Jaji wa Marekani Aliyewalawiti Wafungwa Kufungwa Maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji wa Marekani Aliyewalawiti Wafungwa Kufungwa Maisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 11, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Jaji Herman Thomas, jaji ambaye alikuwa akiheshimika sana kiasi cha kwamba alikuwa akitabiriwa kuwa jaji mkuu wa kwanza mweusi wa Alabama Kusini, huenda akahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwalawiti wafungwa wanaume ili awapunguzie adhabu zao.

  Jaji Thomas anakabiliwa na tuhuma za makosa 78 ya kukiuka misingi ya kutoa haki, kulawiti wafungwa, kuwateka wafungwa na kuwashambulia waliokataa kulawitiwa.

  Jaji huyo mwenye umri wa miaka 48, alijitetea kwamba hakufanya kitendo hicho na kwamba alikuwa akikutana na wafungwa ili kuwapa miongozo bora.

  Wakili wa jaji huyo alidai kwamba mteja wake amebabimbikiwa kesi hiyo na wafungwa ili kumchafulia jina lake kwa kazi nzuri ya ujaji aliyoifanya kwa miaka 20.

  Jaji Thomas na wakili wake walidai kwamba kesi aliyofunguliwa ni njama za wanasiasa ambao hawapendi mafanikio yake.

  Lakini mahakama iliambiwa kwamba Jaji Thomas alianza kufuatiliwa mienendo yake baada ya kuibadilisha hukumu ya binamu yake mwaka 2006 ingawa hukumu ya kesi hiyo ilikuwa imetolewa na jaji mwingine.

  Mahakama iliambiwa pia kwamba jaji Thomas alizichukua kesi walizopewa majaji wengine bila ya kufuata taratibu husika.


  Baadhi ya wafungwa wanaume walielezea jinsi walivyotolewa jela na kupelekwa kukutana na Thomas kwenye gari lake au ofisini kwake.

  Awali kulikuwa na taarifa za wafungwa kuvuliwa nguo zao za ndani na kisha kuchapwa bakora halafu ndipo zilipojitokeza taarifa za kulawitiwa kwa wafungwa na wafungwa wengine kulazimishwa wajipigishe punyeto mbele yake.

  Wafungwa wote waliolawitiwa na jaji huyo walikuwa ni wafungwa weusi hakukuwa na mfungwa mzungu kati yao.

  Alama za bakora kwenye ****** ya baadhi ya wafungwa na pia alama ya majimaji ya mbegu za kiume za mfungwa aliyelazimishwa apige punyeto kwenye zulia la ofisi ya jaji huyo ni miongoni mwa vielelezo vya ushahidi dhidi ya jaji huyo.

  Wafungwa waliotoa ushahidi waliweza kuelezea vizuri kabisa jinsi ilivyo ofisi ya jaji huyo ambayo haina madirisha.

  Thomas alijiuzulu nafasi yake mwaka 2007 baada ya tuhuma za wafungwa kuchapwa bakora kwenye makalio yao kusambaa.

  Waendesha mashtaka walisema kwamba kuna wafungwa 15 wapya na wa zamani ambao wako tayari kutoa ushahidi wa kulawitiwa na jaji huyo.

  Ushahidi huo utachukua wiki kadhaa na jaji Thomas huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu Jaji hana akili
  kwanini asitafute mashoga wenzake.

  Jaji shoga huyu apewe kifungo cha maisha
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Darwin angekuwa tanzania ningemtupa jela ya pemba akawaone vidume wenzake
   
 4. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pemba cha mtoto,jela za uarabuni safi sana kwake huyu jaji.
   
Loading...