Jaji Warioba: Kuna dalili za uwepo wa matukio yanayodhoofisha uzalendo na umoja wa Taifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
wariobapx.gif

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba
JAJI Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania amesema, kuna dalili za uwepo wa matukio yanayodhoofisha umoja, uzalendo na mshikamano wa Taifa.

Jaji Warioba amesema hayo leo tarehe 24 Septemba 2019, katika hafla ya uzinduzi wa Tamasha la 14 la Jinsia linalofanyika katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mabibo jijini Dar es Salaam.

“…kuna dalili za hapa na pale, ambako unaona kuna majaribu ya kudhoofisha umoja wetu, mshikamano wetu,” amesema Jaji Warioba.

Jaji Warioba amesema, nguvu ya Tanzania ni umoja, mshikamano na uzalendo na kwamba wanawake wana nafasi kubwa ya kuhakikisha nguzo hizo zinakuwa imara.

Akitolea mfano mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya uliofanyika mwaka 2013, Jaji Warioba amesema wanawake walitoa mapendekezo yao bila ya kuwa na mgawanyiko wa kiitikadi ama siasa.
“Watanzania nguvu yetu iko kwenye udugu wetu, ndio nguvu tuliyonayo, na tuna amani, umoja ushirikiano na uzalendo. Ni muhimu tulinde uhuru, mshikamano wetu na uzalendo wetu. Lakini wanawake wa nchi hii, ndio ambao wana dhamana ya kulinda umoja wetu na mshikamano wetu,” amesema Jaji Warioba na kuongeza.
“Nilikwenda Bagamoyo nilikuta kuna semina ya wabunge wanawake, wanazungumza lugha moja hawakugawanyika kwamba hawa CCM, CHADEMA, CUF wanazungumza mambo ya kitaifa. Tulipokuwa na jukwaa la katiba, kikundi pekee ambacho kilitoa mapendekezo bila mgawanyiko ni wawanake.

Tamasha la 14 la Jinsia linafanyika kwa siku nne kuanzia leo hadi tarehe 27 Septemba 2019 jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo linawakutanisha wanaharakati wa haki za jinsia, wanasiasa na wadau mbalimbali hasa asasi za kiraia.
 
Ngoyai yupi mlio kuwa mnamporomoshea matusi kipindi amehamia upinzani?


Huyo huyo kwani Wewe mtoto wako akikengeuka utamchekea chekea!

Leo Warioba wakuzungumzia Uzalendo na mshikamano kwa mifano ya kuunga Unga ya wakati wa Jk kweli?

Ingekuwa wakati wa Jk leo ilikuwa siku ya kumuogesha Madongo Rais

Acheni Jk aanze kutoka Kitambi baada ya kustaafu maana Kamati za Roho mbaya zilikuwa live 24/7
 
Hujaeleweka bado
Huyo huyo kwani Wewe mtoto wako akikengeuka utamchekea chekea!

Leo Warioba wakuzungumzia Uzalendo na mshikamano kwa mifano ya kuunga Unga ya wakati wa Jk kweli?

Ingekuwa wakati wa Jk leo ilikuwa siku ya kumuogesha Madongo Rais

Acheni Jk aanze kutoka Kitambi baada ya kustaafu maana Kamati za Roho mbaya zilikuwa live 24/7
 
Back
Top Bottom