Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

Jussa anawakilisha kundi la mambumbu kapewa nafasi ya kutetea anachokita kashindwa,sehemu pekee inayomfaa Jussa ni uhamsho.
Huyu jamaa Jussa ni mbumbumbu wa kweli kweli, lakini Jaji Warioba kambana kiakili sana kwa kumtaka atoe mifano anayoifahamu juu ya muungano huo anaoutetea, naye kajikanyaga vya kutosha.
 
Akili ndogo Vs akili kubwa!
Jussa ataweza?
Mheshimiwa sana Jussa alifikiri yuko kwenye jukwaa la Wawakilishi, lakini hapa kagonga mwamba baada ya kukutana na wajumbe wa Tume ambao ni wanasheria waliobobea.
Kwa kifupi , huyu Bwana Jussa ameonyeshwa kuwa kisheria ni illiterate, na mambo ya kupiga domo mahali pa wasomi sio mahala pake.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mkongwe (Cuf), Ismail Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wake wa madaraka .

Jaji Warioba alichukua hatua hiyo baada ya Jussa kusimama na kutoa maoni ya kutaka mfumo wa Muungano wa mkataba, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikichukua maoni ya Wawakilishi mjini Zanzibar jana.

Alimtaka Jussa atoe mfano angalau mmoja au miwili ya uendeshaji wa serikali ya mkataba ili Tume yake ipate ufahamu katika mapendekezo yake.
Jussa alisema anayo mifano zaidi ya 100 lakini akadai wakati ukifika serikali zinazohusika zitakaa na kuja na fomula ya mgawanyo huo pamoja na uendeshaji wake kimadaraka.

Hata hivyo, Jaji Warioba kwa upande wake akionekana kutoridhika na maelezo hayo ya Jussa alimtaka kuiambia Tume alivyojiandaa na Muungano wa mkataba kinyume na mfumo dola uliopo.

"Bwana Mwakilishi hebu tupe lau mfano mmoja au muundo wa uendeshaji wa Muungano wa serikali ya mkataba ili uweze kukidhi haja yako na kutuonyesha njia" alisema Jaji Warioba.

"Hebu tuweke wazi juu ya utashi wa mpango unaofikirika wa kuwa wa serikali ya mkataba, nafikiri unachokusudia ni kutaka kuvunja Muungano uliopo" alisema Warioba.

Hata hivyo, Jussa alibaki katika msimamo wake huku akisisitiza kuhusu kukaa kwa serikali mbili na kutoa mfumo wa uendeshaji wa serikali ya mktaba.

Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano kwa kuwa kila upande utalazimika kuwa na kiti Umoja wa Mataifa (UN).

"Tanganyika na Zanzibar zikiwa kila moja ina mamlaka yake hakutakuwa na neno Muungano, ndiyo maana nasema nisaidiwe juu ya kupata mfumo wa kuendesha Muungano unaotakiwa chini ya mkataba" alisema Jaji Warioba.

Akiwekea mkazo katika hoja iliyotolewa na Jaji Warioba, mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo, Paramagamba Kabudi, alisema inasikitisha kuona hadi sasa wanaotaka Muungano wa mkataba wanashindwa kutoa rasimu ya mfano wa serikali ya mkataba ili kuisaidia Tume juu ya kile wanachokitetea.

Wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF waligawanyika pande mbili huku wale wa CCM wakitetea mfumo wa serikali mbili na wa CUF wakitaka Muungano wa mkataba.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha alisema muundo wa Muungano wa serikali mbili ndiyo muafaka kwa kuwa umeonyesha faida katika masuala ya ulinzi na usalama lakini pia ukijenga umoja wa kitaifa.

Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

Aidha alitaka nafasi ya Rais wa Muungano itolewe kwa zamu kila upande uwe na kipindi cha miaka kumi.
"Mgawanyo wa mapato usiangalie idadi ya watu kwa vile hata kama Serikali moja ikiwa na watu wawili bado ina jukumu la kuwapatia maisha bora na huduma wananchi wake" alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Said Ali Mbarouk alisema mfumo wa sasa wa Muungano una matatizo kwakuwa kuna mambo ambayo si ya Muungano lakini yanasimamiwa na Muungano kinyume na makubaliano ya mwaka 1964.
Aliyataja baadhi ya mambo aliyodai yanayoleta mkanganyiko kuwa ni utalii, maliasili, habari na michezo ambayo alisema yanahitaji kuwekewa utaratibu na kuzungumziwa kwake katika medani za kimatifa.

Waziri asie na Wizara Maalum Machano Othman Said alitaka mfumo wa Muungano wa sasa uendelee na kutaka Rais wa Zanzibar kubaki kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza alitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka sawa na Rais wa Muungano pamoja na Zanzibar kupata nafasi ya kujiunga na jumuiya ya OIC na nyingine za kiuchumi duniani.

Tume ya mchakato wa ukusanyaji wa maoni inayoongozwa na Jaji Warioba ipo visiwani Zanzibar na tayari imekutana na wananchi katika mikoa ya Kaskazini Unguja na Pemba.


Sosi: Mzalendo.net

Nakala kwa Barubaru, Tume ya Katiba, awadh, Mzee Mwanakijiji, chama, TUMBIRI
Bila kuwasahau Ritz na zomba maana hawa popote uislam unapovuma wao huwa tayar kutetea kwa Gharama yeyote
 
Last edited by a moderator:
Kama moja ya vinara wa serikali huru ya JWZ na muungano wa mkataba (Jussa) anashindwa hata kutoa mfano mmoja wa muungano wa mkataba je itakuwaje kwa maelfu ya wafuasi wake anaowasadikisha suala hili?

Kuna wakati huwa napata wasiwasi kama Waznz know exactly what they want AND how to get it. Tulishawahi kuwasaidia hapa hadi road map ya jinsi ya kufanikisha hilo lakini wapi. Sasa kwa majibu haya ya Jussa napata mashaka kama kweli hizi sio kelele za bata tu na mwisho wa siku, no any action.

Mimi mara zote nimeunga mkono harakati za waznz kuwa huru nje ya muungano wa sasa kwa kuwa sijawahi kuona faida yeyote kubwa ya maana ambayo Tanganyika (Bara) wanapata kwenye huu muungano wa sasa zaidi ya lawama, kejeli na matusi.
 
Hii makala imeandikwa na Mwinyi Saddallah mtu ambaye siku zote anakua anapindisha kalamu yake pale habari inapohusu masilahi ya Zanzibar. Kwa sisi tuliokuwemo ndani ya Baraza na kuwashuhudia Wawakilishi jinsi walivyokua wakitoa michango yao tunawaona NYOTE ambao munachaongia mada hii ni dhaìri kumbe HAMUJUI MUNACHOKIHUBIRIA!
Utafanya jambo zuri kama utatuwekea habari ya yaliyojiri kama unaona kauli za Mwinyi Saddallah zimepotosha kile kilichotokea au kilichosemwa.

Vipi Mwinyi Saddallah amepindisha kalamu katika hili linaloongelewa katika thread hii?

Kama unayo clip ya mkusanyiko/mkutano huo, iweke hapa au sawazisha upotoshaji wa Mwinyi Saddallah.

Hapa zinapatikana picha tu za tukio. Link tumeyawariobawawakilishi
 
nafikiri ingekuwa busara sana kuweka mjadala maalum wa wazi ikiwezekana kwenye TV na Radio kati ya JUSSA na Warioba mtajua uwezo mkubwa wa Jussa dhidi ya Warioba.

Issue sio UWEZO; Issue ni NCHI GANI yenye MUUNGANO wa MKATABA? JUSSA, anachotakiwa kufanya ni kutaja hizo NCHI... Na sio kutafuta ni nani MWENYE HOJA MURUA au MWENYE KIPAJI...

The question was in a Simplicity and Very Simple... TAJA HIZO NCHI...
 

NA ANGALIA PICHA ZAO WAKIJARIBU KUTOA MAONI YAO; JUSA NI WA MWISHO KWENYE HIZO PICHA...

[h=3]WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATOA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA[/h]

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliotishwa na Tume hiyo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kutoka kulia ni Wajumbe wa Tume hiyo, Profesa Paramagamba Kabudi, Suleiman Ali, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ali Abdalla Ali, Mjumbe wa Tume Joseph Butiku, Katibu wa Tume Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki.


Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar , ambapo wajumbe hao walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.


Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha , akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe wa Baraza hilo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.


Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Asha Bakari Makame akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.


Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk, akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Kwa picha zaidi Bofya read more


Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na Mjumbe wa Tume Joseph Butiku.


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kushoto), kuwaaga wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar jana jumapili tarehe 14. Otoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.


Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jussa Ladhu akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya. (FULL SHANGWE)


at 7:40 AM
 
Human psychology ilivyo ni kwamba mtu akihadithia tukio halafu akakupa maoni yake kuhusu tukio na kutetea baadhi ya wahusika wa tukio mara nyingi hadithi yake itakuwa imepakwa rangi ya kujengea hoja yake. Hususan kama ni yeye peke yake aliyekuwepo.

Hii ni one-sided story ambayo mleta hoja nae ana lake, na katika sisi wote hapa so far, ni yeye peke yake alikuwepo, inawezekana ni hadithi yenye uongo mtupu!
 
Swali la Jaji Warioba kwa Jussa na wajinga wenzake kamwe hawana uwezo wa kulijibu Barubaru ebu wasaidie CUF wamepewa nasi ya kutetea hoja zao wameshindwa mbele ya tume sasa tuwasaidie nini ?.
Ngongo tunashukuru sana Jaji Warioba kutusoma. Nimeliuliza swali hili mara 100 hapa JF hakuna anayekuja na majibu.
Sasa msikilize mpuuzi na Juha Jusa anasema wakati ukifika atasema, yaani tukubali tu kitu tusichokijua.Nasema kila siku mwisho wa upuuzi Chumbe, mwisho wa serikali 3 chumbe, mwisho wa ujinga Chumbe.
Mwisho wa kubeba watu Rais-kilomoni.

Here we go! Almaarufu Baru baru, Mstahiki Nonda, Muungwana Takashi, think tank ya ZNZ akina Jusa, Ahmed na Maalim hawana jibu. Je ninyi mnalolote mtuambie
 
Wazanzibari tunaposema tunataka Muungano wa mkataba tuna maana ya kwamba Muungano uvunjike hatuutaki, tumeamua kutumia neno MKATABA baada ya Raisi wenu Kuweka kipengele kinachokataza kabisa kuhusu kuzungumzia kuvunjika kwa Muungano. Tumeamua kuukataa Muungano kwa kutumia njia hii sababu sisi ni wajanja wa kutumia mbinu katika michakato. Na katika hili kila mwenye akili za kuchambua mambo ndiye anaweza KUFAHAMU. Ngoma ipigwavyo ndivyo tuichezavyo!
 
Kama una muda wa kutosha na kama unataka kuelewa juu ya ubadilishaji/marekebisho ya katiba au/katiba mpya/ katiba uitakayo pitia hili chapisho. katibampya

Utakutana na vitu ambavyo hutaweza kuamini kama hiki (nimeweka rangi nyekundu).

Tanzania ni Jamhuri ya Muungano. Ni Muungano wa nchi mbili (Tanganyika naZanzibar) ambazo kabla ya Muungano huo zilikuwa huru na zenye mamlaka kamili. Vile vile nchi hizi zilikuwa na zinaendelea kuwa na historia mfumo wa Katiba ulio tofauti lakini unaingiliana. Katika kuelekea kwenye kutayarisha Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano suala hili ni lazima liwekwe wazi na lijadiliwe kikamilifu.

Hii ni kwa sababu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunazo Katiba mbili na siyo moja. Hizi ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984. Katika hali isiyo ya kawaida, Katiba hizi mbili zina hadhi sawa
kutegemea pale zinapohusika. Hakuna iliyo na nguvu au uwezo kuliko nyingine. Hali hii inaufanya mjadala wa Katiba uwe mpana na uwe wa kuangalia kwa makini sana. uk2-3 link mwongozo
 
Jusa ni kipofu na kiziwi, kwani haelewi Tanzania ndiyo iliyomfanya jusa kukaa nzanzbar, jusa ikirudi Tanganyika utakuwa upande wa unguja au pemba? usilete siasa za majitaka kwenye masuala ya muungano
 
Human psychology ilivyo ni kwamba mtu akihadithia tukio halafu akakupa maoni yake kuhusu tukio na kutetea baadhi ya wahusika wa tukio mara nyingi hadithi yake itakuwa imepakwa rangi ya kujengea hoja yake. Hususan kama ni yeye peke yake aliyekuwepo.

Hii ni one-sided story ambayo mleta hoja nae ana lake, na katika sisi wote hapa so far, ni yeye peke yake alikuwepo, inawezekana ni hadithi yenye uongo mtupu!

Mkuu hii si hadithi, ni tukio la kweli.
Tukio lenyewe ni mkutano wa kutoa maoni mbele ya Tume ya kukusanya maoni ya kubadili katiba ya nchi au kuboresha iliyopo.
Hii si taarifa ya kutunga au oungo, kwa shilingi mia tano tu, waweza kupata stori yote kutoka gazeti la Nipashe toleo la leo 15/10/2012.

Baada ya hapo sasa usikie maoni yangu:
Jussa is a loud mouth who has just exposed himself kwa kukosa uelewa unaohitajika, sasa kwa maoni yangu I am at loss kuwa hao anaowawakilisha, je wanajua kama hajui kitu?
 
Jussa ni mpayukaji na mganja njaa huyo.

Kwanza wengine wetu hatutaki tena muungano wa aina yoyote nao. Wapewe Zenj yao wale jeuri yao, tunawelea sana hawa jamaa
 
Jussa anasema ana mifano 100 lakini anashindwa kutaja hata mfano mmoja! Na anaposema ana mifano 100 ya muungano wa mkataba maana yake ni kwamba kuna nchi 100 zilizoungana (mikataba tofuati tofauti). Muungano ya mkataba 100! Sayari ipi? Na anategemea watu wamchukulie serious anapoongea muungano wa mkataba?

Yote tisa, kumi ni huu mzaha anaosema (Jussa) kuwa wakati ukifika ndio atasema Muungano uwe vipi! Anataka watu wazima wakae chini na ku-sign mkataba kabla ya KUJUA ni kitu gani kiwe kwenye mkataba. ah!

Nirudi kwa Shamsa Vuai.
Yeye anasema urais uwe wa kupokezana kila baada ya miaka 10. Huu ni upuuzi na sitotaka kupoteza muda kuujadili.

Point yake ya pili Shamsa Vuai ni kugawa rasilimali sawa bila ya kuangalia idadi ya watu. Kwa maana hiyo anasema Tanzania bara na Zanzibar wagawane sawa kwa sawa. Sina shida na hilo as long as litaendana na kila upande kuchangia gharama sawa kwa sawa. Kwa miaka 48 Tanganyika ndiyo ingharamia wizara ya mambo ya ndani (police wote), Wizara ya mambo za nchi za nje, Jeshi n.k. Huo usawa anaoongelea Shamsa uanzie kwenye gharama.
 
Mkuu hii si hadithi, ni tukio la kweli.
Tukio lenyewe ni mkutano wa kutoa maoni mbele ya Tume ya kukusanya maoni ya kubadili katiba ya nchi au kuboresha iliyopo.

Mkuu
Ungeweka makala yote, ambayo itamwacha mtu kujitafsiria vile apendavyo.

Makala hii link Home

Baada ya kuisoma makala hii. Jussa anasema ukifika wakati mwafaka serikali zitakaa na kuamua vipi zigawane madaraka. Inaonekana una msimamo wako kuhusu Jussa na umepata nafasi ya kumpiga madongo.

Alichosema Jussa ni kuwa "kesi iko mahakamani, hapaswi kuizungmzia" lol.
 
Natanguliza msimamo wangu (Declare interest).

1. SIUTAKI MUUNGANO WA SASA KWA SABABU NI WA WATU WAWILI NYERERE NA KARUME PAMOJA NA SERIKALI ZA SIKU HIYO.

2. KUIUWA TANGANYIKA KIMAGUMASHI NI KOSA NA NI ZIMWI LITAKALOPASUA CHUPA ILIYOLIFUNGIA

Nataka muungano unaokidhi matakwa ya wananchi. Uwe muungano wa dola mbili Tanganyika na Zanzibar siyo Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu hapajakuwepo dola inayoitwa Tanzania bara iliyoungana na Zanzibar

Mh. Warioba anasimamia hoja ya ulazima wa kuwepo muungano bila kujiuliza uhalali na uhalisi wa muungano kwa matakwa na maslahi ya wananchi wa pande mbili.

Jussa anaweza kuwa mbumbumbu kwa mtazamo wa wanaoulazimisha muungano. Hoja yake na hisia zake zinatuwakilisha wengi mimi nikiwa Mtanganyika. Kama mwana sheria jaji Warioba mvivu wa kutafsiri na kudadavua maana ya muungano wa mkataba. Anadai mifano ya miungano ya mkataba dunia mbona hatoi mfano wa muungano wa sasa tulio nao kama upo duniani?

Ni jukumu lake kuchukua maoni ya wananchi, si kutetea status quo.

Nakusahihisha usijumuishe waTanzania wote na hoja za watawala. Mimi najuta kuwa kwenye muungano huu na naumizwa sana na fikra za kipuuzi za watawala na wakala wao kwenye hili suala. Sababu ni moja tu sijaona manufaa yake zaidi ya matatizo, wala sioni tunakoelekea kuna heri.
Nakugongea like brother u truely great thinker
 
Back
Top Bottom