Jaji Samatta: Rais hana kinga kwa mambo aliyoyafanya akiwa Rais bali yale aliyoyafanya kama Rais

RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
Mkuu Salary Slip, asante kwa bandiko hili. Naunga mkono hoja

.Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu - JamiiForums

P
 
Kumbe ndio maana kajaza wasukuma ili asishitakiwe kwa uovu wake
Mkuu Gulwa kwanza sii kweli kuwa kajaza Wasukuma, bali kwa vile ndio walio wengi, tukifuata haki bin haki, walio wengi lazima tuu watakuwa wengi kwenye kila sehemu.

Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi! - JamiiForums

Pili kweli ni muovu
Na Tatu, kwa vile hakuna mstaafu aliyewahi kushitakiwa, then sii kweli amewajaza ili asishitakiwe.

NB. Ikitokea ni kweli wamejaa, then, wamejaa kwa uwingi wao which is their deserving positions.
Hili la kutokushitakiwa unaweza kufanya rejea hapa
Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu - JamiiForums
P.
 
"Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais"
Hapa sijapaelewa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Papushikashi,
Kuna mambo ambayo rais anapaswa kuyafanya kama rais, yaani zile presidential powers, duties and responsibilities, kama kuteua, kusaini sheria, kusaini hati za adhabu ya kunyongwa etc, mfano rais kasaini death warrant, mtu akanyongwa, baadae muuaji halisi akajitokeza, rais anakuwa hana kosa. Hivyo kinga ya rais kutokushitakiwa, inahusu utekelezaji wa majukumu yake tuu ya urais.

Kinga hiyo pia inahusu kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda, kutumia fedha za umma bila kuidhinishwa na Bunge na makosa mengine ya kiutendaji.

Lakini rais akiwa Ikulu, anaweza kufanya mambo mengine ya ajabu ajabu mfano akaamua kuiba wake za watu, au kupiga madili ya kifisadi, au kuamuru watu wapigwe risasi, wapotezwe etc, yale sio majukumu ya urais, anashitakika

Hili niliwahi kulizungumza hapa na nimekuwekea hadi kifungu cha katiba

Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu - JamiiForums
P
 
Mmenikumbusha December 2015 tulipotangaziwa hakuna sherehe za uhuru, watu wafanye usafi. Nakumbuka kumwambia jamaa yangu, kama jambo hili linaweza kupita kirahisi hivi, mtegemee mambo makubwa huko mbeleni. Kwa nchi yoyote, kumbukumbu ya uhuru wa nchi siyo ya kuchezea kirahisi.

Tatatibu za kushehekea zinaweza kubadilika ila zinapaswa kufanyika kwa utaratibu unaoeleweka.

Personally, siyo mpenzi sana wa magwaride lakini inawezekana bado ni muhimu kama sshemu ya sherehe za uhuru ila badala ya kukagua Uwanja wa Taifa kwenye shughuli inayosemekana ilikuwa inakula hela nyingi, Rais anaweza kwenda kukagulia kwenye kambi ya jeshi kuokoa gharama. Hilo linafanyika huku shughuli nyingine za kuadhimisha uhuru kwa ngazi mbalimbali za kijamii zikiendelea, mfamo midahalo, hadithi na simulizi mbalimbali, nk.

Kuna mtu ameongelea 'emergency'. Kulikuwa na cases mbili tatu za kipindupindu wakati ule ndiyo wakatumia kama 'a matter of fact', ila haikuwa na uzito wa kisheria. Siku yoyote usafi unaweza kufanyika, kwa nini ni iwe siku ya uhuru? Na hakukuwa na issued official emergency statement kujustify uamuzi mkubwa kama ule.

Ile ilitoa mwanya mkubwa sana kuliko wengi mnavyodhani. Naamini mengi yaliyofuata na yanayoendelea hata leo yalianzia pale.

Tunachohitaji ni mifano hai badala ya kubaki na nadharia tu. Wakipelekwa wawili watatu, wakahenyeshwa na kutolewa jasho kidogo, hata wakija kuchomoa itasaidia kiasi fulani huko mbeleni.
 
Mkuu Papushikashi,
Kuna mambo ambayo rais anapaswa kuyafanya kama rais, yaani zile presidential powers, duties and responsibilities, kama kuteua, kusaini sheria, kusaini hati za adhabu ya kunyongwa etc, mfano rais kasaini death warrant, mtu akanyongwa, baadae muuaji halisi akajitokeza, rais anakuwa hana kosa. Hivyo kinga ya rais kutokushitakiwa, inahusu utekelezaji wa majukumu yake tuu ya urais.

Kinga hiyo pia inahusu kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda, kutumia fedha za umma bila kuidhinishwa na Bunge na makosa mengine ya kiutendaji.

Lakini rais akiwa Ikulu, anaweza kufanya mambo mengine ya ajabu ajabu mfano akaamua kuiba wake za watu, au kupiga madili ya kifisadi, au kuamuru watu wapigwe risasi, wapotezwe etc, yale sio majukumu ya urais, anashitakika

Hili niliwahi kulizungumza hapa na nimekuwekea hadi kifungu cha katiba

Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu - JamiiForums
P
Shukrani mkuu
Nimekuelewa sana na ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Gulwa kwanza sii kweli kuwa kajaza Wasukuma, bali kwa vile ndio walio wengi, tukifuata haki bin haki, walio wengi lazima tuu watakuwa wengi kwenye kila sehemu.

Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye Ukabila, Tatizo Ndio Walio Wengi! - JamiiForums

Pili kweli ni muovu
Na Tatu, kwa vile hakuna mstaafu aliyewahi kushitakiwa, then sii kweli amewajaza ili asishitakiwe.

NB. Ikitokea ni kweli wamejaa, then, wamejaa kwa uwingi wao which is their deserving positions.
Hili la kutokushitakiwa unaweza kufanya rejea hapa
Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu - JamiiForums
P.
Najua msimamo wako unatokana na nini, hivi tukienda vyuoni tutakuta wanafunzi wasukuma ni wengi kuliko wote kila idara? jeshini je nk. Kumbuka jiwe sio msukuma ila anawapendelea kwa sababu ukaribu wa kihistoria. Ukweli ni kama nuru haifichiki
 
Mkuu Gulwa, kiukweli wakoloni wametufanya mbaya, wameleta maendekeo makubwa maeneo yenye mazao ya biashara ya pesa ndefu, na maeneo mengine kutelekezwa.

Maeneo ya Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya kwenye zao la Kahawa kulijengwa mashule hivyo Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa, wamesoma sana. Wasukuma ni miongoni mwa makabila ya wakulima na wafugaji, waliosoma ni wale waliolima zao la pamba, wafugaji wengi ni masikini wa kutupa, na wametapakaa nchi nzima.

Kufuatia wengi kutokusoma sana, huu wingi wao is not equally represented kwenye higher learning institutions, lakini tukija kwenye aggregate, Wasukuma bado ndio wengi zaidi, estimates, kati ya watu milioni 60 wa makabila 120 ya Tanzania, Wasukuma ni milioni 20, that is 1/3rd ya Watanzania wote, hivyo kwenye kila nafasi 3 za kila kitu, kulipaswa kuwe na Msukuma 1, halafu nafasi 2 zilizobakia ndizo makabila 119 yaliyobakia yagawane.

Hivyo mkiwaona wengi wengi wanateuliwa, sio ukabila ni just a deserving proportionalities.

P
 
Kenya tayari wana Katiba Mpya lakin Matatizo hayajaisha

Kabla ya uhuru Kila kitu walikuwa wanasema ndio sababu tunataka uhuru wakadhan Kila kitu kitakuwa solved kwa kupata uhuru

Tupunguze Kuwa Na 'over expectations'
Nimeikubali sanaaaa michango yako kwenye hii thread Mkuu
 
Mkuu Papushikashi,
Kuna mambo ambayo rais anapaswa kuyafanya kama rais, yaani zile presidential powers, duties and responsibilities, kama kuteua, kusaini sheria, kusaini hati za adhabu ya kunyongwa etc, mfano rais kasaini death warrant, mtu akanyongwa, baadae muuaji halisi akajitokeza, rais anakuwa hana kosa. Hivyo kinga ya rais kutokushitakiwa, inahusu utekelezaji wa majukumu yake tuu ya urais.

Kinga hiyo pia inahusu kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda, kutumia fedha za umma bila kuidhinishwa na Bunge na makosa mengine ya kiutendaji.

Lakini rais akiwa Ikulu, anaweza kufanya mambo mengine ya ajabu ajabu mfano akaamua kuiba wake za watu, au kupiga madili ya kifisadi, au kuamuru watu wapigwe risasi, wapotezwe etc, yale sio majukumu ya urais, anashitakika

Hili niliwahi kulizungumza hapa na nimekuwekea hadi kifungu cha katiba

Je, wajua kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa? Kinga ya kutoshitakiwa haihusu Rais kufanya biashara Ikulu - JamiiForums
P
Mkuu Pascali Wasukuma wanaweza kuwa ni wengi sawa, lakini kwa miaka mingi wamekuwa ni wachunga ng'ombe, hivyo kutokuwa wengi kwenye vyuo vya elimu ya juu. Kwa hiyo ikitokea leo wawe wengi kwenye teuzi Utakuwa ni upendeleo wa dhahiri. Kumbuka Mikoa ya Usukuma ni miongoni mwa Mikoa inayofanya vibaya katika mitihani ya kitaifa kwa miaka mingi plus Mikoa ya Pwani
Pili, kuvunja Katiba ni sehemu ya shughuli za urais au nimekuelewa vibaya, maana umesema hawezi kushtakiwa akivunja Katiba!
 
Mkuu Zakaria, kutokufanya vizuri Wasukuma, ni kutokana na ufugaji na kutotulia, lakini kutofanya vizuri mikoa ya Pwani, Singida, Dodoma na mikoa ya Kusini ni kutokana na lishe duni inayosababishwa na umasikini uliotopea, kitu cha ajabu kwa mikoa ya Pwani na Zanzibar, kuna bahari na samaki ndio mboga kuu, na ndio lishe inayoongoza kwa vitamin ya Omega3, responsible kwa brain power.

Kwa vile Wasukuma ndio wengi, hawakujaa kwenye teuzi zilizopita kutokana na being disregarded, hivyo tukawa na a big pool ya reserve ya wasomi wa Kisukuma wenye sifa lakini hawakuteuliwa, sasa ametokea mtu anayetenda haki ya wengi wape, which is their deserving positions, watu mnaona kama ni upendeleo. Kiukweli they are very good performers, very hard-working and they deliver, tatizo lao ni ushamba tuu, ubishi na Wanaume wao, ule udhaifu wao.

Ushahidi ni hii track record ya performance ya Rais Magufuli, tena tumeanza kushauri, tusindelee kuchagua rais by chances tuu tukaja kujikuta Magufuli anapokelewa na non performer, na kuharibu mazuri yote Magufuli aliyoyaanzisha, hivyo kwa rais ajae baada ya Magufuli, lazima tuanze na kuandaa succession plan kwa kufanya head hunting mapema, kwa kuwa spot presidential materials na kuwafanyia grooming, hatutaki tena rais wa majaribio au wa kubeep, hivyo tumeanza mapendekezo kadhaa akiwemo

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... - JamiiForums

Kwenye pendekezo hilo, hatuangalii kabila kwa sababu kazi ya urais sio kutambika, tunafuata falsafa ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, hatuta mchagua mtu kwa sababu ya kabila lake, na hatuta mkataa mtu kwa sababu ya kabila lake.

Au tufanye kwa zamu baada ya Msukuma, aje Mhaya, Mchagga, tuende hivyo hivyo hadi makabila yote 120 ya Tanzania yatoe rais?.
P
 
Kenya tayari wana Katiba Mpya lakin Matatizo hayajaisha

Kabla ya uhuru Kila kitu walikuwa wanasema ndio sababu tunataka uhuru wakadhan Kila kitu kitakuwa solved kwa kupata uhuru

Tupunguze Kuwa Na 'over expectations'
Haya mambo yanahitaji uelewa wa hali ya juu sana ili kuweza kuelewa utagundua kuwa watu wengi wanachukia jpm ni kwa vile yeye anasema ukweli hataki kukupa matumaini ambayo hayapo lkn binadamu yeye hataki hilo anachotaka ni uhongo uhongo wenye matumaini ambayo wala hawez kufikia.
 
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.

Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile

Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu

Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
Kwa kauli hii sipati picha hali ya Magugumaji huko Chato, he must be wetting his pants!
 
Yuko sahihi Kwenye kuzungumza lakin hayatekelezeki Kwenye Uwanja wa kisheria

Uzi unaotenganisha hayo mambo Mawili ni mwembamba sana

Huo Ufisadi ili aweze kufanya unakuwa Kwenye Wajibu wake wa Urais

Mf. Rais anaweza kusema Tufanye Mradi Fulani let say Ujenzi wa Mradi wa Ununuzi wa Jengo Yeye akaishia hapo
Lakin akatoa Maelekezo Kama Rais nini Cha kufanya

Rejea Sakata la Ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy wakati wa Ubalozi wa Prof Mahalu

Mzee Benjamin Mkapa alifika Mahakamani akasema Ni Yeye ndio aliamuru ifanyike 'Single source' Kwenye mchakato wa Ununuzi akaulizwa Na Wakili wa Serikal wapi aliandika akajibu Maelekezo ya Rais sio lazima yawe kimaandishi anamaliza ushahdi huku anacheka kwa dharau Mahakamani

Tukumbuke Ufisadi huwa unafanyika kwa umakini Sana Hata asie Rais kumtia hatiani sio jambo dogo

Rais fisadi tusidhan anapiga Simu kwa Governor Na kuelekeza awekewe Fedha Kwenye Account Fulani, ingekuwa hivyo ingekuwa Rahisi Sana kumtia hatiani
Sasa ndo umeandika nini wewe mbuzimaji?
 
Nimemjua akiwa mwanza kitambo
Mf Hayati Judge Nixon Chipeta
Aliitwa Buxton David Chipeta. Sio Nixon.
Nimeishi naye kama jirani akiwa Mahakama Kuu Tabora (akiwa na akina Marando, Mushi na Rubama).
Hawa, pamoja na akina Katiti, Rugakingira, etc walikuwa very seroius na kazi yao....no wonder walikuwa wa kuhesabu.[/QUOTE]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom