Jaji Warioba anena

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
Mzee Warioba, Nakuangalia mzee wangu ITV...

Mmmmmhhhhhh..........kaaaaaazi kweli kweli......itikadi ya vyama iendane na dira ya nchi......how do the Katiba enforce this? Freeman, Kinana, Jussa.... mnampata mzee??
 
Hizi sasa jaji Waryoba yupo kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa Itv.

Amewambia viongozi kuacha kuzungumzia masuala yanayohusu power na kuwaasa kujibu kero zinazowagusa wananchi moja kwa moja.

Kwa maelezo yake anasema maoni ya watu wengi yalijikita kuondoa matatizo yanayowakabili, elimu, umasikini, kuhusu gharama za serikali ya shirikisho la muungano anasema ni bora ziwepo kuliko kuvunjika kwake anasema hayo ndio maoni ya wananchi.

Kuhusu maadili ya viongozi anadai wananchi wengi wanataka hatua zichukuliwe ili kudhibiti maadili ya viongozi wao.
 
Naanza kuwa na imani na hii tume ya mabadiliko ya katiba. mwanzoni nilidhani kwa kuwa JK wa Bagamoyo ndio ameiteua kwa marupurupu makubwa nikadhani watanzania tumekwisha.

Prof. Baregu hongera pia, uliweka wazi kwamba utaifa mbele kuliko uchama.
 
Inaonekana kama msukumo mkubwa wa kuandaa katiba mpya umetokana na watanzania kukosa imani na CCM na serikali yake.

Warioba, watu wanataka watu wapya. wenye maadili maana yake CCM haiaminiki tena
 
Back
Top Bottom