Jaji Warioba: Kurudia Uchaguzi Zanzibar ni Hatari

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Akihojiwa na ITV Jaji warioba amesema kurudia Uchaguzi Zanzibar ni hatari na inaweza kupelekea umwagaji wa damu.

Jaji Warioba amesema ni vema atafutwe msuluhishi wa katikati na pande zote zirudi mezani.

MyTake: Kada wa CCM amemkataa Jecha,Bado kuna watu wanajitoa ufahamu,muda utawadia,Asiyesikia la mkuu huvujika guu.Guu la CCM lipo hatarini

=============
Akiongea jana Jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa ili kutuliza mzozo huo wa kisiasa visiwani humo ni bora akapatikana msuluhishi watatu ambaye anaweza kusuluhisha mgogoro huo ili kuepuka damu kumwagika.

Jaji Warioba amesema kuingia katika kutafuta uongozi mpya bila kuwa na maridhiano ya vyama vyote Zanzibar inaweza ikarudia machafuko kama yaliyotokea katika kipindi cha miaka ya nyuma jambo ambali litaichafua Tanzania.

Aidha waziri mkuu huyo mstaafu amesema kuwa vyama vinapaswa kuachana na dhana ya kwamba malumbano hayo ni ya kivyama zaidi na badala yake watoke katika dhana hiyo na waweze kuwajali wananchi wa visiwa hivyo na kujua ni kitatokea baada ya Uchaguzi.

Kwa upande wake Prof. Mwesiga Baregu amesema licha ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kutoa sababu tisa za kufuta uchaguzi huo lakini alikiuka katiba ya Zanzibar pamoja na sheria za uchaguzi halali ambayo inaweza kuchafua siasa za Tanzania.
 
Zanzbar Inahitaji Maombi !
Lakini inahitaji Ukweli zaidi !!

Kuna watu wanapotosha kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar wakidai ni wa marudio !

Ukweli ni kwamba ni Uchaguzi mpya unohitaji
Kuanza Upya Na wagombea waombe upya!!

Sifa za Uchaguzi wa Marudio kwa mujibu wa sheria duniani kote:

Kwanza :
Uchaguzi wa marudio
ni
ule ulioharibika kwenye
baadhi
ya maeneo ,Na hurudia maeneo husika .

Pili :
Uchaguzi wa Marudio ni ule ambao unaoongozwa

Na Sheria inayomtaka mshindi
kupata asilimia ya kura zaidi nusu ya waliopiga kura ,

Sifa za Uchaguzi uliofutwa :

1:Uchaguzi uliofutwa ni zaidi ya kuharibika''

2:Ni kama hakuna kilichokuwa kinafanyika

3heria zilikiukwa
kuanzia Uteuzi wa wagombea ,,,'

4:Wapiga kura walio wengi
hawakuwa Na sifa za kupiga kura

5:Upigaji kura haukukamilika katika maeneo yaliyo
Mengi !

6:Ni vigumu kuyatambua Na kuhakiki matokeo yaliyotoka vituoni. Nk

7:Ni kitu cha kuanza Upya kila hatua ikiwemo uteuzi wa wagombea

Kwa Maoni yangu :

Hii Tabia ya kurudia Mtihani
darasa zima, Kisa Mtoto wa
mwaalimu kafeli !!

Ikiendekezwa itatupeleka Tanzania pabaya !

Mwana wa Adili :
Kiwaryalema
 
uchaguzi urudiweeee

Nyati akiisha kuanguka kujifanya kumkata shingo ni uongo tu. Kile nacho ni kibudu ila tamaa na uchu ndo hutufanya tuhalalishe. Urudiweeee! Dah! Ili iweje? Picha ni nyingine zinawekwa au? Kama bi bao la mkono hakuna haja, miaka yoote CUF ikiambiwa imeshindwa mbona hamkurudia. Wapeni wazanzibari haki yao. Msiwabughudhi kwa kura maruhani
 
Akihojiwa na ITV Jaji warioba amesema kurudia Uchaguzi Zanzibar ni hatari na inaweza kupelekea umwagaji wa damu.

Jaji Warioba amesema ni vema atafutwe msuluhishi wa katikati na pande zote zirudi mezani.

MyTake: Kada wa CCM amemkataa Jecha,Bado kuna watu wanajitoa ufahamu,muda utawadia,Asiyesikia la mkuu huvujika guu.Guu la CCM lipo hatarini
Nimemskia Shein akitoa vitisho badala ya kutumia busara hata ya kunyamaza..yangu macho maskio
 
Mezani watarudije sasa wakati maalim hataki? suala siyo kukosekana mtu wa kati, tatizo ni maalim yeye anataka atangazwe mshindi kwa uchaguzi uliopita
 
Baada ya kushinda kimagumashi mtihani wa uchaguzi mkuu bara sasa huu wa Zanzibar ni mtihani wa pili na lazima mtu aangukie pua.
 
Warioba alishaonana na rais Magufuli je alimtahadharisha kuhusu hilo?
 
Wazee wetu walichelewa sana kuyasema haya mapema hila kama wameyaona ni bora busara zitumike katika huu mkwamo
 
huyu mzee ni kada wa ccm kindakindaki sio km wachumia tumbo kama akina January,mwakembe,mwigulu wanaofanya siasa maji taka na za kimajungu. Mzee kaona kina kitu kimekosewa na ubabe ukiendelezwa tutapoteza ata hiki kidogo tulichonacho. Na jinsi ccm ni mankurunziza hawawezi kusikia wala kuona wao ni tamaa ya madaraka.
 
Back
Top Bottom