Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,130
Akiwa mwalikwa kwenye kongamano la haki za binadamu lililoandaliwa kwa ajili ya viongozi wa dini, lililofanyika jijini Dar tarehe 14 mwezi huu, Jaji Warioba alizitaja kasoro kuu 4 zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu uliopita.
Alizitaja kasoro hizo kama ifuatavyo:-
1. Wagombea wengi wa upinzani kuenguliwa na Wasimamizi wa uchaguzi (maDED) pasipo sababu za msingi na Tume ya uchaguzi ya Taifa kujifanya kama hawaioni kasoro hiyo!
2. Mawakala wa vyama vya upinzani kuzuiliwa wasiingie kwenye vyumba vya kupigia kura.
3. Vyama vya siasa, hususani CCM kupuuza mapendekezo ya wajumbe waliyoyatoa kwenye kura za maoni kwenye majimbo yao na badala yake wao Kamati Kuu ya Chama kuwaletea watu "wao" ili wananchi hao wawapitishe bila ya kupingwa!
4. NEC kutosikiliza malalamiko ya wagombea wa uchaguzi, hususani wa vyama vya upinzani kwa wakati muafaka.
Alifafanua Waziri Mkuu huyo mstaafu Jaji Warioba kuwa chanzo cha kuvunjika amani katika nchi nyingi barani Afrika ni nchi hizo kupuuza Haki ya wananchi na kutoshughulikia kasoro kama hizo wakati wa chaguzi.
Akaendelea kusisitiza kuwa AMANI ni tunda la HAKI na mahali ambapo HAKI haipo ni vigumu sana kudumisha AMANI
Alisema kuwa nchi yetu inajivunia amani tuliyonayo ambayo tunapaswa kuienzi kwa kuondoa kasoro hizo za wazi kabisa zilizojitokeza kwenye uchaguzi uliopita
Jaji Warioba ni mmojawapo wa viongozi wastaafu wachache sana ambaye amediriki kuukosoa uchaguzi mkuu uliopita kwa namna ulivyoendeshwa
Swali langu ni kuwa, je viongozi wastaafu wengine hawakuziona kasoro hizo na kuamua kuwa "mabubu" bila kukemea kasoro hizo ambazo Jaji Warioba ametahadharisha kuwa kama zisipotafutiwa ufumbuzi wa haraka, basi zinaweza kutuondolea tunu hii adimu sana ya amani tuliyonayo kwenye nchi hii?
Au ndiyo tuseme kuwa viongozi wastaafu wengine pamoja na kuyaona hayo "madudu" ya uchaguzi wamejiamlia kujikakia kimya kwa kuogopa kuwa watakaripiwa na Jiwe na kuambiwa kuwa wanawashwawashwa?
Mungu ibariki Tanzania.