Taasisi ya Mwalimu Nyerere imeandaa mdahalo kuhusu kuzingatia mambo muhimu katika Katiba Inayopendekezwa. Huu ni mfululizo wa midahalo na majadiliano kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Mdahalo huu utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 20/12/2014, kuanzia saa 9:00 mchana mpaka saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Mwanza.
Washiriki katika mdahalo huu ni pamoja na baadhi ya wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiwemo Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume; wengine ni waliokuwa makamishina wa Tume ambao ni Ndugu Joseph Butiku, Prof. Mwesiga Baregu, Prof. Paramagamba Kabudi, Ndugu Humprey Polepole na Ndugu Ali Saleh kutoka Zanzibar. Vilevile wananchi na Viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika, vyama vya wafanyakazi, n.k. wanakaribishwa kushiriki.

Imetolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
16.12.2014
16.12.2014