Rais ni kuwa ni uchwara, wengine walimuita dhaifu lakini halikuwa jambo la ajabu.

“Mnasema heshima ya mtu imeharibiwa, je, kumuita rais ni uchwara si ni kumharibia heshima yake?” alihoji.

Alisema linapokuja suala kubwa la kupambana na dawa za kulevya, tatizo lenyewe linakwepwa na watu wanaanza kuibua malumbano.

“Hivi mkimjadili Makonda inawasaidia nini au kama kuna wanaomuunga mkono Makonda na wasiomuunga mkono itawasaidia nini?” alihoji Jaji Warioba.

Pia Jaji huyo alisema kuwa nchi ina matatizo mengi lakini watu wamejikita katika siasa tu.

Alisema hadi bungeni walisema wamedhalilishwa lakini na wao huko nyuma walitoa matamko ya kudhalilisha wenzao na hata kumhusisha rais na dawa za kulevya.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu hana maana ni opportunist, he is irrelevant, quite so...amesubiri kuona upepo unakoelekea ndo anajitokeza kujifanya ana hekima, akafie mbele huko sisi umma tutashinda wenyewe, wao waendelee kufanya kazi yao kumlamba magu miguu pale magogoni!
 
Mzee amesahau kuwa vyombo vya habari vinaendana na reactions zinazotokea kwenye jambo husika. Laiti kwenye list of shame wahusika wangesema wanaenda mahakamani au kulifanya mjadala lazima vyombo vya habari vingeenda nalo tu.

Hata Mzee angekomalia ishu ya kufanyiwa fujo na Daudi wkt wa katiba mpya lazima vyombo vya habari vingeenda nalo tu.

Mzee tulia muziki umefika mahali pale.
 
Huyu hana maana ni opportunist, he is irrelevant, quite so...amesubiri kuona upepo unakoelekea ndo anajitokeza kujifanya ana hekima, akafie mbele huko sisi umma tutashinda wenyewe, wao waendelee kufanya kazi yao kumlamba magu miguu pale magogoni!
Tatizo ninyi kila anayeongea tofauti na mtazamo ni kumpinga tu. Hamuangalii mantiki. Ipo siku utaambiwa Mbowe anatembea na mke wako utasifia kuwa ni kitendo cha kikamanda!
 
Huyu hana maana ni opportunist, he is irrelevant, quite so...amesubiri kuona upepo unakoelekea ndo anajitokeza kujifanya ana hekima, akafie mbele huko sisi umma tutashinda wenyewe, wao waendelee kufanya kazi yao kumlamba magu miguu pale magogoni!
Ukweli unauma

Ukiwa mwelewa usingesema haya ila kwa kuwa ni makada lazima mtaumia ,mtu ambaye yupo neutral amemuelewa mh Warioba

Tatizo mlionayo chadema&ccm mtu akiwa against na nyie kidogo mnaanza kutokwa mapovu na kashfa kibao,kwenye ishu ya katiba mlimsifia huku ccm wakimponda leo imekuwa vice versa?



Kudos Warioba sema unayoyaamini ila yawe ya haki na ya ukweli,simamia haki

Tatizo ya ukweli huwa inachoma
 
Back
Top Bottom