Jaji Warioba: Kubadili sheria nyingi katika kila Bunge kunaonesha kuna umuhimu wa Katiba Mpya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Jaji Warioba akiwa katika kipindi cha Dakika 45 ITV amesema suala la kubadili sheria nyingi katika kila bunge zinaonesha umuhimu wa Katiba Mpya.

Hata hivyo amesema ni muhimu kuwa waangalifu kwa kuwa Katiba Mpya haitaweza kutatua matatizo yote.

Ametolea mfano kuwa tunaweza kuwa na Tume nzuri ya Uchaguzi lakini bila kuwa na demokrasia katika vyama changamoto hazitakuwa zimetatuliwa.
 
Warioba....katiba mpya Ni muhimu
Werema ...katiba mpya ni muhimu
Diallo.........miwka 5 tumepita kwenye giza kinene. Tulichagua mtu aliyekuwa na faili Milembe.

Kama hawa wazee wamesema haya wewe mwanaccm msafisha viatu huko kwa Mtogole na Nanjilinji ni nani hadi upinge katiba mpya??
 
Katiba mpya isio na kona kona ni muhimu, lakini na hao watawala waanze kujifunza kuheshimu katiba. Sio katiba mpya kesho wanaanza kuichokonoa na kuitia viraka ili ikidhi matakwa yao binafsi.

Unafiki, uroho, fitina, uwongo, kiburi, ulinbukeni, bora mimi na majungu ndio tatizo la nchi yetu.
 
Warioba kaongea vizuri sana tena bila ushabiki, kawaeleza ukweli wanasiasa wote wa upinzani na chama tawala

1. Kawashangaa wanasema eti katiba siyo kipaumbele

2. Kasema ile rasimu yake ni maoni ya wananchi siyo rasimu yake

3. Kasema kuna mambo ya msingi wananchi waluraka yawemo mle kama vile tunu za taifa, maadili ya viongozi

4. Kasema kuwa katiba pendekezwa ile ya Chenge ina kipengele kinachosema eti Wazanzibar shurti wabadili katiba yao iendane na katiba hiyo ya Chenge, kasema hilo halitowezekana, maana katina ya Zanzibar kuna mambo mle hayawezi kubadilika mpaka maoni ya wazanzibar, Sasa huwezi kuwaconvince wazanzibar kubadili katiba yao ili kuendana na takwa hilo la katiba ya Chenge. Kasema hata kufanya hivyo kutamdistabilize rais Mwinyi ambaye sasa hivi anangoza nchi iliyotulia vizuri.

5. Warioba kamtaka rais Samia akutane na wapinzani wazungunze namna gani ya kuaporoach suala hili la katiba, mathalani kwa mfano kupitia hayo mazungumzo waone kama wanaibadili yote at once au gradually na timeframe ipi Yaani ilimradi mazungumzo yafanyike

6. Warioba kasema kuwa mtu anayepinga katiba mya huyo anapinga maoni ya wananchi

7. Warioba anasema suala la katiba mpya ni suala la kisheria, ipo sheria inayo-govern hilo suala.

8. Warioba pia amewapiga konzi wapinzani, wasiigeuze suala ka katiba mpya kama suala la kisiasa tu la kudai kwa nguvu mambo ya kuwawezesha kuingia madarakani kama vile tume huru ya uchaguzi huku wakiyapa kisogo mambo mengine ya wananchi ambayo waliyaona muhimu sana kipindi cha kukusanya maoni.
 
Warioba....katiba mpya Ni muhimu
Werema ...katiba mpya ni muhimu
Diallo.........miwka 5 tumepita kwenye giza kinene. Tulichagua mtu aliyekuwa na faili Milembe.

Kama hawa wazee wamesema haya wewe mwanaccm msafisha viatu huko kwa Mtogole na Nanjilinji ni nani hadi upinge katiba mpya??
Hao waliosema hivyo wengine hawana tena nafasi na wanajiona hawaongelewi kwenye mchango wowote wa hili taifa.

Sasa hivi watu wapya kabisaa kwa asilimia 85 ndani ya chama na wana mitizamo tofauti na hao wazee.
 
Hivi huyu mzee nikweli hua anavuta sigara

Inawezekana akiwa anavuta hukumbuka mengi

Toka namfahamu sijawahi msikia kaongea kitu akajikwaa

Moja yamawaziri wakuu wastaafu mungu mpesana muda mrefu hapa duniani

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Hao waliosema hivyo wengine hawana tena nafasi na wanajiona hawaongelewi kwenye mchango wowote wa hili taifa.

Sasa hivi watu wapya kabisaa kwa asilimia 85 ndani ya chama na wana mitizamo tofauti na hao wazee.
Hao ndiyo wenye chama na ndiyo wenye maamuzi ndani ya chama. Hao 85% wanaweza kuwa ni akina "njoo tukae" halafu hiyo % iliyobakia ndiyo akina Warioba wenye sauti na maamuzi.
 
Hao waliosema hivyo wengine hawana tena nafasi na wanajiona hawaongelewi kwenye mchango wowote wa hili taifa.

Sasa hivi watu wapya kabisaa kwa asilimia 85 ndani ya chama na wana mitizamo tofauti na hao wazee.
Kesho
 
Warioba....katiba mpya Ni muhimu
Werema ...katiba mpya ni muhimu
Diallo.........miwka 5 tumepita kwenye giza kinene. Tulichagua mtu aliyekuwa na faili Milembe.

Kama hawa wazee wamesema haya wewe mwanaccm msafisha viatu huko kwa Mtogole na Nanjilinji ni nani hadi upinge katiba mpya??

Rais Samia Suluhu Hassan katiba mpya msubiri kidogo
 
Wanaandaa ajali uko wapo busy kutafuta mbuzi wa kafara

Yaani bila katiba sijui ataongea nini Samia 2025

Ccm endeleeni kucheza tu 2025 hamtoamini kitakachowakuta
Kutakuwepo na Tume nyingine ya uchaguzi, ama hii hii iliyopo sasa hapo 2025?
 
Warioba kaongea vizuri sana tena bila ushabiki, kawaeleza ukweli wanasiasa wote wa upinzani na chama tawala
Mkuu 'Missile',
Inanibidi niwe 'personal'

Tukiacha ushabiki mwingine pembeni, unao uwezo mzuri sana wa uelewa wa mambo. Kisomo chako kimekupika vizuri katika eneo unalolisimamia.

Imenilazimu niandike haya, kwa sababu michango yako mingi, unapoamua kuweka ushabiki wa mambo mengine pembeni, inafurahisha sana kukusoma.
Unapotoa mhitasari wa taarifa, unaufanya uwe rahisi sana kuusoma na kamilifu.

Imenibidi leo nitoe ushuhuda huo, kwa sababu hiyo ni hazina kwa jukwaa hili la JF.
 
Back
Top Bottom