Jaji Warioba kuendesha mdahalo wa katiba Mwanza, 20.12.2014 ukumbi wa Gold Crest saa 9 jioni

Kiokote

Member
Nov 9, 2010
64
95
Taasisi ya Mwalimu Nyerere imeandaa mdahalo kuhusu kuzingatia mambo muhimu katika Katiba Inayopendekezwa. Huu ni mfululizo wa midahalo na majadiliano kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Mdahalo huu utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 20/12/2014, kuanzia saa 9:00 mchana mpaka saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Mwanza.

Washiriki katika mdahalo huu ni pamoja na baadhi ya wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiwemo Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume; wengine ni waliokuwa makamishina wa Tume ambao ni Ndugu Joseph Butiku, Prof. Mwesiga Baregu, Prof. Paramagamba Kabudi, Ndugu Humprey Polepole na Ndugu Ali Saleh kutoka Zanzibar. Vilevile wananchi na Viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika, vyama vya wafanyakazi, n.k. wanakaribishwa kushiriki.


Imetolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
16.12.2014
 

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,689
2,000
Kama kawaida mzee wetu wa CCM halisi wewe sio CCM maslahi. Safari hii waovu watakosa pakupumulia.
 

PUNJE

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
354
250
..Ni jambo jema hilo. Walio na nafasi kwa siku hiyo tafadhali ni vema kushiriki.
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,044
2,000
kama ni jumamosi i will do all my best niende hapo kuona live
Paul Makonda usijaribu kutia mguu hapo!
 
Last edited by a moderator:

mjinga

JF-Expert Member
May 11, 2008
328
195
Yaani huu moto unapelekwa kalibu na nyumbani kwa alieandika rasimu ya Sitta!!!lazima presha impate mzee wa vijisenti na mzee Sitta
 

YAGHAMBA

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
539
250
Hii kitu ilifaa ifanyike viwanja vya wazi kama pale Furahisha, Magomeni n.k, ili watu wengi na wa tabaka mbalimbali waweze kupata ujumbe huu muhimu. Hat hivyo naamini ITV na Radio One wataendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka ukumbini ili ujumbe uwafikie watu wengi zaidi.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Ila itabidi Taasisi hiyo ya Mwalimu Nyerere iweke mabouncer getini, kwa maana ya kuwa mabouncer hao wahakikishe wakimuona tu Makonda, wamshughulikie na kumchapa na kumgalagaza kwa staili ile ile ya Ukawa namna walivyolichapa kisawa sawa na kuligaragaza, lichama lake la Mafisadi, aka lichama la Mapingamizi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa za wiki iliyopita!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom