Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482

Jaji Joseph Warioba

Tume ya kuratibu maoni kwa ajili ya kuandika Katiba mpya inatarajia kuzindua zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi muda wowote kuanzia sasa.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na NIPASHE ofisini kwake.

"Maandalizi yote tumeishayakamilisha na muda wowote tutazindua zoezi rasmi la ukusanyaji wa maoni kama tulivyopanga na wananchi wasiwe na wasiwasi," alisema.

Alitaja baadhi ya vitu vilivyokamilika kuwa ni masula ya kisheria na pamoja na namna watakavyoanza kuendesha zoezi hilo.

"Wananchi wasiwe na wasiwasi, watulie muda wowote zoezi la kukusanya maoni litaanza na kila mmoja atapata fursa ya kushiriki," alisema Jaji Warioba.

Mwezi uliopita tume hiyo ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa ofisi huku Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akieleza kuwa itapewa zana za kisasa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ikiwemo magari na nyumba za kuishi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na tume hiyo baada ya kuikabidhi ofisi, Balozi Sefue alisema kuna mambo 10 ambayo serikali itayafanya kwa ikiwemo utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati alipoiapisha Tume hiyo Aprili 13, mwaka huu.

Akziungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, Jaji Warioba aliahidi kwamba watatumia uwezo wao wote kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata fursa ya kutoa maoni yao.

"Tutatumia uwezo wetu wote kutekeleza yote ambayo Watanzania wanayataka, tunakwenda kwa Watanzania watuambie wanataka Tanzania ya aina gani," alisema Jaji Warioba.

Rais Kikwete aliipa Tume miezi 18 kukamilisha kazi ya kukusanya maoni.


CHANZO: NIPASHE
(<a href="http://www.widgeo.net">widget</a>)
 
Hii nchi tumeshakuwa na viongozi wa ajabu kweli kweli.Celina Kombani kuongoza wizara ya sheria na katiba? Walikuwa wanafikiria nini?
 
Wezi tu hawa.

Mbona kazi hii sasa hivi inafanywa na viongozi wa Matawi ya CCM kwa kukusanya maoni ya Wanachama wa CCM na kuwalazimisha kujaza jinsi chama kinavyotaka iwe.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Back
Top Bottom