Jaji Warioba: Kuteswa ka Kibanda kulipangwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Warioba: Kuteswa ka Kibanda kulipangwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Mar 8, 2013.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,765
  Likes Received: 11,002
  Trophy Points: 280
  Jaji mkuu mstaafu Jaji Sinde Warioba amedai kuwa kipigo na mateso aliyoyapata Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini bwana Kibanda ni tukio la kupangwa na si la kiarifu kama ilivyodaiwa na Kamanda Kova mzee wa seriez.

  Concern:
  Kama ni mipango na mchunguzi mkuu (Kova) keshatoa taarifa za mwanzo kuwa ni uharifu tutarajie nini kama mtuhumiwa ajichunguze mwenyewe.

  Haaiingii akilini hivi raia wa kawaida atatembeaje na bunduki (smg) usiku kama si askari?
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,373
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  mimi nachukia sana unafiki wa hawa watu, warioba, viongozi wa kijamii, viongozi wa kidini mlikuwa wapi Dr. Ulimboka alipokuwa analia kuwa amepigwa na maofisa wa ikulu. watu wote niliowataja hapo walikaa kimya isipokuwa wana harakati wachache ndio walijitokeza kuiomba ikulu itoe maelezo kuhusiana na tukio hilo. kwanini viongozi wote hao wasijitokeze hadharani kusimamia ukweli wakati muhimu wanapokuwa wanaitajika. leo wanaibuka na issue ya kibanda wakati hakuna tofauti yeyote katika issue hizi mbili.
   
 3. f

  frank cain JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 17, 2012
  Messages: 470
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama makosa yalifanyika nyuma hatuna haja ya kuendelea kuyafanya sasa. kama zaman tulinyamazia uovu haitakiwi hata leo tuendelee kunyamazia uovu. na baadae tuendelee kunyamazia uovu.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2013
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,218
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kova alishasema ule si uhalifu kwani hapakuwa na wizi wowote. Lile ni tukio la kisasi tu
   
 5. successor

  successor JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2013
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 1,856
  Likes Received: 2,736
  Trophy Points: 280
  Tusitarajie mapya kutoka kwa hawa polisi wetu....kwani yaliyopita yana tofauti gani na hili, ngedere amchunguze nyani.
   
 6. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2013
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wasauzi wanatushangaa tunavyojua kung'oana kucha
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,045
  Likes Received: 2,290
  Trophy Points: 280
  Lile tukio la Mwangosi kwa maoni yangu ndio kama 'litmus'.....kama waliweza "kukataa" kuhusika katika tukio lile basi itakuwa ni miujiza kukubali katika matukio haya mengine!
   
 8. h

  hoyce JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2013
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,121
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kichwa chako hakina kumbukumbu. Hao wote uliowataja walitoa matamko yao wakati wa Ulimboka. Labda hukuyasoma. Jipange kutoa hoj nyingine.
   
 9. Konya

  Konya JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kwa haya yanayotokea kila kukicha (utekaji,utesaji,uuaji wa makusudi wa raia wasio na hatia) na ambacho Ikulu wakati mwingine kuelezwa kuhusika,kumeifanya kusiwe(ikulu) mahala patakatifu tena
   
 10. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na Mh. Warioba 100%. Kama Serikali inataka kujinasua katika hizi lawama basi iombe msaada toka FBI ya Merikani au Scotland Yard ya Uingereza kuchunguza. Kutumia Kova ni kugeresha tu.


  Ikumbukwe kwamba hivi karibuni Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar ilikaribisha FBI kuchunguza mauaji yaliyoonekana ni vigumu Polisi wetu kuchunguza.
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,859
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Then viongozi wa jeshi la Police wajiuzuru kwa kushindwa kazi. Maana haina maana walipwe mishahara wakati kazi hawafanyi. Wao ni kutoa matamko hata kabla ya uchunguzi. Sasa kama Kova anasema ni waharifu mbona anashindwa kuwakamata?? Kuwaleta FBI ni ushahidi tosha kuwa hakuna kinachoendelea hapa. Rais anatakiwa kuwawajibisha hawa kwa vile kila mmoja wetu pamoja na serikali yenyewe wamekubali kushindwa kazi na ndiyo sababu wanatafuta msaada wa FBI!!
   
 12. l

  lufungulo k JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 1,432
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Tutegemee mengi kutokea ,kwani viongozi wetu wanaona gharama za usalama wetu ni kubwa mnoooooooo.
   
 13. s

  salmar JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 784
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 45
  Yuko wapi nchimbi atutangazie na sisi bara kuna magaidi yana baka yana kongota ni ma dentist waje FBI wachunguze yuko wapi mzee mwana kijiji aje atuambie hawa watu walokua mahodari wa kutoa meno na kucha ni magaidi wanatoka zanzibar mmmmmmmhhhh tanzania eeeee mwanangu kuwa uyaone
   
 14. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2013
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Kova si mzee wa movies?
   
 15. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280

  Mbowe na Tanzania Daima wanayo siri ya Kutekwa na Kujeruhiwa kwa Kibanda

  Salaam Wakuu,
  Tasnia ya Habari kwa sasa imejawa na simanzi kutokana na kitendo cha kuvamiwa na kuumizwa na watu ambao hawajabainika walikuwa na lengo gani. Mimi kwa ujumla nimesikitishwa sana kutokana na tukio hilo na nawalaani wote waliohusika. Aidha, natumia fursa hii kumuombea ndugu yetu Kibanda apone kwa haraka ili arejee nyumbani salama kuungana na familia yake na hatimaye kuendelea na majukumu yake.

  Baada maelezo hayo, naomba kwa pamoja tutafakari mambo yafuatayo;


  1. Juzi Jumanne tarehe 05/03/2013 kulikuwa na kikao cha wadau wa demokrasia nchini kilichoandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini (Tanzania Centre for Democracy – TCD). Wenyeviti wa vyama vyote vya siasa ni wajumbe na walipata barua za mwaliko kuhudhuria kikao hicho. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), FREEMAN MBOWE, ni miongoni mwa wajumbe walioalikwa. Hata hivyo, Mbowe alitoa udhuru ya kutohudhuria kikao hicho kwa madai kuwa atakuwa jimboni kwake, Hai kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri wilaya ya Hai (Full Council). Hizi zote ni facts na mimi nikiwa miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho, nilimsikia ANTHONY KOMU, Mkurugenzi wa Utawala wa CHADEMA ambaye ndiye alimwakilisha Mbowe akitoa maelezo hayo.
  2. Hata hivyo, katika tukio la kuvamiwa na kuumizwa vibaya kwaAbsalom Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri wa New Habari Corporation (2006), Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameonekana Hospitali ya Taifa ya Mhimbili akimjulia hali ndugun yetu Kibanda.
  3. Pia hakuna uthibitisho kuwa Mbowe alienda jimboni kwake kama alivyodai wakati akitoa udhuru wa kutohudhuria kikao cha TCD.
  4. Kwa vile kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa, KIBANDA amekuwa na mgogoro na Tanzania Daima gazeti ambalo linamilikiwa na FREEMAN MBOWE, na kwa vile KIBANDA ana siri nyingi sana za CHADEMA na kwa hali hiyo viongozi wa Chama hicho wanamuona kama ni adui, na kwa kuwa kitendo cha Mbowe kutohudhuria kikao cha TCD kilitumika tu kama ushahidi wa yeye kutokuwepo Dar es Salaam wakati wa tukio hilo na hivyo asiwe mshukiwa nambari moja, kitendo cha yeye kuonekana Hospitali ya Mhimbili akimsalimia KIBANDA, kilinishtua na kuniachia maswali mengi.
   
 16. L

  Loka G Laizer Member

  #16
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  angalia wasije 2jeruia roma we2 maana dah!
   
 17. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  huu ndio ukweli mchungu, kova anatakiwa aanzie hapa.kovaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa njooooooooooooooooo uchukue ushahidi wa mateso na watesaji wa kibandaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 18. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Nasi tumezidi kuilaumu serikali na hivyo maadui zetu kutumia mianya hiyo kutudhuru huku wakijua lawama zitawaendelea viongozi wa serikali
   
 19. taamu

  taamu JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2013
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 4,240
  Likes Received: 620
  Trophy Points: 280
  vipi raisi awawajibishe ikiwa yeye mwenyewe ahitaji kuwajibishwa kwa maswala mengine uchafu hauwezi kujiondosha.
   
 20. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nashangaa sana POLISI sijui wanawaogopa hawa CDM, mazingira yanaonesha wazi kabisa kuhusika na hili tukio bado wana delay na ndiyo maana Serikali inalaumiwa kuwa haichukui hatua.
   
Loading...