Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,888
- 143,985
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP
Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam
Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais
Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.
Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile
Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu
Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo
Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums