Jaji Warioba: Matamanio ya katiba mpya bado yapo nchini

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
3,863
2,000
Jaji Warioba aibua tena katiba mpya. Nipashe yanukuu mahojiano kipindi Konani ITV.

Asema lipo hitaji kubwa kupata katiba mpya, japo kwa haraka tunahitaji maboresho ya dharula tume huru ya uchaguzi.

Vinginevyo katiba iboreshwe tusiwe na uchaguzi mkuu 2020 waliopo waendelee miaka mitano zaidi, ili pesa uchaguzi zifanyanye mchakato katiba mpya, ndani ya miaka mitano ijayo.

======

Warioba.jpg

Jaji Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba
Warioba aliyasema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Konani kinachorushwa na televisheni ya ITV.
Mchakato wa Katiba mpya ulisimamiwa na iliyokuwa Tume ya Marekebisho ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Warioba ambao waliandaa Rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa Desemba 30, mwaka 2013.

Akizungumza kuhusu Katiba Mpya, Warioba ambaye katika mchakato huo alisema haiwezi kuzuiliwa kwa sababu ya gharama.

“Tume ya Katiba Mpya ilichukua maoni nchi nzima ilikuwa ni gharama, lakini zinafaida zake kwa sababu tunajua maoni ya wananchi na yapo yametunzwa.

“Bunge Maalum la Katiba lilikuwa na gharama, lakini lilikamilika, gharama iliyobaki ni kupata kura za maoni.
“Nitastaajabu kama mnataka uchaguzi na kura ya maoni ni uchaguzi ikiwa mtachagua viongozi ni sawa, lakini wananchi wakitaka kutunga Katiba yao siyo sawa, mnasema gharama, hii siielewi.”

Katika mahojiano hayo Jaji Warioba alisema hata uchaguzi gharama zake ni kubwa, na kufafanua kuwa katiba ndiyo moyo wa taifa, na kwamba haiwezi kuzuilika.

“Kwa kusema hivyo, yapo mambo mengi utayaacha sioni kama ni gharama kubwa sana… huko nyuma tulizitengeneza zilikuwa na gharama mfano ni Katiba ya mwaka 1977 ilikuwa na gharama, mambo ya maendeleo ni gharama, lazima tuyakubali,” alisema.

Akizungumzia Katiba iliyopo, Jaji Warioba alisema ina afya, na kwamba Katiba Mpya kazi yake ni kuboresha yaliyopo.
Hata hivyo, alisema Katiba Mpya utangulizi wake ni mzito zaidi ambao unaonyesha dhamira ya kuitunga na katika sura ya nne na ya tano imefafanua madaraka ya wananchi.

“Imefafanua zaidi kuwa Katiba ni Sheria Kuu, pia imeingiza umuhimu wa utamaduni wa kitaifa ndiyo maana ya tunu, imefafanua kwa upana zaidi malengo ya nchi inakoelekea, imeweka misingi ya uongozi na miiko ya uongozi na haki za binadamu na uraia,” alisema.

Kuhusu tunu za Taifa, Jaji Warioba alisema Tume ilizipendekeza na ameona katika serikali ya awamu ya tano inasukuma mambo hayo ambayo yangekuwa msingi wa utamaduni wa nchi.

“Tunataka uadilifu, tunataka kukwepa rushwa, tunataka nidhamu, katika Katiba Mpya haya ndiyo tunu, lazima yaingie kwenye Katiba, Katiba ndiyo Sheria Kuu hivyo yakiwamo humo mtu yeyote atakayekwenda kinyume basi anakuwa katika matatizo,” alisema.

Akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya, Jaji Warioba alisema lazima itakuja na kwamba yote aliyozungumza huwa yanachukua muda na kutolea mfano Katiba ya mwaka 1977 ambayo walikaa tangu mwaka 1965, lakini ilikuja baadaye.

“Mabadiliko yatakuja, sina wasiwasi juu ya hilo, ninaamini kazi kubwa imeshafanywa ya kufikia Katiba Mpya huwezi kuzuia kuwa na mabadiliko katika katiba, kazi kubwa itakapofika hakuna tatizo kubwa kwa sababu kila kitu kinafahamika ni kukamilisha tu,” alisisitiza Jaji Warioba na kuongeza:

“Huwezi kuzuia mabadiliko, Katiba ni sheria kama nyingine, kama kutokea mabadiliko lazima yafanyike.”
Alipoulizwa kama kuna ambacho kilimvunjia heshima wakati wa mchakato huo ukiendelea, alisema yaliyotokea wakati wote yalikuwa ya kawaida hasa inapotokea mtu anapokuwa kiongozi.

“Nilipata lawama, lakini haikunitikisa, tulipopeleka mapendekezo Bunge Maalum la Katiba mengi yalisemwa, walinisema, lakini tuliendelea na kazi… kiongozi ukiwa katika nafasi fulani ujue hutawapendeza watu wote.
“Yapo maneno mazito yalisemwa juu yangu, lakini nilichukulia ni jukumu la uongozi, sikuchukua hatua yoyote,” alisema Jaji Warioba aliyeongoza tume hiyo iliyokuwa na wajumbe 30 kutoka sehemu zote za Muungano wa Tanzania.

MADAI YA KUPIGWA
Jaji Warioba alikanusha madai ya kwamba alipigwa baada ya kuzuka vurugu Novemba, mwaka 2014 wakati wa mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa Katiba Mpya jijini Dar es Salaam.
“Sikupigwa, kilichotokea ni vurugu kwenye kikao kimoja, hiyo ni mambo ya media (vyombo vya habari), sikupigwa,” alisisitiza.

TUME HURU YA UCHAGUZI
Kuhusu tume huru ya uchaguzi, alisema ni moja ya taasisi ambazo zimeainishwa katika katiba.
“Mapendekezo ya wananchi yaliyotoa ni kwamba Tume siyo huru, walipendekeza isingeteuliwa na Rais, Katiba Mpya ilikuwa na haya, chombo chochote lazima kiwe na mteuzi.

KIPINDI CHA URAIS
Kuhusu muda wa urais, alisema miaka kumi inamtosha mtu kufanya mambo mengi na kueleza kuwa mabadiliko yanaletwa na mawazo mapya ambayo yanatoka kwa vijana.

Akiongelea kuhusu suala la viongozi kutoshtakiwa, alisema suala hilo ni la kawaida, hata hiyo imeweka misingi ya kushtaki viongozi na Rais analindwa ili kutekeleza majukumu yake na ana ulinzi wa sheria.
Alipoulizwa kama Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa anaandaa maraisi, alisema alikuwa haandai, bali aliamini cheo ni dhamana siyo mali yake.

“Ndiye mtu alikuwa anaamua kuachia madaraka, mara nyingi viongozi hawataki kuachia madaraka, lazima ifike wakati yale mambo waliyozungumzwa kama tunu ambayo ndiyo yanaleta utamaduni wa taifa, yaangaliwe vizuri.
“Haya mambo ndiyo yanaleta matatizo kwenye uongozi unakuta viongozi wasio na nidhamu, uadilifu, uaminifu hii tunataka iwe katika Katiba Mpya ili iwe muongozo wa katiba.

“Unakuta viongozi wengine hawafuati misingi ya uongozi, mwingine anatumia madaraka vibaya, lazima iwe katika katiba ili iwe miiko.”

YANAYOENDELEA CCM
Kuhusu baadhi ya viongozi ambao wameitwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhojiwa, Jaji Warioba alisema siyo kitu kipya, na kwamba hakuna chama ambacho hakitakuwa na vuguvugu.

“CCM imekuwa hivyo, wakati wote tangu wakati wa Tanu, kumekuwa na majadiliano, mnajadiliana na viongozi… hata huko nyuma walifanya hivyo, viongozi walifukuzwa, siyo kitu kipya,” alisema.


Chanzo: Nipashe
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,145
2,000
February 10, 2020
Dar es Salaam, Tanzania

ITV Kipindi Konani : Judge Joseph Warioba afunguka mambo mengi ikiwemo kupigwa.

Jaji Warioba ni msomi mwenye digrii toka vyuo vikuu vya UDSM na The Hague Academy of International Law The Hague Academy of International Law


Jaji Joseph Warioba alipata kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Jaji wa East African Court of Justice, Mjumbe wa Baraza la Kimataifa kusuluhisha Migogoro ya Mipaka ya Nchi iliyopo Baharini ITLOS Germany -based International Tribunal for the Law of the Sea United Nations Convention on the Law of the Sea , Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mwalimu Nyerere Foundation Publications – By Mwalimu – NYERERE FOUNDATION na pia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania. Pia aliwahi kuhudumu kama Mwanasheria wa Jiji (City Council) la Dar es Salaam, Tanzania.

Source : ITV Tanzania
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
4,477
2,000
Warioba tumia ushawishi wako katika chama chenu,lakini ukiona hukubaliwi ujue uko peke yako,na ukilazimisha hutaweza kukinga makonde mazito toka kwa karateka sensei Makonda.Safari hii utapelekwa na ambulance.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
3,863
2,000
Warioba tumia ushawishi wako katika chama chenu,lakini ukiona hukubaliwi ujue uko peke yako,na ukilazimisha hutaweza kukinga makonde mazito toka kwa karateka sensei Makonda.Safari hii utapelekwa na ambulance.
Mzee Warioba ni miongoni mwa Watanzania wachache wenye hekima wasio wanafiki.Nilitarajia wenye hekima wengi wamuunge mkono wakati huu wa uhitaji mkubwa wa hoja zake. Ajabu akianguka ,kupumzika watajitokeza lukuki na sifa za kinafki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,145
2,000
February 10, 2020
Dar-Es-Salaam, Tanzania

"Wanaotaka Rais aliyepo madarakani abaki wana maslahi binafsi " - Jaji Joseph Warioba

Jaji Warioba aelezea maana pana ya ukomo wa Rais kubakia madarakani katika nchi ambayo ni Jamhuri ya watu-huru kwa maana nyingine taifa lisilo koloni au nchi ya kifalme / kisultani.


Source: ITV Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom